035-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Haki Ya Mume Juu Ya Mke

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب حق الزوج عَلَى المرأة

035-Mlango Wa Haki Ya Mume Juu Ya Mke

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ﴿٣٤﴾

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. [An-Nisaa: 34]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امرَأتَهُ إِلَى فرَاشِهِ فَلَمْ تَأتِهِ ، فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا ، لَعَنَتْهَا المَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية لهما : (( إِذَا بَاتَت المَرأةُ هَاجِرَةً فِرَاشَ زَوْجِهَا لَعَنَتْهَا المَلاَئِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ )) .

وفي رواية قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( والَّذِي نَفْسِي بيَدِهِ مَا مِنْ رَجُلٍ يَدْعُو امْرَأتَهُ إِلَى فِرَاشهِ فَتَأبَى عَلَيهِ إلاَّ كَانَ الَّذِي في السَّمَاء سَاخطاً عَلَيْهَا حَتَّى يَرْضَى عَنها )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mume anapomuita mkewe kitandani mwake wala asije, akalala akiwa amemkasirikia mkewe, Malaaikah watamlaani mke huyo mpaka apambazukiwe." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah yao wawili: "Mke anapolala kwa kuhama kitanda cha mumewe, Malaaikah humlani mpaka kupambazuke."

Katika riwaayah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakuna mwanamume yoyote anamuita mkewe kitandani, akamkatalia isipokuwa Aliye mbinguni Humkasirikia mpaka mume Amridhie."

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه أيضاً : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ يَحِلُّ لامْرَأةٍ أنْ تَصُومَ وزَوْجُهَا شَاهدٌ إلاَّ بإذْنِهِ ، وَلاَ تَأذَنَ في بَيْتِهِ إلاَّ بِإذنِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ وهذا لفظ البخاري .

Imepokewa kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa mke kufunga na mumewe yuko (mjini) ila kwa idhini yake. Wala siruhusa (kwa mke) kumruhusu mtu kuingia nyumbani (kwao) ila kwa idhini ya mumewe." [Al-Bukhaariy na Muslim] Na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( كلكم رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ : وَالأمِيرُ رَاعٍ ، والرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أهْلِ بَيتِهِ ، وَالمَرْأةُ رَاعِيةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجها وَوَلَدهِ ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ  رَعِيَّتِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ 

Imepokewa kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa alio wachunga. Amiri ni mchunga, na mume ni mchunga wa watu wa nyumbani kwake, na mke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake; nyote ni wachunga mtaulizwa mlivyovichunga." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي علي طَلْق بن علي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا دَعَا الرَّجُلُ زَوْجَتهُ لحَاجَتِهِ فَلْتَأتِهِ وَإنْ كَانَتْ عَلَى التَّنُور)) . رواه الترمذي والنسائي ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwake Abuu 'Aliy Twalqbin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindi mume anapomuita mkewe kwa haja zake (jimai) aje kwake mara moja hata akiwa kwenye tanuri." [At-Tirmidhiy na An-Nasaa'iy, na akasema At-Tirmidhiy kuwa ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَوْ كُنْتُ آمِراً أحَداً أنْ يَسْجُدَ لأحَدٍ لأمَرْتُ المَرأةَ أنْ تَسْجُدَ لزَوجِهَا )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau ningemuamuru mke kumsujudia mumewe." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أم سَلَمَة رضي الله عنها ، قَالَتْ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( أيُّمَا امْرَأةٍ مَاتَتْ ، وَزَوْجُهَا عَنْهَا رَاضٍ دَخَلَتِ الجَنَّةَ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke aliyekufa na mumewe yu radhi naye, ataingia Peponi." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 7

وعن معاذ بن جبل رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ تُؤْذِي امْرَأةٌ زَوْجَهَا في الدُّنْيَا إلاَّ قَالَتْ زَوْجَتُهُ مِنَ الحُورِ العِينِ لاَ تُؤذِيهِ قَاتَلكِ اللهُ ‍! فَإِنَّمَا هُوَ عِنْدَكِ دَخِيلٌ يُوشِكُ أنْ يُفَارِقَكِ إِلَيْنَا )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke hamuudhi mumewe duniani ila anasema mkewe katika Huuril 'Iyn watamwambia, 'Usimuudhi, Allaah Akulaani! Hakika yeye ni mgeni aliye kwako na karibuni atakuacha na kuungana nasi." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أسامة بن زيد رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَا تَرَكْتُ بَعْدِي فِتْنَةً هِيَ أضَرُّ عَلَى الرِّجَالِ مِنَ النِّساء )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sijaacha baada yangu fitna iliyo na madhara makubwa kwa wanaume kuliko ile ya wanawake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share