Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Aashuraa: Inafaa Swawm Siku Ya ‘Aashuraa Pekee Au Ni Makruwh (Inachukiza)?

 

Inafaa Swawm Siku Ya ‘Aashuraa Pekee Au Ni Makruwh (Inachukiza)?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je inajuzu Swawm siku 'Aashuraa peke yake bila ya kufunga kabla au baada yake? Kwani nimesoma katika moja ya majarida ya Fatwa kuwa inajuzu kwa sababu ile karaha imeondoka kwa kuwa Mayahudi hawafungi siku hizi?

 

 

JIBU:

 

Karaha ya Swawm siku ya 'Aashuraa peke yake sio jambo lilowafikiwa na Ahluli-'Ilm (Wanazuoni) kwani kuna miongoni mwao wanaona hakuna karaha ya kufunga peke yake.

 

Hata hivyo, ni bora zaidi  kufunga kabla au baada yake.

 

Siku ya tisa ni bora kuliko ya kumi na moja. Yaani ni bora kufunga siku kabla yake kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  "Nikibakia hadi mwakani nitafunga siku ya tisa." [Swahiyh Muslim 1134] yaani pamoja na siku ya kumi.

 

Baadhi ya Ahlul-‘Ilm wametaja  kuwa Swiyaam ya ya 'Aashuraa ina hali tatu:

 

Hali ya kwanza: Kufunga siku kabla yake au siku baada yake.

 

Hali ya pili: Kuifunga 'Aashuraa peke yake.

 

Hali ya tatu: Kufunga siku kabla yake na siku baada yake. (siku zote tatu).

 

Na wakataja kuwa,  ukamilifu ni kufunga siku kabla na siku baada yake. Kisha afunge tisa na kumi, kisha afunge kumi na kumi na moja. Au aifunge 'Aashuraa peke yake. Na kilichodhihiri ni kuwa kuifunga peke yake sio makruwh (kuchukiza). Lakini lilo bora kabisa ni  kufunga siku kabla na siku baada yake.

 

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Rasaail Ash-Shaykh Muhammad Swaalih Al-‘Uthyamiyn Mjalada 20 Kitaab Asw-Swiyaam]

  

  

Share