10-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Kulaaniana

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ

Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

 

بَابُ اَللِّعَانِ

 

10-Mlango Wa Kulaaniana[1]

 

 

 

 

935.

عَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {سَأَلَ فُلَانٌ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَرَأَيْتَ أَنْ لَوْ وَجَدَ أَحَدُنَا اِمْرَأَتَهُ عَلَى فَاحِشَةٍ، كَيْفَ يَصْنَعُ ؟ إِنْ تَكَلَّمَ تَكَلَّمَ بِأَمْرٍ عَظِيمٍ، وَإِنْ سَكَتَ سَكَتَ عَلَى مِثْلِ ذَلِكَ! فَلَمْ يُجِبْهُ، فَلَمَّا كَانَ بَعْدَ ذَلِكَ أَتَاهُ، فَقَالَ: إِنَّ اَلَّذِي سَأَلْتُكَ عَنْهُ قَدِ ابْتُلِيتُ بِهِ، فَأَنْزَلَ اَللَّهُ اَلْآيَاتِ فِي سُورَةِ اَلنُّورِ، فَتَلَاهُنَّ عَلَيْهِ وَوَعَظَهُ وَذَكَّرَهُ، وَأَخْبَرَهُ أَنَّ عَذَابَ اَلدُّنْيَا أَهْوَنُ مِنْ عَذَابِ اَلْآخِرَةِ. قَالَ: لَا، وَاَلَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ مَا كَذَبْتُ عَلَيْهَا، ثُمَّ دَعَاهَا اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَوَعَظَهَا كَذَلِكَ، قَالَتْ: لَا، وَاَلَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ إِنَّهُ لَكَاذِبٌ، فَبَدَأَ بِالرَّجُلِ، فَشَهِدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ، ثُمَّ ثَنَّى بِالْمَرْأَةِ، ثُمَّ فَرَّقَ بَيْنَهُمَا} رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Fulani aliuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Nieleze lau mmoja wetu atamkuta mkewe katika machafu (zinaa) afanye nini? Ikiwa atazungumza basi atasema jambo kubwa, na ikiwa atanyamaza, atanyamazia kitu kibaya.” Wala hakumjibu. Baada ya hapo akamuendea tena, akasema: “Lile swali nililokuuliza mimi nimejaribiwa nalo.” Allaah akateremsha Aayah katika Suwrah An-Nuwr, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamsomea Aayah hizo akamnasihi akamkumbusha na akamueleza kuwa adhabu ya duniani ni sahali kuliko adhabu ya Aakhirah. Akasema: “Hapana, naapa kwa aliyekutuma kwa haki sikumzulia uongo!” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuita (mwanamke) akamnasihi vile vile. Mwanamke akasema: “Hapana naapa kwa Aliyekutuma kwa haki yeye ni muongo!” Akaanza kwa mwanamume, akashuhudilia mara nne kwa kiapo cha Allaah. Halafu akamgeukia yule mwanamke (akashuhudia kama yule mume), kisha akawaachanisha.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

936.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَيْضًا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ لِلْمُتَلَاعِنَيْنِ: "حِسَابُكُمَا عَلَى اَللَّهِ تَعَالَى، أَحَدُكُمَا كَاذِبٌ، لَا سَبِيلَ لَكَ عَلَيْهَا" قَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَالِي ؟ قَالَ: "إِنْ كُنْتَ صَدَقْتَ عَلَيْهَا، فَهُوَ بِمَا اِسْتَحْلَلْتَ مِنْ فَرْجِهَا، وَإِنْ كُنْتَ كَذَبْتَ عَلَيْهَا، فَذَاكَ أَبْعَدُ لَكَ مِنْهَا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) alisema tena kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaambia wale waliolaaniana: “Hisabu yenu iko kwa Allaah.[2] Mmoja wenu ni muongo, wewe (mume) huna njia ya kumrudia mkeo.” Yule mume akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mali yangu?” Akasema: “Ikiwa ulisema kweli kumhusu yeye (mwanamke) basi mali hiyo ni kwa uchi wake uliojihalalishia.[3] Na ikiwa umemzulia uongo basi mali hiyo iko mbali nawe zaidi kuliko huyo (mwanamke).” [Al-Bukaariy, Muslim]

 

 

 

937.

وَعَنِ أَنَسٍرَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {أَبْصِرُوهَا، فَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أَبْيَضَ سَبِطًا فَهُوَ لِزَوْجِهَا، وَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أَكْحَلَ جَعْدًا، فَهُوَ اَلَّذِي رَمَاهَا بِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtizameni, ikiwa aliyezaliwa ni mweupe maumbile yake yamekamilika basi ni wa mume wake, na akiwa  macho yake ni kama yaliyopaka wanja na nywele koto basi huyo ni wa aliyemsingizia uzinifu (uzinzi).”[4] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

938.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  أَمَرَ رَجُلاً أَنْ يَضَعَ يَدَهُ عِنْدَ اَلْخَامِسَةِ عَلَى فِيهِ، وَقَالَ: "إِنَّهَا مُوجِبَةٌ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamrisha mtu aweke mkono wake mdomoni[5] mwake katika ile mara ya tano na akasema: “Itawajibisha.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nisaaiy na wapokezi wake ni Madhubuti]

 

 

 

939.

وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍرَضِيَ اللهُ عَنْهُ   فِي قِصَّةِ اَلْمُتَلَاعِنَيْنِ قَالَ: {فَلَمَّا فَرَغَا مِنْ تَلَاعُنِهِمَا قَالَ: كَذَبْتُ عَلَيْهَا يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنْ أَمْسَكْتُهَا، فَطَلَّقَهَا ثَلَاثًا قَبْلَ أَنْ يَأْمُرَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Sahl bin Sa’d (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kisa cha wale waliolaaniana: “Walipomaliza kulaaniana kwao mume alisema: “Nitakuwa nimemsingizia Ee Rasuli wa Allaah! Kama nitakuwa naye.” Akamtaliki talaka tatu[6] kabla ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumuamrisha kufanya hivyo.” [Al-Bukhaariy, Muslim

 

 

 

940.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَجُلاً جَاءَ إِلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَقَالَ: إِنَّ اِمْرَأَتِي لَا تَرُدُّ يَدَ لَامِسٍ. قَالَ: "غَرِّبْهَا". قَالَ: أَخَافُ أَنْ تَتْبَعَهَا نَفْسِي. قَالَ: "فَاسْتَمْتِعْ بِهَا"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالْبَزَّارُ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ.

وَأَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ: عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ بِلَفْظٍ{قَالَ: طَلِّقْهَا. قَالَ: لَا أَصْبِرُ عَنْهَا. قَالَ: "فَأَمْسِكْهَا}

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Mtu mmoja alimuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Mke wangu harudishi mkono wa mwenye kugusa.”[7] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Mhamishe.” Akasema: “Nahofia kumfuata.”  Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Basi starehe naye.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Al-Bazzaar, na wapokezi wake ni waaminifu (madhubuti)]

 

Na An-Nasaaiy ameipokea kwa njia nyingine kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwa lafdhi: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Mtaliki.” Yule mtu akasema: “Siwezi kuwa mbali naye.” Akamuambia: “Basi baki naye.”

 

 

 

941.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقُولُ حِينَ نَزَلَتْ آيَةُ اَلْمُتَلَاعِنَيْنِ: "أَيُّمَا اِمْرَأَةٍ أَدْخَلَتْ عَلَى قَوْمٍ مَنْ لَيْسَ مِنْهُمْ، فَلَيْسَتْ مِنْ اَللَّهِ فِي شَيْءٍ، وَلَنْ يُدْخِلَهَا اَللَّهُ جَنَّتَهُ، وَأَيُّمَا رَجُلٍ جَحَدَ وَلَدَهُ وَهُوَ يَنْظُرُ إِلَيْهِ اِحْتَجَبَ اَللَّهُ عَنْهُ، وَفَضَحَهُ اَللَّهُ عَلَى رُءُوسِ اَلْخَلَائِقِ اَلْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Alimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema iliposhuka Aayah[8] ya wanaolaaniana: “Mwanamke yeyote amemuingiza katika watu asiye miongoni mwao[9] basi mwanamke huyo hana kitu kwa Allaah na Allaah Hatamuingiza katika Jannah Yake, na mwanaume yeyote anayekana mtoto wake naye anamuangalia, Allaah Atajitenga naye na Atamfedhehesha mbele ya watu wa mwanzo na wa mwisho.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

942.

وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ:{مَنْ أَقَرَّ بِوَلَدٍ طَرْفَةَ عَيْنٍ، فَلَيْسَ لَهُ أَنْ يَنْفِيَهُ} أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ، وَهُوَ حَسَنٌ مَوْقُوف

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mwenye kumkiri mtoto wake japo kwa kupepesa jicho hana haki ya kumkana.”[10] [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy, na Hadiyth hii ni Hasan na Mawquwf]

 

 

 

943.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ   {أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ اِمْرَأَتِي وَلَدَتْ غُلَامًا أَسْوَدَ ؟ قَالَ: "هَلْ لَكَ مِنْ إِبِلٍ ؟" قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "فَمَا أَلْوَانُهَا ؟" قَالَ: حُمْرٌ. قَالَ: "هَلْ فِيهَا مَنْ أَوْرَقَ ؟"، قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "فَأَنَّى ذَلِكَ ؟"، قَالَ: لَعَلَّهُ نَزَعَهُ عِرْقٌ. قَالَ: "فَلَعَلَّ اِبْنَكَ هَذَا نَزَعَهُ عِرْقٌ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ:{وَهُوَ يُعَرِّضُ بِأَنْ يَنْفِيَهُ}، وَقَالَ فِي آخِرِهِ:{وَلَمْ يُرَخِّصْ لَهُ فِي اَلِانْتِفَاءِ مِنْهُ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Mtu mmoja alimuendea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mke wangu amejifungua mtoto mweusi.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Je, una ngamia?” Akasema: “Ndio.”  Akasema: “Ni rangi gani?” Akasema: “Ni wekundu.” Akasema: “Je kuna mwenye rangi nyeusi miongoni mwao?” akasema: “Ndio.”  Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Imekuwaje hilo?” Akasema: “Pengine amerithi hilo.” Akasema: “Na huyu (pia) yawezekana katika baba (na babu) zake yuko aliyekuwa na rangi hiyo na pia ikampata.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah nyingine ya Muslim inasema: “Naye anazungumza kwa mafumbo ili amkane mtoto wake.” Amesema mwisho wake: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakumkubalia kumkana mtoto wake.”

 

[1] Al-Li’aan inamaanisha kumtuhumu mmoja wa wanandoa kuwa amezini, bila ya kuwepo kwa ushahidi madhubuti. Ikiwa mwanamke anakana tuhuma, mwanamme analazimika kuapa viapo vine akirejea tuhuma katika kila kiapo, cha tano atasema: “Ghadhabu ya Allaah inishukie ikiwa nimesema uongo.” Ikiwa mwanamke atakaa kimya ataadhibiwa. Hata hivyo akikana hutuma, atawajibika kuapa viapo vinne akikana tuhuma ile katika kila kiapo na katika kiapo cha tano atasema: “Ikiwa anasema kweli basi laana ya Allaah iniangukie.” Laana hii inayokusudiwa hapa inarejea katika Li’aan. Li’aan maana yake ni kuwajibisha kutengana, hakuna njia nyingine ya hawa wawili kuoana tena.

[2] Katika Hadiyth hii umuhimu umewekwa katika kufanya toba ya dhambi aliyokuwa nayo mtu.

 

[3] Hii ina maana kwamba mahari ya mwanamke haiwezi kurejeshwa tena kwa mume.

[4] Hadiyth hii inahusu mambo matatu: Kwanza, kuhusu mas-ala ambayo hayajawekwa wazi na wahyi, mambo hayo huwa yanatolewa ufafanuzi na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Pili: Ikiwa dalili za msingi ya maamuzi ya jambo hayapo, kuamua kwa kudhania kunakubaliwa. Tatu: kuhusu suala la Li’aan, hata ikiwa kudhania kumesibu, mwanamke hawezi kuadhibiwa kwa uzinifu.

 

[5] Kuweka mkono mdomoni ni dalili ya kumzindua mtu kwa kiapo cha mwisho; baada ya kiapo hiki majukumu yanarudi kwao katika maisha haya na ya kesho Aakhirah. Ikiwa mwanamme atanyamaza kwenye kiapo cha tano ataadhibiwa kwa kumsingizia na kumkashifu. mwanamke ana haki ya kufanya Li'aan akitaka.

[6] Baada ya Li’aan hakuna haja tena ya kutoa talaka, wakati huo talaka inakuwa imeshatoka. Baada ya Li’aan mwanamke hana haki ya kupokea masrufu yoyote.

[7] Ina maana nyingi: Kwanza, ni hajali anapokutana na ajnabi. Pili: ni mzinifu. Tatu: si muangalizi mzuri wa mali ya mume wake. Maana ya kwanza ndio inayoelekea kuwa sahihi zaidi. Ingekuwa maana ya pili ni sahihi basi mwenye kutuhumu inabidi aje na mashahidi, na hapo basi Li’aan itabidi ifanyike, au mwanamke angeadhibiwa. Hata hivyo yote haya hayakufanyika. Kinyume chake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtaka avumilie. Lau maana ya pili ingekuwa sahihi, basi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) angekuwa ameruhusu yule bwana kuwa Dayyuwth (mtu asiyejali tabia mbaya aliyouwa nayo mwanamke ambaye yumo katika himaya yake)

[8] Angalia Suwrah An-Nuwr aayah ya 6 (24:6)

 

[9] Hii ina maana ya kuzaa mtoto ambaye si halaal kisha kuonesha kuwa ni halaal. Suala hili linaleta matatizo mengi katika mirathi, mambo ya kishariy’ah na mas-ala ya ndoa, n.k.

[10] Hatakiwi mtu kumkana mtoto wake, muda wa kuwa uzazi umeshakubalika, ikiwa hali imejitokeza hivyo, kwa upande mmoja, atakuwa ni mtoto wa kitendo cha haraam, na kwa upande wa pili mama yake atakuwa ametuhumiwa uzinifu na mtoto atatengwa na mirathi.

Share