16-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Kufufua Ardhi Iliyokufa

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ إِحْيَاءِ اَلْمَوَاتِ

16-Mlango Wa Kufufua Ardhi Iliyokufa[1]

 

 

 

 

 

776.

عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ عَمَّرَ أَرْضاً لَيْسَتْ لِأَحَدٍ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهَا} قَالَ عُرْوَةُ: وَقَضَى بِهِ عُمَرُ فِي خِلَافَتِهِ. رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa ‘Urwah naye kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuamrisha (kuendeleza) ardhi isiyo na mwenyewe, basi mtu huyo ana haki zaidi katika ardhi hiyo.” ‘Urwah amesema: ‘Umar alihukumu hukumu hii katika Ukhalifa wake. [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

777.

وَعَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {مَنْ أَحْيَا أَرْضاً مَيْتَةً فَهِيَ لَهُ} رَوَاهُ اَلثَّلَاثَةُ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ.

وَقَالَ: رُوِيَ مُرْسَلاً. وَهُوَ كَمَا قَالَ، وَاخْتُلِفَ فِي صَحَابِيِّهِ، فَقِيلَ: جَابِرٌ، وَقِيلَ: عَائِشَةُ، وَقِيلَ: عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ عَمْرٍو، وَالرَّاجِحُ اَلْأَوَّلُ 

Kutoka kwa Sa’iyd bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuimarisha ardhi iliyokufa, ardhi hiyo ni yake.”[2] [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na At-Tirmidhiy akaipa daraja ya Hassan]

Akisema kuwa imepokewa ikiwa ni Mursal. Hata hivyo hakuna makubaliano kuhusu Maswahaba waliosikia Hadiyth hii kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Inasemekana kuwa ni Jaabir, ‘Aaishah au ‘Abdullaah bin ‘Amr na kauli yenye nguvu ni ya kwanza yaani Jaabir.

 

 

 

778.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ اَلصَّعْبَ بْنَ جَثَّامَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَخْبَرَهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا حِمَى إِلَّا لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema Asw-Swa’b bin Jath-thaamah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimueleza kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna himaya[3] isipokuwa ya Allaah na Nabiy Wake.”[4] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

779.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَابْنُ مَاجَهْ  .

 وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي سَعِيدٍ مِثْلُهُ، وَهُوَ فِي اَلْمُوَطَّإِ مُرْسَلٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halaal kudhuriana wala kulipiziana madhara.”[5] [Imetolewa na Ahmad na Ibn Maajah]

Kadhalika Ibn Maajah ameripoti Hadiyth mfano wa hii kutoka kwa Abuu Sa’iyd. Hadiyth hii inapatikana katika Muwatwa ikiwa ni Hadiyth Mursal

 

 

 

780.

وَعَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {مَنْ أَحَاطَ حَائِطًا عَلَى أَرْضٍ فَهِيَ لَهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْجَارُودِ 

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuzungusha ukuta katika ardhi yoyote (ardhi tupu), ardhi hiyo ni yake.”[6] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Al-Jaaruwd]

 

 

 

781.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ حَفَرَ بِئْرًا فَلَهُ أَرْبَعُونَ ذِرَاعًا عَطَنًا لِمَاشِيَتِهِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuchimba kisima basi ana dhiraa arubaini kwa ajili ya wanyama wake[7] (karibu na maji).” [Imetolewa na Ibn Maajah kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

782.

وَعَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ وَائِلٍ، عَنْ أَبِيهِ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  أَقْطَعَهُ أَرْضًا بِحَضْرَمَوْتَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa ‘Alqamah bin Waail[8] naye kutoka kwa baba yake amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimkatia kipande cha ardhi[9] Hadhwramawt (Yemen).” [Imetolewa na Abuu Daawud na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

783.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  أَقْطَعَ اَلزُّبَيْرَ حُضْرَ فَرَسِهِ ، فَأَجْرَى اَلْفَرَسَ حَتَّى قَامَ ، ثُمَّ رَمَى سَوْطَهُ. فَقَالَ: " أَعْطُوهُ حَيْثُ بَلَغَ اَلسَّوْطُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَفِيهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimkatia ardhi Az-Zubayr kiasi cha kuruka farasi wake, akamkimbiza farasi mpaka akasimama kisha (Az-Zubayr) akarusha mjeledi wake, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema:[10] Mpeni (kipande cha ardhi) hadi ulipofika mjeledi.”[11] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na katika Isnaad yake kuna udhaifu]

 

 

 

784.

وَعَنْ رَجُلٍ مِنْ اَلصَّحَابَةِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {غَزَوْتُ مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ: اَلنَّاسُ  شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي اَلْكَلَأِ ، وَالْمَاءِ ، وَالنَّارِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ 

Mtu mmoja katika Maswahaba amesema: “Nilipigana Jihaad pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) nikamsikia anasema: “Watu ni washirika katika mambo matatu: Majani, maji na moto.” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd na wapokezi wake ni madhubuti]

 

[1] Neno Al-Mawaat nimelitafsiri kwa ‘ardhi iliyokufa’, lakini makusudio ni ardhi ambayo haijaimarishwa, au ardhi isiyo na mmiliki wala hakuna anayenufaika nayo.

 

[2] Ina maana ya kuwa yeyote atakayelima katika ardhi tupu, basi ni yake, maadamu kuwa ardhi hiyo si miliki ya Muislamu au Dhimmi (asiyekuwa Muislamu anayeishi katika nchi ya Kiislamu). Baadhi ya Wanazuoni wana mtazamo kuwa kuomba ruhusa serikali husika nalo ni jambo la lazima, kwa wengine sivyo.

 

[3] Wakati wa Jaahiliyya ilikuwa ni ada mkuu wa ukoo au kabila kutenga ardhi yenye rutuba kulishia mifugo yao. Jambo hili limekatazwa katika Uislamu. Hata hivyo, kiongozi au mkuu wa nchi anaweza kutenga ardhi kama Swadaqah katika njia ya Allaah. Ardhi iliyotolewa Swadaqah kwa kulishia mifugo ni ya Allaah na Nabiy wake. Mkuu wa nchi hawezi kutumia ardhi hii kwa maslaha yake au mifugo yake.

 

[4] Hima ni ardhi ambayo si milki ya mtu. Kiongozi wa Waislamu huwa anaizuwia kwa ajili ya maslahi fulani kama vile kuwalisha wanyama wa Zakaah na kwa dharura nyinginezo.

 

[5] Katika lugha ya kiarabu Dhwaraar ina maaana ya kumdhuru na kumuumiza mwingine pasina haki, na Dhwiraar ni kulipa kisasi kwa aliyeanza kukudhuru. Hadiyth hii ni kanuni ya msingi. Shariy’ah haitaki kudhuru au kudhuriwa kwa yeyote. Mbali na haya kuna maelezo mengi kuhusu Hadiyth hii. Mifano ni mingi katika maisha yetu ambayo watu kwa makusudi wamedhamiria kuwaudhi  wenzao mara kwa mara.

 

[6] Kwa ajili ya ujengaji wa nyumba, kuzungushia ukuta kwa kadiri ya uchache wa futi tatu kuenda juu inathibitisha kuwa ni aliyefanya hivyo, muda wa kuwa ardhi hiyo haina mwenyewe. Hata hivyo, kuthibitisha uhalali wa ardhi ya kilimo ni kwa kulima.

 

[7] Yaani atakayechimba kisima kwa maslahi ya watu, Shariy’ah inamruhusu kuwa na nafasi ya dhiraa arubaini kuzunguka kisima kwa ajili ya mifugo yake.

 

[8] Huyu ni ‘Alqamah bin Waail bin Hujr Al-Hudhrami Al-Kufi, alipokea Hadiyth hii kutoka kwa baba yake na kwa Al-Mughiyrah.

 

[9] Hii ina maana katika dola ya Kiislamu inaruhusiwa kukata kipande cha ardhi kumpa mtu fulani. Kuna aina mbili za hali hii: kutoa kama milki yake na kuruhusu kutumia ardhi kwa muda fulani.

 

[10] Hapa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akizungumza na wale aliokuwa nao pamoja.

 

[11] Dola kutoa zawadi au hiba kwa mtu aliyeutumikia Uislamu na Ummah wake, inaruhusiwa na ni halaal kishariy’ah maadamu kuwa ardhi hiyo si milki ya mtu binafsi. Ama mtu kuzawadiwa kwa kusaliti akipewa na dola isiyokuwa ya Kiislamu ni haraam.

Share