046-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kupenda kwa Ajili ya Allaah na Kuhimiza hilo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل الحب في الله والحث عَلَيهِ وإعلام الرجل من يحبه ، أنه يحبه ، وماذا يقول لَهُ إِذَا أعلمه

046-Mlango Wa Fadhila za Kupenda kwa Ajili ya Allaah na Kuhimiza hilo

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ ﴿٢٩﴾

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao. [Al-Fat-h: 29] Hadi mwisho wa Surah.

 

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ ﴿٩﴾

Na wale waliokuwa na masikani (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao. [Al-Hashr: 9]

 

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أنسٍ رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( ثَلاثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ بِهِنَّ حَلاوَةَ الإيمانِ : أنْ يَكُونَ اللهُ وَرَسُولُهُ أحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سَوَاهُمَا ، وَأنْ يُحِبّ المَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إلاَّ للهِ ، وَأَنْ يَكْرَهَ أنْ يَعُودَ في الكُفْرِ بَعْدَ أنْ أنْقَذَهُ الله مِنْهُ ، كَمَا يَكْرَهُ أنْ يُقْذَفَ في النَّارِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sifa tatu yeyote mwenye kuwa nazo atapata ladha (utamu) wa Imani: Kuwa Allaah na Rasuli Wake ndiyo awapendao zaidi kuliko wasiokuwa wao; (la pili) kumpenda mtu kwa ajili ya Allaah Peke Yake, (la tatu) kuchukia kurudi katika ukafiri kama anavyochukia kutupwa motoni. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إلاَّ ظِلُّهُ : إمَامٌ عَادِلٌ ، وَشَابٌّ نَشَأ في عِبَادَةِ الله (عزّ وجلّ)، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في اللهِ اجْتَمَعَا عَلَيهِ وتَفَرَّقَا عَلَيهِ ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأةٌ ذَاتُ حُسْنٍ وَجَمَالٍ ، فَقَالَ : إنِّي أخَافُ الله ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ ، فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu saba atawafunika chini ya kivuli Chake siku hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake: Imamu (kiongozi) muadilifu, kijana aliyeinukia katika kumuabudu Allaah ('Azza wa Jall), na mtu moyo wake umetundikwa Msikitini, na watu wawili wamependana kwa ajili ya Allaah, wakajumuika juu yake, na kufarikiana kwa ajili Yake, na mtu ameitwa na mwanamke mzuri mwenye kuvutia, akasema: 'Mimi namwogoa Allaah,' na mtu aliyetoa sadaka akaificha hadi kushoto kwake kusijue ulichotoa kulia kwake, na mtu amemtaja Allaah faraghani macho yake yakabubujika machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنّ الله تَعَالَى يقول يَوْمَ القِيَامَةِ : أيْنَ المُتَحَابُّونَ بِجَلالِي ؟ اليَوْمَ أُظِلُّهُمْ فِي ظِلِّي يَوْمَ لاَ ظِلَّ إلاَّ ظِلِّي )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa atasema Siku ya Qiyaamah: "Wawapi waliopendana kwa Utukufu Wangu?, Leo nitawafunika katika kivuli Changu siku hakuna kivuli isipokuwa kivuli Changu." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لا تَدْخُلُوا الجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا ، وَلا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا ، أوَلاَ أدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ ؟ أفْشُوا السَّلامَ بينكم )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Hamtaingia Peponi hadi Muamini, wala hamtaamini mpaka mpendane. Je niwaonyeshe kitu mkikifanya mtapendana? Enezeni salamu baina yenu." [Muslim].

 

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( أنَّ رَجُلاً زَارَ أخاً لَهُ في قَرْيَةٍ أخْرَى ، فَأرصَدَ اللهُ لَهُ عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكاً … )) وذكر الحديث إِلَى قوله : (( إنَّ الله قَدْ أحبَّكَ كَمَا أحْبَبْتَهُ فِيهِ )) رواه مسلم ، وقد سبق بالباب قبله .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu mmoja alimzuru nduguye katika Kijiji chengine. Allaah alimwakilisha Malaika njiani...." Akataja hadiyth hadi kauli yake: "Hakika Allaah amekupenda kama ulivyompenda ndugu yako kwa ajili Yake." [Muslim]. Imetanguliwa kutajwa katika mlango uliofuata.

 

 

 

Hadiyth – 6

وعن البرَاءِ بن عازب رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ  صلى الله عليه وسلم أنَّهُ قَالَ في الأنصار : (( لاَ يُحِبُّهُمْ إلاَّ مُؤمِنٌ ، وَلاَ يُبْغِضُهُمْ إلاَّ مُنَافِقٌ ، مَنْ أحَبَّهُمْ أَحَبَّهُ الله ، وَمَنْ أبْغَضَهُمْ أبْغَضَهُ الله )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa'i bin 'Aazib (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema yafuatayo kuhusu Ansari: "Hawapendi wao isipokuwa Muumini na hawachukii isipokuwa mnafiki. Kwa hiyo Allaah Atampenda anayewapenda na Atamchukia anayewachukia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 7

وعن معاذ رضي الله عنه، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : المُتَحَابُّونَ في جَلالِي ، لَهُمْ مَنَابِرُ مِنْ نُورٍ يَغْبِطُهُمُ النَّبِيُّونَ وَالشُّهَدَاءُ )) . رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwake Mu'aadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Amesema Allaah ('Azza wa Jall): Wanaopendana kwa ajili ya Utukufu Wangu, watakaa katika minbari za nuru huku Manabii na mashahidi wakitamani hadhi na kheri hiyo." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي إدريس الخولاني رحمه الله ، قَالَ :دخَلْتُ مَسْجِدَ دِمَشْقَ ، فَإذَا فَتَىً بَرَّاق الثَّنَايَا وَإِذَا النَّاسُ مَعَهُ ، فَإِذَا اخْتَلَفُوا في شَيْءٍ ، أَسْنَدُوهُ إِلَيْه ، وَصَدَرُوا عَنْ رَأيِهِ ، فَسَأَلْتُ عَنْهُ ، فَقيلَ : هَذَا مُعَاذُ بْنُ جَبَل رضي الله عنه. فَلَمَّا كَانَ مِنَ الغَدِ ، هَجَّرْتُ ، فَوَجَدْتُهُ قَدْ سَبَقَنِي بالتَّهْجِيرِ ، ووَجَدْتُهُ يُصَلِّي ، فانْتَظَرتُهُ حَتَّى قَضَى صَلاتَهُ ، ثُمَّ جِئْتُهُ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ ، فَسَلَّمْتُ عَلَيهِ ، ثُمَّ قُلْتُ : وَاللهِ إنّي لأَحِبُّكَ لِله ، فَقَالَ : آلله ؟ فَقُلْتُ : اللهِ ، فَقَالَ : آللهِ ؟ فَقُلْتُ : اللهِ ، فَأخَذَنِي بِحَبْوَةِ رِدَائِي ، فجبذني إِلَيْهِ ، فَقَالَ : أبْشِرْ ! فإنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( قَالَ الله تَعَالَى : وَجَبَتْ مَحَبَّتي لِلْمُتَحابين فيَّ ، وَالمُتَجَالِسينَ فيَّ ، وَالمُتَزَاوِرِينَ فيَّ ، وَالمُتَبَاذِلِينَفِيَّ )) حديث صحيح رواه مالك في الموطأ بإسناده الصحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Idris Al-Khawlaani (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Niliingia Msikiti wa Damascus, nikamuona kijana ana meno meupe masafi (mwenye kutabasamu sana), watu wako pamoja naye. Watu wanapotofautiana katika jambo walikuwa wakitaka na kuichukua rai yake. Nikauliza kuhusu yeye na nikaambiwa: 'Huyu ni Mu'aadh bin Jabal (Radhwiyah Allaahu 'anhu). Siku ya pili nilifika mapema Msikitini lakini nikapata kuwa ameshafika kabla yangu. Nilimpata yeye anaswali hivyo nilingojea mpaka akamaliza Swalah yake. Hapo nilikwenda mbele yake na kumsalimia, kisha nikamwambia: 'Naapa kwa Allaah kuwa mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'je, ni kwa ajili ya Allaah?' Nikasema: 'Ndio, kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'Je, ni kwa ajili ya Allaah?' Nikasema: 'Ndio kwa ajili ya Allaah.' Hapo akanishika kwa mkunjo wa shuka yangu na kunileta karibu naye, akasema: 'Hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Amesema Allaah Ta'aalaa! Ni wajibu kuwapenda wale wanaopendana kwa ajili Yangu, na wenye kukaa pamoja kwa ajili Yangu na wenye kutembeleana kwa ajili Yangu na wenye kusaidiana kwa ajili Yangu." [Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Imam Malik katika al-Muwatta' kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي كَرِيمَةَ المقداد بن معد يكرب رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أَحَبَّ الرَّجُلُ أخَاهُ ، فَليُخْبِرْهُ أَنَّهُ يُحِبُّهُ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ :(( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Kariimah al-Miqdaad bin Ma'diyakrib (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ndugu mmoja anapompenda mwenziwe, ampashe habari ya kuwa anampenda." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Hadiyth – 10

وعن معاذ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أخذ بيدهِ ، وَقالَ : (( يَا مُعَاذُ ، وَاللهِ ، إنِّي لأُحِبُّكَ ، ثُمَّ أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ لاَ تَدَعَنَّ في دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ تَقُولُ : اللَّهُمَّ أعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ ، وَشُكْرِكَ ، وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود والنسائي بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimshika mkono wake na kumwambia: "Ee Mu'aadh! Naapa kwa Allaah kuwa nakupenda, kisha nakuusia ee Mu'aadh; Usiache kusema kila baada ya Swalah ya faradhi maneno yafuatayo: 'Ee Mola Wangu! Nisaidie katika kukutaja na kukushukuru na kukuabudu katika njia bora kabisa." [Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu Daawuud na An-Nasai kwa isnaad swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن أنس رضي الله عنه: أنَّ رَجُلاً كَانَ عِنْدَ النَّبيِّ ، صلى الله عليه وسلم، فَمَرَّ رَجُلٌ بِهِ ، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، أنِّي لأُحِبُّ هَذَا ، فَقَالَ لَهُ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( أأعْلَمْتَهُ ؟ )) قَالَ : لا . قَالَ : (( أعْلِمْهُ )) فَلَحِقَهُ ، فَقَالَ : إنِّي أُحِبُّكَ في الله ، فَقَالَ : أَحَبَّكَ الَّذِي أحْبَبْتَنِي لَهُ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba: "Kwa hakika kulikuwa na mtu pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akapita mbele yao mtu mwingine. Akasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nampenda huyu mtu.' Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: 'Je, umemjulisha hili?' Akasema: 'La! Akamwambia: 'Basi kamjulishe hilo.' Aliondoka huyu mtu na kukutana naye na hapo akamwambia: 'Hakika mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'Akupende Allaah ambaye kwa ajili Yake umenipenda mimi'." [Abu Daawuud kwa isnaad iliyo swahiyh]

 

 

 

 

 

Share