011-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuingia Nyumbani

Hiswnul-Muslim

011-Du’aa Ya Kuingia Nyumbani

www.alhidaaya.com

 

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

 

[18]

    بِسْـمِ اللهِ وَلَجْنـا، وَبِسْـمِ اللهِ خَـرَجْنـاَ، وَعَلـى رَبِّنـا تَوَكّلْـناَ

 

BismiLLaahi walajnaa, wa BismiLLaahi kharajnaa, wa ’alaa Rabbinaa tawakkalnaa

 

Kwa jina la Allaah tunaingia, na kwa jina la Allaah tunatoka, na Rabb wetu tumetawakali[1]

 

Kisha asalimie watu walio ndani kwa maamkizi ya Kiislamu:

 

السَّلامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ

”Assalamu ‘alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh”.

 

 

 


[1]Abu Maalik Al-Ash’ariyy (wametofautiana jina lake; wengine wamesema: ‘Ubayd au ‘Abdullaah, au ‘Amruw, au Ka’ab bin Ka’ab au ‘Aamir bin Al-Haarith (رضي الله عنه)   - Abu Daawud (4/325), na Isnaad yake imepewa daraja ya Hasan na Ibn Baaz katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 28), na Majmuw’ Fataawaa Ibn Baaz (26/35).

 

 

Tanbihi: Imaam Al-Albaaniy ameidhoofisha Du'aa ifuatayo ambayo inaanza kwa tamshi la ziyada:

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ الْمَوْلَجِ ، وَخَيْرَ الْمَخْرَجِ ، بِسْمِ اللَّهِ وَلَجْنَا، وَبِسْمِ اللَّهِ خَرَجْنَا، وَعَلَى اللَّهِ رَبِّنَا تَوَكَّلْنَا، ثُمَّ لِيُسَلِّمْ عَلَى أَهْلِهِ

 

Imaam An-Nawawiy amesema katika Al-Adkhaar (23): “Inapendekezeka mtu anapoingia katika nyumba aseme: 

بسم الله

Na akithirishe kumdhukuru Allaah (عزّ وجلّ), kutokana na kauli ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

(( فإذَا دَخَلْتُمْ بُيُوتاً فَسَلِّمُوا على أنْفُسِكُمُ تَحِيَّةً مِنْ عِنْدِ اللَّهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَة))  

[An-Nuwr: 61].”

 

Na pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:  

إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيْتَهُ فَذَكَرَ اللَّهَ عِنْدَ دُخُولِهِ وَعِنْدَ طَعَامِهِ  قَالَ الشَّيْطَانُ : لا مَبِيتَ لَكُمْ وَلا عَشَاءَ))

((Atakapoingia mtu nyumbani kwake akamdhukuru Allaah wakati wa kuingia na katika chakula, shaytwaan husema: Hakuna malazi wala chakula cha usiku)) [Muslim] [2018]

 

 

 

Share