02-Imaam Ibn Baaz: Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Na Muda Wake

Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Na Muda Wake

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, Takbiyr (Masiku ya Tashriyq) inakusurishwa baada ya Swalaah tu au katika nyakati zote? Na kwa muda gani baada ya ‘Iyd?

 

 

JIBU:

 

Takbiyr ni Mutwlaq (nyakati zote) na Muqayyad (nyakati maalumu za kukadirika) ni muda wote na baada ya kila Swalaah. Huanzia alfajiri ya siku ya 'Arafah  hadi jua linapozama siku ya kumi na tatu. Hizo ni siku tano yaani tarehe tisa, kumi, kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu mpaka jua linapozama (Magharibi) (inapaswa) Mutwlaq na Muqayyad.

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Maqaalaat Mutanawwi’ah Mjalada 26]

 

 

Share