031-Hiswnul-Muslim: Ipasavyo Kufanya Na Kusema Mwenye Kuota Ndoto Njema Au Mbaya

Hiswnul-Muslim

031-Ipasavyo Kufanya Na Kusema Mwenye Kuota Ndoto Njema Au Mbaya

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[114]

 

Anayeota ndoto mbaya anatakiwa afanye yafuatayo:  

 

1- Atafili (ateme mate) kushotoni kwake mara tatu.

 

2-Aombe kinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan kwa shari aliyoiota (aseme:

 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم

A’uwdhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym – mara tatu)

 

 

3-Asimuhadithie mtu yeyote[1]  

 

 

4-Agueuke upande mwengine (alioota ndoto mbaya)[2]    

 

 

[115]

 

5-Ainuke kuswali akitaka[3]   

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Qataadah bin Rib-’iyy;  imesemekana jina lake pia ni: Al-Haarith na pia imesemekana ni: ‘Amruw (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:  ((Ndoto nzuri inatoka kwa Allaah, na ndoto mbaya ni kutoka kwa shaytwaan. Atakapoota mmoja wenu kinachomchukiza, basi atakapozindukana, apulize kushotoni mwake mara tatu na aombe kinga kwa Allaah kutokana na shari yake, basi hakitamdhuru [kitu])). Na riwaayah nyingine: ((Atakayeota mmoja wenu atakachokipenda, asimhadithie yeyote isipokuwa yule anayempenda. Na atakapoota anachokichukia asimhadithie mtu, na atafili (ateme mate) kushotoni mwake mara tatu na aombe kinga kwa Allaah kutokana na shaytwaanir-rajiym kwa shari aliyoiota, basi haitamdhuru [kitu])) Kauli hizo ni kutoka Hadiyth katika Muslim (4/1772) [2261], Al-Bukhaariy [7044].   

[2]Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayeoota mmoja wenu ndoto anayoichukia, atafili (ateme mate) kushotoni mwake mara tatu, na aombe kinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan mara tatu, na ageuke [kulala] upande mwengine)) - Muslim (4/1773) [2262].   

[3]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: “Muda utakapokuwa mfupi, njozi ya Muumini itakuwa haiongopi tena, na mwenye njozi ya kweli zaidi kati yenu ni yule aliye msema kweli zaidi, na njozi ya Muumini ni sehemu moja kati ya sehemu 46 za Unabii.  Na ndoto ni aina tatu: Njozi njema ambayo ni bishara toka kwa Allaah, na ndoto ya kuhuzunisha itokanayo na shaytwaan, na ndoto kutokana na mtu kuizungumzisha nafsi yake (mawazo yaliyotawala zaidi kwenye akili yake).” [Muslim (2263]4/1773)]

 

 

Share