14-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Hakukataa Kuhudumiwa Na Watumwa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

14-Unyenyekevu Wake: Hakukataa Kuhudumiwa Na Watumwa   

www.alhidaaya.com

 

 

  عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا صَلَّى الْغَدَاةَ جَاءَ خَدَمُ الْمَدِينَةِ بِآنِيَتِهِمْ فِيهَا الْمَاءُ فَمَا يُؤْتَى بِإِنَاءٍ إِلاَّ غَمَسَ يَدَهُ فِيهَا فَرُبَّمَا جَاءُوهُ فِي الْغَدَاةِ الْبَارِدَةِ فَيَغْمِسُ يَدَهُ فِيهَا ‏.‏

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza kuswali Alfajiri, watumwa wa Madiynah walikuja na vyombo vyao vya maji, basi hakimfikii chombo (cha maji) ila alitumbukiza mikono yake. Na mara nyengine huja asubuhi ya ubaridi mno (hata hivyo hakukataa kwa kupuuza ombi lao ila) alitumbukiza mkono wake.” [Muslim]

 

Share