122-Hiswnul-Muslim: Du’aa Wakati Wa Kustaajabu Na Wa Furaha

Hiswnul-Muslim

122-Du’aa Wakati Wa Kustaajabu Na Wa Furaha

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

[240]

 

سُبْحَانَ اللهِ!

Subhaana Allaah!

 

Utakasifu ni wa Allaah[1]   

 

 

 

 [214] 

 

اللهُ أَكْبرُ!

Allaahu Akbar!

 

Allaah ni Mkubwa[2]

 

 

 

[1]Katika riwaaya kadhaa zenye maudhui kadhaa zimetajwa kauli hizo mbili; Subhaana Allaah! Allaahu Akbar! Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (1/210) [155], [390] [283], Muslim [371], [414], [314] na  (4/1857) [332]. Miongoni mwa riwaaya ni Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) :

 

أن النبي صلى الله عليه وسلم لقيه في بعض طريق المدينة وهو جنب فانخنس منه فذهب فاغتسل ثم جاء فقال: ((أين كنت يا أبا هريرة)) قال: كنت جنبا فكرهت أن أجالسك وأنا على غير طهارة. فقال: ((سبحان الله إن المسلم لا ينجس))

Nabiy alikutana naye katika mtaa mmojawapo wa Madiynah naye akiwa katika hali ya janaabah, akamkwepa akaenda kuoga kisha akarudi. Akamuuliza: ((Ulikuwa wapi ee Abaa Hurayrah?)) akajibu: “Nilikuwa katika hali ya janaabah hivyo nilichukia kukaa nawe na hali siko katika twahaarah”. Akasema: ((Subhaanah Allaah! Muislamu si najsi)) Al-Bukhaariy.

 

 

Tanbihi Kuhusu Kosa Lilozoeleka Katika Jamii: Sio kusema: ”Mtume!” kama ilivyozoeleka kwa wengi wanapopatwa na jambo kama kujikwaa au kusikia habari ya mshtuko na kadhaalika. Kumtaja Nabiy (صلى الله عليه وسلم) ni kumpandisha cheo cha Allaah, jambo ambalo yeye mwenyewe Nabiy (صلى الله عليه وسلم) amelikemea kulinganishwa Naye kwa sababu yeye ni kiumbe asiyeweza kumnufaisha mtu wala kumdhuru mtu. Tahadhari Muislamu kwani kumtaja Nabiy (صلى الله عليه وسلم) katika hali kama hizo kunapeleka kuwa ni shirki na ambayo ni dhambi kubwa!

 

 

[2]Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (8/441) [4741], na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (2/103) na (2/235), na Musnad ya Ahmad (5/218)

 

 

 

 

Share