Tekeleza Sunnah Ya Kukithirisha Swiyaam Katika Mwezi Wa Sha’baan

 

Tekeleza Sunnah Ya Kukithirisha Swiyaam Katika Mwezi Wa Sha’baan

 

Alhidaaya.com

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikithirisha kufunga (Swiyaam) katika mwezi wa Sha’baan kuliko miezi mengineyo:

 

 

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: (كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏يَصُومُ حَتَّى نَقُولَ لَا يُفْطِرُ، وَيُفْطِرُ حَتَّى نَقُولَ لَا يَصُومُ، وَمَا رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏اِسْتَكْمَلَ صِيَامَ شَهْرٍ قَطُّ إِلَّا رَمَضَانَ، وَمَا رَأَيْتُهُ فِي شَهْرٍ أَكْثَرَ مِنْهُ صِيَامًا فِي شَعْبَانَ)  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ   

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akifunga hadi tunasema kuwa hatofungua; na anakula (huwa hafungi) hadi tunasema kuwa hatofunga. Sikuwahi kumuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anafunga mwezi mzima bila kufungua isipokuwa mwezi wa Ramadhwaan tu, na sikumuona anafunga sana katika mwezi wowote zaidi ya Sha’baan.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na pia,

 

 

 عن عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ حَدَّثَتْهُ قَالَتْ، لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَصُومُ شَهْرًا أَكْثَرَ مِنْ شَعْبَانَ، فَإِنَّهُ كَانَ يَصُومُ شَعْبَانَ كُلَّهُ، وَكَانَ يَقُولُ ‏ (خُذُوا مِنَ الْعَمَلِ مَا تُطِيقُونَ، فَإِنَّ اللَّهَ لاَ يَمَلُّ حَتَّى تَمَلُّوا) وَأَحَبُّ الصَّلاَةِ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم مَا دُووِمَ عَلَيْهِ، وَإِنْ قَلَّتْ ‏"‏ وَكَانَ إِذَا صَلَّى صَلاَةً دَاوَمَ عَلَيْهَا‏.‏
 

‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufunga mwezi wowote zaidi ya kufunga mwezi wa Sha’baan. Alikuwa akisema:  ((Fanyeni amali ambazo mnaziweza kwa wepesi, kwani Allaah Hachoki (kulipa thawabu) mpaka nyinyi muwe na ajizi na mchoke (kutenda ‘amali njema)).  Na Swalaah bora kabisa aipendayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni ile inayodumishwa (maishani mwa mtu), japo kama (Swalaah zenyewe) ni chache. Na alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposwali Swalaah (za ziyada) alikuwa akizidumisha.”  [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia,

 

 

عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ لَقَدْ كَانَتْ إِحْدَانَا تُفْطِرُ فِي رَمَضَانَ فَمَا تَقْدِرُ عَلَى أَنْ تَقْضِيَ حَتَّى يَدْخُلَ شَعْبَانُ وَمَا كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُومُ فِي شَهْرٍ مَا يَصُومُ فِي شَعْبَانَ كَانَ يَصُومُهُ كُلَّهُ إِلاَّ قَلِيلاً بَلْ كَانَ يَصُومُهُ كُلَّهُ ‏.‏

‘Aaishah (رضي الله عنه) amesema: “Tulikuwa kati yetu (wanawake) tukifungulia Ramadhwaan, na hutokea kuwa hawezi mtu kulipa deni lake mpaka inapoanza Sha’baan. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa akifunga mwezi wowote zaidi kama alivyokuwa akifunga Sha’baan, alikuwa akifunga wote isipokuwa siku chache. bali alikuwa akifunga (mwezi) wote.” [Sunan An-Nasaaiy]

 

 

Sababu Za Swiyaam Mwezi Wa Sha’baan:

 

أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، قَالَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَمْ أَرَكَ تَصُومُ شَهْرًا مِنَ الشُّهُورِ مَا تَصُومُ مِنْ شَعْبَانَ ‏.‏ قَالَ ‏ "‏ ذَلِكَ شَهْرٌ يَغْفُلُ النَّاسُ عَنْهُ بَيْنَ رَجَبٍ وَرَمَضَانَ وَهُوَ شَهْرٌ تُرْفَعُ فِيهِ الأَعْمَالُ إِلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ فَأُحِبُّ أَنْ يُرْفَعَ عَمَلِي وَأَنَا صَائِمٌ ‏"

Usaamah bin Zayd (رضي الله عنه) amehadithia: Nilimwambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Ee Rasuli wa Allaah, sijapatapo kukuona ukifunga mwezi wowote zaidi kama unavyofunga Sha’baan.  Akasema:  ((Huo ni mwezi ambao watu wanaghafilika nao, ambao uko baina ya Rajab na Ramadhwaan, na huo ni mwezi ambao amali zinapandishwa kwa Rabb wa ulimwengu, nami napenda amali zangu zipandishwe hali yakuwa niko katika Swawm))  [Swahiyh An-Nasaaiy 2356 ].

 

 

 

Katazo La Swiyaam Baada Ya Nusu Ya Sha’baan:

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {إِذَا اِنْتَصَفَ شَعْبَانَ فَلَا تَصُومُوا} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَاسْتَنْكَرَهُ أَحْمَدُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ikifika nusu ya mwezi wa Sha’baan, msifunge.” [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

Na pia,

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{لَا تَقَدَّمُوا رَمَضَانَ بِصَوْمِ يَوْمٍ وَلَا يَوْمَيْنِ، إِلَّا رَجُلٌ كَانَ يَصُومُ صَوْمًا، فَلْيَصُمْهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msitangulize Ramadhwaan kwa Swawm siku moja au mbili  isipokuwa mtu alikuwa ana (mazoea ya) Swawm makhsusi basi afunge.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na pia,

 

 

عن إبن عبَّاس رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:  ((لا تَقَدَّمُوا شَهْرَ رَمَضَانَ بِصِيَامٍ إِلا أَنْ يُوَافِقَ ذَلِكَ صَوْمًا كَانَ يَصُومُهُ أَحَدُكُمْ)) رواه البخاري
 

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msiutangulize mwezi wa Ramadhwaan kwa (Swawm) siku moja au mbili, ila kwa wale tu wenye mazoea ya Swawm kila mara, na kwa hali hiyo hao wanaweza kufunga (siku hizo))) [Al-Bukhaariy]

 

 

Swiyaam makhsusi ni zile za Sunnah ambazo mtu alikuwa na mzoea nazo kama Jumatatu na Alkhamiys.

 

 

Kwa faida zaidi bonyeza kiungo kifuatacho upate Fadhila mbali mbali Za Swawm: 

 

 

Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah

 

 

 

 

Share