049-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kumtembelea Mgonjwa

Hiswnul-Muslim

049-Du’aa Ya Kumtembelea Mgonjwa

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[147]

 

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

Laa ba-asa twahuwrun In Shaa Allaah

 

Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi) Akipenda Allaah[1]

 

 

 

[148]

أَسْـأَلُ اللهَ العَـظيـم، رَبَّ العَـرْشِ العَـظيـم أَنْ يَشْفِـيَك

 

As-aluLLaaha Al-‘Adhwiyma Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiymi an Yashfiyak (mara 7)

 

 Namuomba Allaah Mtukufu Rabb wa ‘Arshi Tukufu Akuponyeshe[2]

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (10/118) [3616].

 

كَانَ النَّبِيّ صّلّى الله عليه وسلم إِذا دَخَلَ عَلى الْم إذا دخل على من يعوده قال: :لا بأس، طهور إن شاء الله

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa anapoingia kumzuru mgonjwa akimwambia:

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

 

[2]Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) - Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hapana mja yeyote Muislamu anaemtembelea mgonjwa ambae wakati wake wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba, isipokuwa   Allaah Humponyesha mgonjwa huyo)) At-Tirmidhiy [2083], Abu Daawuwd [3106], Taz pia Swahiyh At-Tirmidhiy (2/210), Swahiyh Al-Jaami’ (5/180) [5766].

 

 

Share