03-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Nabiy Wa Mwisho

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) 

03-Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Nabiy Wa Mwisho

www.alhidaaya.com

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amethibitisha katika Qur-aan kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Nabiy wa mwisho baada ya Manabii na Rusuli wote, kuanzia Nabiy Aadam ('Alayhis-Salaam) mpaka Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) kisha wa mwisho kabisa ndiye Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab: 30]

 

Wafasiri wa Qur-aan wamesema kwamba inamaanisha hakuna tena Wahyi na Risala kutoka mbinguni, kwa maana Qur-aan ni Kitabu cha mwisho na uthibitiso Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema pia katika kauli Yake Aliyoiteremsha pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposimama Siku ya ‘Arafah kuwakhutubia Maswahaba katika Hijjah yake ya kuaga:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ  

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.  [Al-Maaidah: 3]

 

Na uthibitisho mwengine ni katika Hadiyth zake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضى الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ مَثَلِي وَمَثَلَ الأَنْبِيَاءِ مِنْ قَبْلِي كَمَثَلِ رَجُلٍ بَنَى بَيْتًا فَأَحْسَنَهُ وَأَجْمَلَهُ، إِلاَّ مَوْضِعَ لَبِنَةٍ مِنْ زَاوِيَةٍ، فَجَعَلَ النَّاسُ يَطُوفُونَ بِهِ وَيَعْجَبُونَ لَهُ، وَيَقُولُونَ هَلاَّ وُضِعَتْ هَذِهِ اللَّبِنَةُ قَالَ فَأَنَا اللَّبِنَةُ، وَأَنَا خَاتِمُ النَّبِيِّينَ )) البخاري ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wangu na mfano wa Mananbii wa kabla yangu ni kama mfano wa mtu aliyejenga nyumba akaifanya nzuri na kuipamba isipokuwa sehemu moja ya tofali katika kona. Watu wakawa wanalizunguka na kustaabishwa uzuri wake na husema: “Je, hili tofali litajazwa sehemu yake?” Basi mimi ndio tofali, nami ndiye Nabiy wa mwisho)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na pia:

 

عن أَنَس بْن مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( إِنَّ الرِّسَالَةَ وَالنُّبُوَّةَ قَدِ انْقَطَعَتْ فَلاَ رَسُولَ بَعْدِي وَلاَ نَبِيَّ)) ‏ قَالَ فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَى النَّاسِ فَقَالَ: ((لَكِنِ الْمُبَشِّرَاتُ))‏.‏ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا الْمُبَشِّرَاتُ؟  قَالَ: ((رُؤْيَا الْمُسْلِمِ وَهِيَ جُزْءٌ مِنْ أَجْزَاءِ النُّبُوَّةِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ الترمذي وصححه الالباني (2272)

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamb Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Risala za Unabii zimekatika, kwa hiyo hakuna Rasuli baada yangu wala Nabiy)). Akasema (Anas) Ikawa (khabari) nzito kwa watu kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Isipokuwa Mubash-shiraat [wabashiriaji])) Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah? Nini Mubash-shiraat? Akasema: ((Ndoto ya Muislamu nayo ni chembe ya sehemu  katika sehemu ya Unabiy)) [Hadiyth Hasan, Swahiyh Ghariyb At-Tirmidhiy (2272) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy, na katika Irwaa Al-Ghaliyl kwa daraja ya Swahiyh kwa sharti ya Imaam Muslim, na Imaam Al-Waadi’iy katika Swahiyh Al-Musnad pia kwa daraja ya Swahiyh kwa sharti ya Imaam Muslim]

 

Share