Keki Ya Maziwa Kwa Icing Ya Zaafarani

Keki Ya Maziwa Kwa Icing Ya Zaafarani

 

Vipimo

 

Siagi -  Kikombe 1

Sukari -  Kikombe 1 

Unga - Vikombe 2 

Maziwa -  1/2 (nusu) Kikombe 

Mayai -  4

Baking Powder - 1 Kijiko cha supu

Arki rose -  kidogo

Icing ya kawaida

Zaafarani kiasi

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
  2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
  3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
  4. Mimina baking powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
  5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
  6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
  7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
  8. Epua iache ipoe.
  9. Tengeneza Icing ya kawaida, na roweka zaafarani kidogo.
  10. Mwagia Icing na nyunyizia zaafarani.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share