Wali Na Kamba Wa Sosi Ya Nyanya Na Paprika

Wali Na Kamba Wa Sosi Ya Nyanya Na Paprika

 

 

 

Vipimo:

               

 

Mchele  -    3 Vikombe  

Kamba (Prawns) – kilo 1 size kubwa kabisa

Nayanya – 3 katakata au saga

Nyanya kopo – vijiko 3 vya supu

Paprika – kijiko 1 cha supu

Bizari ya mchuzi

Ndimu – 1 kamua

Chumvi kiasi

Mafuta - vijiko 3 vya supu

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Roweka mchele kisha uchemshe na upike kama kawaida ya mwali mweupe.
  2. Chemsha kamba kidogo tu kwa chumvi, ndimu na bizari ya mchuzi
  3. Weka mafuta katika kikaangio kisha kaanga nyanya hadi ziwive kisha tia nyanya kopo na paprika, chumvi.
  4. Mimina kamba uchanganye vizuri na sosi.
  5. Pakua wali katika sahani, mwagia sosi la kamba, tayari kuliwa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share