120-Hiswnul-Muslim: Adkhkaar Katika Mash’arul-Haraam (Muzdalifah)

 Hiswnul-Muslim

120-Adkhkaar Katika Mash’arul-Haraam (Muzdalifah)

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[238]

 

حَدِيْث جَابِر بن عَبْدِ الله  (رضي الله عنهما): رَكِبَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم الْقَصْوَاءَ حَتَّى أَتَى الْمَشْعَرَ الْحَرَامَ فَاسْتَقْبَلَ الْقِبْلَةَ (فَدَعاهُ  وَكَبَّرَهُ، وَهَلَّلَهُ، وَوَحَّدَهُ) فَلَمْ يَزَلْ وَاقِفاً حَتَّى أسْفَرَ جِداً فَدَفَعَ قَبْلَ اَنْ تَطْلُعَ الشَّمْسُ

 

Hadiyth ya Jaabir (رضي الله عنه)    kwamba: ”Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alimpanda Al-Qaswa (jina la ngamia wake) mpaka alipofika Mash’arul Haraam (Muzdalifah), kisha akaelekea Qiblah akamuomba Du’aa kwa Allaah, akaleta takbiyr  (akamtukuza - Allaahu Akbar), akaleta Tahliyl (akampwekesha – laa ilaaha illa Allaah) akamkanusha kuweko mwabudiwa mwengine na akampwekesha. Hakuacha kusimama mpaka kulipopambazuka ndipo alipoondoka kabla ya kutoka jua”[1]

 

 

 

[1]Muslim (2/891) [1218]

 

Faida:  Sehemu hiyo ya Muzdalifah Haajj anapaswa kumdhukuru Allaah (عزّ وجلّ) kwa kila aina ya Adhkaar, kuswali Jamaa’ah, na kuomba Du’aa, kuomba maghfirah, kumshukuru na kumsifu Allaah (عزّ وجلّ)  na kadhaalika.

 

 

Share