15-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

15-Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo

 

ملاطفة الزوجة

 

 

 

Mume anapoingia kwa mke wake katika siku hii muhimu katika m'Aaishah ya ndoa mara nyingi hisia za khofu na wasiwasi za mwanamke zinakuwa juu, hivyo basi ni juu ya mwanamme kukaa nae kwa upole na kumbembeleza hadi nae ajihisi anaanza kuzoea hali hiyo na kupunguza khofu na wasiwasi aliokuwa nao juu yako. Hekima itumike, ugomvi, matusi au kupiga si mahali pake kabisa, na sio lazima kumuingilia usiku ule ule, unaweza kusubiri hadi asubuhi au hata siku ya pili, mara nyingi mwenye pupa huwa anakosea na matokeo yake yanakuwa ni mabaya (na yenye kudumu katika m'Aaishah mazima ya ndoa yenu).

 

 

Imepokewa kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd bin as-Sakan amesema: “Nilimuendea Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  hali ya kuwa amejipamba kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) nikamuondoa khofu. Baada ya muda kidogo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akaja pembeni yake na kikombe cha maziwa, akayanywa kidogo kisha akampa Bibi 'Aaishah nae akateremsha kichwa chake kwa kuona haya. (Asmaa) nikamnyanyua ('Aaishah), nikamwambia: chukua kutoka kwa mkono wa Mtume wa Allah. ('Aaishah) Akachukua na kuyanywa, kisha (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamwambia, “Wape marafiki zako wa umri wako.” (Ahmad)

 

 

Na si neno kwa mke kumkatalia kidogo mumewe kwani katika hilo mtu husisimkwa, na hujitayarisha, na kunapelekea kumjali zaidi na kumtaka. Na kunanasihiwa kwa wanandoa kuwa ni vizuri wakavua nguo zao zote kama vile mshairi anavyosema:

 

Na tahadhari kuingiliana kunako nguo kwani huo ni ujahili usiokuwa na shaka!

 

Bali kila mlicho nacho – ee, rafiki yangu mkivue

 

Na uwe ni mchezaji nae ili asifadhaike.

 

Ni Sunnah mume kusema anapoingia kwa mkewe siku ya mwanzo:

        

  اللهّم إني أسألك من خيرها وخير ما جبلته وأ عوذ بك من شرها وشّر ما جبلتها عليه

“Ee, Allaah nakuomba kheri yake na kheri aliyokuja nayo na uniepushe na shari yake na shari aliyokuja nayo.” (Abu Daawuwd na Ibn Maajah)

 

 

Du'aa kama hii hutuliza hisia za mwanamke na Nafsi yake na hukaribisha baraka, na huenda kwa hayo Allaah Akajaalia baraka katika usiku huu.

 

 

Share