Maelekezo Kuhusu Utoaji Wa Zakaah

SWALI:

 

asalam alaikum wa rahmatullahi wabarakat mimi natowa pongezi zangu kwa wa kurugenzi wa chombo cha alhidaaya nimenufaika sana na chombo hiki nawa ombeya kwa mwenyezimungu awalipe kila la hery kwa juhudi yenu yakumtumikiya allahuma amin, swali langu ni nasumbuka sana na swala la zaka kwetu hakuna baitul mali nimejaribu siku moja shehe baidhi ya viongozi wa dini kwetu anielekeze namna ya zaka ili nimpe akanihesabiya visivyo nikampa baada ya kuuliza ungine shehe akanambiya vyenye vinapaswa kutolewa zaka ni vitu ambavyo ni mali umengayi biashara apana gari yako na nyumba yako na viwanja hata haujajenga kama ungelikuwa pakawa watu wanalipa kodi sawa, na sijuwi kama zimewafikiya wahitaji allahu ya allam sasa mimi nishidwa gisi ntafanya naomba kwa ajili ya mwenyezimungu inshaallah

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu utoaji wa Zakaah.

Hakika Zakaah inatolewa kwa akiba iliyoiweka ikafikiwa na kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah; kiwango hicho huitwa ‘Niswaab’, pia dhahabu na fedha na wanyama wa mifugo na mazao ya ukulima. Katika tulivyovitaja juu vina masharti mawili makuu ili kupaswa kutolewa zakaah. Masharti yenyewe ni:

 

1.   Kufikiwa na Niswaab (kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah). Kwa pesa taslimu ni kuwa na akiba inayoweza kununua gramu 85 ya dhahabu safi. Na dhahabu ni kuwa na gramu 85 ilhali fedha ni gramu 595. Ama wanyama inategea kwa mbuzi na kondoo ni kuwa na idadi iliyo 40 ilhali ngamia ni 5. Na mazao ni wakati wa kuvuna.

 

2.   Kupitiwa na Hawl (mwaka mzima katika kalenda ya Kiislamu).

 

Ama ikiwa una nyumba au gari au vyombo vya nyumbani hivi havitolewi Zakaah ila ikiwa ni vya biashara. Ikiwa nyumba umeikodisha au gari linafanyiwa kazi utaanza kulipa tu Zakaah ikiwa katika akiba kwa unachopata itafikia kiwango cha kutolewa Zakaah basi itabidi ufanye hesabu kwa unachopata katika mapato yako. Na wakati inafika Niswaab utaweka hiyo tarehe kwani ikifika mwaka unaofuatia ikiwa bado iko katika kiwango hicho au zaidi itabidi utoe 2½% ya akiba hiyo kuwapatia wale waliotajwa katika Suratut Tawbah 9: aayah 60.

 

Zaidi, unaweza kufaidika kwa makala zinazohusiana na Zakaah hapa chini:

 

Zakaah Na Viwango Vyake

 

 

Umuhimu Wa Zakaah - 1: Umuhimu Wa Kutoa Zakaah Na Malengo Yake

Umuhimu Wa Zakaah - 2: Masharti Yanayomuwajibikia Mwenye Kutoa Zakaah

Umuhimu Wa Zakaah - 3: Zakaah Ya Mapambo Ya Dhahabu

Umuhimu Wa Zakaah - 4: Zakaah Ya Bidhaa Na Mali Ya Biashara

Umuhimu Wa Zakaah - 5: Zakaah Ya Fedha Taslimu

Umuhimu Wa Zakaah - 6: Zakaah Ya Mali Ya Haraam

Umuhimu Wa Zakaah - 7: Wanaostahiki Kupewa Zakaah

Umuhimu Wa Zakaah - 8: Wasiostahiki Kupewa Zakaah

Umuhimu Wa Zakaah - 9: Masaail Ya Ziada Kuhusu Zakaah

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share