109-Hiswnul-Muslim: Namna Ya Kumrudishia Salaam Kafiri Anapokusalimia

Hiswnul-Muslim

109-Namna Ya Kumrudishia Salaam Kafiri Anapokusalimia

www.alhidaaya.com

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

[227]

 

إِذَا سَلَّم عَلَيْكُمْ أهْلُ الكِتَابِ؛ فَقُولُوا: وَعَلَيْكُمْ

 

Ahlul-Kitaab (Mayahudi na Manaswara) wakikuamkieni (maamkizi ya maangamizi) semeni:

وَعَلَيْكُمْ

Wa ’alaykum

 

Na juu yenu[1]

 

 

 

 


[1] Hadiyth ya Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/42) [6258], Muslim (4/1705) [2163].

 

Tanbihi:  Lakini wakikusalimieni kwa maamkizi mema yaliyo bayana na sahihi yaani wakisema:

 

السَّلامُ عَلَيْكُم

 

”Assalaamu ’alaykum”

 

Basi jibuni vizuri kama vile Alivyomrisha Allaah (سبحانه وتعالى) yaani mjibu:

وعليكم السلام

Wa ’alaykumussalaam

 

Imethibiti hivyo kutoka kwa ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuhusu Aayah:

 

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ

Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.  [An-Nisaa 4: 86] – Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad [1107]

 

 

Ama wakikuamkieni kwa matamshi yasiyokuwa bayana kama vile ”assaam ’alaykum” bila ya kutamka herufi ya laam ambayo inapeleka kuleta maana ya: ”mauti yawe juu yenu”, basi ndio mjibu hivyo: ”Wa ’alaykum”

 

Hadiyth ya Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((إِذَا سَلَّمَ عَلَيْكُمُ الْيَهُودُ فَإِنَّمَا يَقُولُ أَحَدُهُمُ السَّامُ عَلَيْكُمْ فَقُولوا: وَعَلَيْكَ))

 

((Akikusalimieni Myahudi, kawaida husema “Assaam ‘alaykum (mauti yakufikeni), basi semeni: “wa ‘alayka” (na kwako yakufikie)) Al-Bukhaariy [6257], Muslim [2164].

 

 

 

 

Share