033-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwafanyia Upole Mayatima, Mabinti, Wanyonge wote, Maskini, Waliofilisika Pamoja na Kuwafanyia Hisani, Kuwahurumia, Kuwanyenyekea na kuwainamishia Bawa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب ملاطفة اليتيم والبنات وسائر الضعفة والمساكين

والمنكسرين والإحسان إليهم والشفقة عليهم

والتواضع معهم وخفض الجناح لهم

033- Mlango Wa Kuwafanyia Upole Mayatima, Mabinti, Wanyonge wote, Maskini, Waliofilisika Pamoja na Kuwafanyia Hisani, Kuwahurumia, Kuwanyenyekea na kuwainamishia Bawa

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾

Usikodoe kabisa macho yako katika Tuliyowasterehesha makundi fulani miongoni mwao, na wala usihuzunike juu yao. Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia). [Al-Hijr: 88]

 

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf: 28]

 

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾ وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾ 

Kwa hivyo basi yatima usimuonee. Na mwombaji usimkaripie. [Adhw-Dhwuhaa: 9-10]

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾ فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾ وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾

Je, umemuona yule anayekadhibisha malipo? Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima. Na wala hahamasishi kulisha maskini. [Al-Maa'uwn: 1-3]

 

 

Hadiyth – 1

وعن سعد بن أَبي وَقَّاص رضي الله عنه، قَالَ : كُنَّا مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم سِتَّةَ نَفَرٍ ، فَقَالَ المُشْرِكُونَ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: اطْرُدْ هؤلاء لا يَجْتَرِئُونَ عَلَيْنَا ، وَكُنْتُ أنَا وَابْنُ مَسْعُودٍ . وَرَجُلٌ مِنْ هُذَيْلٍ وَبِلالٌ وَرَجُلاَنِ لَسْتُ أُسَمِّيهِمَا ، فَوَقَعَ في نفس رَسُول الله صلى الله عليه وسلم مَا شَاءَ اللهُ أنْ يَقَعَ فَحَدَّثَ نَفسَهُ ، فَأنْزَلَ اللهُ تعالى : ( وَلا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ) [ الأنعام : 52 ] رواه مسلم .

Amesema Sa'ad bin Abu Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) Tulikuwa watu sita pamija na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na washirikina wakamwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Wafukuze hawa (watu sita) ili wasiwe na ujasiri wa kutukabili sisi." Watu sita hao walikuwa ni mimi, Ibn Mas'uud, mtu katika ukoo wa Hudhayl, Bilaal na watu wawili ambao sikuyajua majina yao. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akahisi alivyopenda Allaah ahisi, hivyo kuanza kuihadithia nafsi yake kuhusu hilo. Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akateremsha: (Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake). [Al-An'aam:52]  Muslim

 

 

 Hadiyth – 2

وعن أَبي هُبَيرَة عائِذ بن عمرو المزنِي وَهُوَ مِنْ أهْل بيعة الرضوان رضي الله عنه: أنَّ أبا سُفْيَانَ أتَى عَلَى سَلْمَانَ وَصُهَيْبٍ وَبلاَلٍ في نَفَرٍ ، فقالوا : مَا أخَذَتْ سُيُوفُ اللهِ مِنْ عَدُوِّ الله مَأْخَذَهَا ، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍرضي الله عنه: أتَقُولُون هَذَا لِشَيْخِ قُرَيْشٍ وَسَيدِهِمْ ؟ فَأتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَأخْبَرهُ ، فَقَالَ : (( يَا أَبَا بَكْرٍ ، لَعلَّكَ أغْضَبتَهُمْ ؟ لَئِنْ كُنْتَ أغْضَبْتَهُمْ لَقَدْ أغْضَبتَ رَبَّكَ )) فَأَتَاهُمْ فَقَالَ : يَا إخْوَتَاهُ ، أغْضَبْتُكُمْ ؟ قالوا : لاَ ، يَغْفِرُ اللهُ لَكَ يَا أُخَيَّ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah 'Aa'idh bin 'Amr Al Muzaniy. katika maswahaba wa Bay'ah ya Ridhwaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Abu Sufyaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipita kwenye kikundi cha watu akiwemo Salman, Suhayb na Bilaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) wakasema: "Panga za Allaah hazijatekeleza haki yake kwa adui wa Allaah." Abu Bakr akasema: "Mnasema haya kwa mzee na bwana wa Maquraysh?" Wakaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakampa habari. Akasema: "Ee Abu Bakr! Nimekuudhini? ikiwa umewaudhi umemkasirisha Mola wako." Akaenda kwao akawaambia: "Ndugu zangu, je nimewaudhi?" Wakasema: "Hapana, Ee ndugu yetu Allaah Akughufirie." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن سهل بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أَنَا وَكَافلُ اليَتِيمِ في الجَنَّةِ هَكَذا )) وَأَشارَ بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى ، وَفَرَّجَ بَيْنَهُمَا . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Sahl (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima tuko Peponi kama hivi." Akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati na kupambanua baina yake."  [Al-Bukhaariy]

 

 

 Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَافلُ اليَتيِم لَهُ أَوْ لِغَيْرِهِ أَنَا وَهُوَ كَهَاتَيْنِ في الجَنَّةِ )) وَأَشَارَ الرَّ‌اوِي وَهُوَ مَالِكُ بْنُ أنَس بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى . رواه مسلم .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima wake au mwengineo, mimi na yeye tutakuwa hivi Peponi." Maalik bin Anas ambaye ndie mpokezi akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَيْسَ المِسْكينُ الَّذِي تَرُدُّهُ التَّمْرَةُ وَالتَّمْرَتَانِ ، وَلا اللُّقْمَةُ وَاللُّقْمَتَانِ إِنَّمَا المِسكِينُ الَّذِي يَتَعَفَّفُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية في الصحيحين : (( لَيْسَ المِسكِينُ الَّذِي يَطُوفُ عَلَى النَّاسِ تَرُدُّهُ اللُّقْمَةُ واللُّقْمَتانِ ، وَالتَّمْرَةُ والتَّمْرَتَانِ ، وَلَكِنَّ المِسْكِينَ الَّذِي لاَ يَجِدُ غنىً يُغْنِيه ، وَلاَ يُفْطَنُ بِهِ فَيُتَصَدَّقَ عَلَيهِ ، وَلاَ يَقُومُ فَيَسْأَلُ النَّاسَ )) .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si maskini mwenye kurudisha kwa ajili ya tende moja au mbili. hakika maskini ni yule anayeacha kuomba pamoja na ufakiri wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah iliyo katika Sahihi Mbili: "Sio maskini mwenye kuwazungukia watu akapewa tonge moja au mbili na tende moja au mbili lakini maskini ni yule asiyepata cha kumtosheleza wala hajulikani ili akapewa sadaka wala haombi."

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( السَّاعِي عَلَى الأَرْمَلَةِ وَالمِسْكِينِ ، كَالمُجَاهِدِ في سَبيلِ اللهِ )) وَأحسَبُهُ قَالَ : (( وَكالقَائِمِ الَّذِي لاَ يَفْتُرُ ، وَكَالصَّائِمِ الَّذِي لاَ يُفْطِرُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ . 

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumsimamia mjane na maskini (kwa matumizi) ni kama Mujaahid katika Njia ya Allaah." Na nadhani alisema: "Na ni kama anayeswali usiku pasi na kupumzika na mafungaji asiyekula." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( شَرُّ الطَّعَامِ طَعَامُ الوَلِيمَةِ ، يُمْنَعُهَا مَنْ يَأتِيهَا ، وَيُدْعَى إِلَيْهَا مَنْ يَأْبَاهَا ، وَمَنْ لَمْ يُجِبِ الدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَى اللهَ وَرَسُولَهُ )) رواه مسلم .

وفي رواية في الصحيحين ، عن أَبي هريرة من قوله : (( بئْسَ الطَّعَامُ طَعَامُ الوَلِيمَةِ يُدْعَى إِلَيْهَا الأغْنِيَاءُ ويُتْرَكُ الفُقَراءُ )) .

Na imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Chakula kibaya kabisa ni chakula cha walima, kinanyimwa anayekiendea na hualikwa anayekikataa. Na asiyejibu mwaliko basi amemuasi Allaah na Rasuli wake." [Muslim]

Katika riwaayah iliyo katika Sahihi Mbili: Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa kauli yake chakula kibaya ni cha walima. wanaalikwa kwayo matajiri na kuachwa mafakiri."

 

 

Hadiyth – 8

وعن أنس رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ عَالَ جَارِيَتَيْن حَتَّى تَبْلُغَا جَاءَ يَوْمَ القِيَامَةِ أنَا وَهُوَ كَهَاتَيْنِ )) وضَمَّ أصَابِعَهُ . رواه مسلم .

Na imepokewa na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakaye wasimamia mabinti wawili mpaka akabaleghe, atakuja siku ya Qiyaamah mimi na yeye ni kama hivi." Akavishikanisha vidole vyake viwili. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : دَخَلَتْ عَلَيَّ امْرَأةٌ وَمَعَهَا ابنتان لَهَا ، تَسْأَلُ فَلَمْ تَجِدْ عِنْدِي شَيئاً غَيْرَ تَمْرَةٍ وَاحدَةٍ ، فَأعْطَيْتُهَا إيَّاهَا فَقَسَمَتْهَا بَيْنَ ابْنَتَيْها ولَمْ تَأكُلْ مِنْهَا ، ثُمَّ قَامَتْ فَخَرجَتْ ، فَدَخَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَينَا ، فَأخْبَرْتُهُ فَقَالَ : (( مَنِ ابْتُليَ مِنْ هذِهِ البَنَاتِ بِشَيءٍ فَأحْسَنَ إلَيْهِنَّ ، كُنَّ لَهُ سِتراً مِنَ النَّارِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Aliingia kwangu mwanamke akiwa na binti zake wawili kuomba. sikuwa na chochote ila tende moja, ambayo nilimpatia, naye akaigawa mara mbili ili kuwapatia binti zake, naye hakula chochote. Kisha akasimama, akatoka. hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia, nami nikampasha habari kuhusu tukio hilo, akasema: "Mwenye kutahaniwa na mabinti hawa kwa chochote, naye akawafanyia ihsani, watakuwa ni kinga kwake na Moto." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : جَاءتني مِسْكينةٌ تَحْمِلُ ابْنَتَيْنِ لَهَا ،  فَأطْعَمْتُها ثَلاثَ تَمرَات ، فَأعْطَتْ كُلَّ وَاحِدَة مِنْهُمَا تَمْرَةً وَرَفَعتْ إِلَى فِيها تَمْرَةً لِتَأكُلها ، فَاسْتَطعَمَتهَا ابْنَتَاهَا ، فَشَقَّتِ التَّمْرَةَ الَّتي كَانَتْ تُريدُ أنْ تَأكُلَهَا   بَيْنَهُما ، فَأعجَبَنِي شَأنُهَا ، فَذَكَرْتُ الَّذِي صَنَعَتْ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : (( إنَّ الله قَدْ أوْجَبَ لَهَا بها الجَنَّةَ ، أَوْ أعتَقَهَا بِهَا مِنَ النَّارِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Maskini alikuja kwangu na mabinti wawili. Nikampa tende tatu, naye akampatia kila mmoja wao tende, akanyanyua moja mdomoni mwake ili aile. Mabinti zake wakaitaka, akagawa baina yao tende aliotaka kuila. Bikapendezwa na aliochofanya, nikamtajia jambo hilo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "hakika Allaah Amewajibisha kuingia kwake Peponi kwa kitendo hicho au kumwacha nacho na Moto." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي شُرَيحٍ خُوَيْلِدِ بن عمرو الخزاعِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( اللَّهُمَّ إنِّي أُحَرِّجُ حَقَّ الضَّعِيفَينِ : اليَتِيم وَالمَرْأةِ )) حديث حسن رواه النسائي بإسناد جيد .

Imepokewa kutoka kwa Abu Shurayh Khuwaylid bin 'Ammr Al-Khuzaa'iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Hakika nimemtangaza kuwa mwenye dhambi yeyote anayepoteza haki ya wanyonge wawili: Yatima na mwanamke." [Hadiyth hasan iliyonukuliwa na An-Nasaa'iy kwa isnad nzuri].

 

 

Hadiyth – 12

وعن مصعب بن سعد بن أَبي وقَّاص رضي الله عنهما ، قَالَ : رَأى سعد أنَّ لَهُ فَضْلاً عَلَى مَنْ دُونَهُ ، فَقَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( هَلْ تُنْصرُونَ وتُرْزَقُونَ إلاَّ بِضُعَفَائِكُمْ )) رواه البخاري هكذا مُرسلاً ، فإن مصعب بن سعد تابعيٌّ ، ورواه الحافظ أَبُو بكر البرقاني في صحيحه متصلاً عن مصعب ، عن أبيه رضي الله عنه.

Amesema Musw'ab bin Sa'ad bin waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Sa'ad aliona yeye ni mwenye fadhila kuliko wengine. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Hamnusuriwi na kuruzikiwa ila kwa wanyonge wenu." [Al-Bukhaariy ameipokea hivi Mursal, kwani Musw'ab bin sa'ad ni Taabi'iyy, na ameipokea Haafidh Abuu Bakr Al-Barqaaniy katika sahihi yake toka kwa Musw'ab kwa baba yake Radhwiya Allaahu 'anhu]

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي الدَّرداءِ عُويمر رضي الله عنه، قَالَ : سمعتُ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم، يقول :  (( ابْغُوني الضُّعَفَاء ، فَإنَّمَا تُنْصَرُونَ وتُرْزَقُونَ ، بِضُعَفَائِكُمْ )) رواه أَبُو داود بإسناد جيد .

Kutoka kwake Abu Dardaa' 'Uwaymir Amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Nisaidieni (kwa kuwasaidia) wanyonge, hakika mnanusuriwa na kuruzukiwa kwa sababu ya wanyonge wenu." [Abuu Daawuud kwa Isnaad nzuri]

 

 

 

 

Share