066-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tahriym Aayah 1-5: يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ

 

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

066-At-Tahriym Aayah 1-5

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu, na Allaah ni Mola wenu Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ﴿٣﴾

 

3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri, na huyo mke alipoipasha habari na Allaah Akamdhihirishia (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), akataarifu baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha hayo, akasema: “Nani aliyekujulisha haya?” Akasema: “Amenijulisha Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.”

 

 

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.

 

 

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾

 

5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.

 

 

Sababun-Nuzuwl (1):

 

حَدَّثَنِي الْحَسَنُ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ صَبَّاحٍ، حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ زَعَمَ عَطَاءٌ أَنَّهُ سَمِعَ عُبَيْدَ بْنَ عُمَيْرٍ، يَقُولُ سَمِعْتُ عَائِشَةَ  رضى الله عنها   أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَمْكُثُ عِنْدَ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ، وَيَشْرَبُ عِنْدَهَا عَسَلاً، فَتَوَاصَيْتُ أَنَا وَحَفْصَةُ أَنَّ أَيَّتَنَا دَخَلَ عَلَيْهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلْتَقُلْ إِنِّي أَجِدُ مِنْكَ رِيحَ مَغَافِيرَ، أَكَلْتَ مَغَافِيرَ فَدَخَلَ عَلَى إِحْدَاهُمَا فَقَالَتْ لَهُ ذَلِكَ، فَقَالَ ‏"‏ لاَ بَلْ شَرِبْتُ عَسَلاً عِنْدَ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ وَلَنْ أَعُودَ لَهُ ‏"‏‏.‏ فَنَزَلَتْ:‏ ((‏يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ‏)) إِلَى: ((إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ‏))‏ لِعَائِشَةَ وَحَفْصَةَ ‏  ((وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَى بَعْضِ أَزْوَاجِهِ‏))‏ لِقَوْلِهِ ‏"‏ بَلْ شَرِبْتُ عَسَلاً ‏"‏‏.‏

 

Amenihadithia Al-Hassan bin Muhammad bin As-Swabbaah amenihadithia Hajaaj kutoka kwa Ibn Jurayj amesema: ‘Atwaa alisema kuwa alimsikia ‘Ubayd bin ‘Umayr akisema nimemsikia ‘Aaishah (Radhwiya Allahu ‘anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa na kushinda kwa Zaynab bint Jahsh na huwa akinywa kwake asali. Mimi (‘Aaishah) nikakubaliana na Hafswah kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakapoingia kwa mmoja wetu basi   aseme: “Mimi nasikia kwako harufu ya Maghaafiyr (ubani unatoka katika mti), je umekunywa Maghaafiyir?” Akafika kwa mmoja wao na akamwambia yeye hivyo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: ((Hamna neno nilikunywa asali kwa Zaynab bint Jahsh na sitorudui kufanya hivyo tena)). Baada ya hapo ikateremka:

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ

 

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah?

 

Hadi

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah…  

 

(imekusudiwa ‘Aaishah na Hafswah)

 

Na ikateremka tena:

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا  

3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri,  

 

Kuhusu kauli yake: ((Bali nilikunywa asali))

 

[Al-Bukhariy Kitaab Atw-Twalaaq]

 

 

Sababun-Nuzuwl (2):

 

 عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَتْ لَهُ أَمَةٌ يَطَؤُهَا فَلَمْ تَزَلْ بِهِ عَائِشَةُ وَحَفْصَةُ حَتَّى حَرَّمَهَا عَلَى نَفْسِهِ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏: ‏ يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ   ‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kijakazi (Maariyah Mkoptic) ambaye alikuwa akimwingilia, lakini  ‘Aaishah na Hafswah (kutokana na wivu wa kiuke) waliendelea kumbana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa vitimbi na visavisa) mpaka  akafanya kuwa ni haraam kwa nafsi yake, hapo Allaah Akateremsha:

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

[An-Nasaaiy kama ilivyo katika Tafsiyr Ibn Kathiyr (Juz 4 uk 386) na Al-Hakam (Juz 2 uk 493) na akasema ipo katika shuruti za Muslim na ikathibitishwa na Adh-Dhahabiy]

 

 

Pia:

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas (Radhwiya Allaahu ‘ahumaa) kwamba Aayah

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ  

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako;  

 

imeteremka hii kuhusu kijakazi wake .

 

[Majma’ Az-Zawaaid (Juz 7 uk 126) Imepokewa na Al-Bazzar kwa Isnaad mbili na At-Twabaraaniy na wapokezi wa Al-Bazzar ni wapokezi sahihi isipokuwa mmoja ambaye ni Bishri bin Adam nae ni Thiqqha (mwaminifu)].

 

 

Pia:

 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alimwambia Hafswa, “Usimwambie mtu kwa hakika Ummu Ibraahiym ni haraam kwangu.” Hafswah akasema: Unaharamisha Alilokuhalalishia Allaah? Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema, “Wa-Allahi simkurubii.” Akasema: Hivyo hakumkurubia hadi (Hafswah) akamwelezea ‘Aaishah akasema baada ya hapo Allaah Akateremsha:

 

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu. 

[Imepokewa na Al-Haytham bin Kuleyb katika musnad yake kama ilivyo katika tafsiri ya Ibn Kathiyr (Juz 4 uk 386)]

 

Al-Haafidhw amesema katika Al-Fat-h (Juz 10 Uk 283): “Inayumkinika Aayah ikawa imeteremka kwa sababu mbili mpigo; yaani kujiharamishia asali na kujiharamishia kijakazi wake.”

 

Ash-Shawkaaniy amesema katika tafsiri yake (Juz 5 Uk 252): “Na hizi ni sababu mbili sahihi za kuteremka Aayah, na kuzikusanya pamoja kunawezekana kwa kutokea visa viwili; kisa cha asali na kisa cha kijakazi (Maariyah Al-Qubtwiyyah), na kwamba Qur-aan iliteremka kuhusiana na visa hivyo viwili kwa pamoja, na katika kila kisa kati ya viwili, yeye alizungumza kwa siri kwa baadhi ya wakeze.”

 

 

 

Share