Kababu Za Kuchoma Na Vitunguu, Pilipili Tamu, Nyanya

Kababu Za Kuchoma Na Vitunguu, Pilipili Tamu, Nyanya

Vipimo

Nyama ya kusaga  (Beef   Regular) - 2LB

Vitu Vya Kuchanganya na nyama

Tangawizi na kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 1 Kijiko cha soup

Chumvi -  kisia

Kiitunguu maji kilichosagwa (Crushed) - 1 Kikubwa

Yai -  1

Chenga za Mkate (bread crumbs) -  1   Kikombe

Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo - 1 Kikombe

Parsely   iliyokatwa ndogo ndogo - 1 Kikombe

Pili pili manga ya powder  - 2 Vijiko vya chai

Bizari ya pilau  ya powder  (cummin)  - 2 Vijiko vya chai

Mafuta (ya kunyunyizia baada ya kupanga kababu)  - ¼ cup

Ni bora mafuta ya zaytuun (olive oil)  

Saladi ya kumwagia karibu na kababu kuwiva  (tayarisha kwa kukata na kuweka kando kama ilivyo katika picha )

Vitunguu - 2

Pilipili kubwa  (Capsicum)  - 2

Nyanya -  2

 

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya nyama na vitu vyake kisha fanya vidonge vya oval na upange katika sinia ya kupikia katika jiko la oven

 

  1. Nyunyiza mafuta kidogo kote
  2. Zipike kwa moto wa juu (broil)   mpaka zipikike huku
  3. Unazigeuza upande wa pili.
  4. Karibu na kuwiva kabisa mwagia vitu ulivyotayarisha na uchanganye  na ziwache ndani ya jiko kwa dakika kama  5.
  5. Ziepue haraka na uziweke katika Sahani ya kupakulia nzuri zikiwa tayari kuliwa. 

Unaweza kutolea na  mkate au  wali   kama huu:

Wali Wake:

Mchele    Basmati (osha na kuroweka )  -  3 Vikombe

Kitunguu  kilichokatwa (chopped) - 1 medium

Tomato  iliokatwa ndogo ndogo (chopped) - 1 medium

Mafuta - 2 kijiko cha soup

Kitunguu saumu/thomu (iliyosagwa) - 1 Kijiko cha Soup

Mdalasini mzima - 1 kijiti

Hiliki - 2 chembe

Karafuu  5 – 7 chembe

Chumvi -Kisia

Bizari ya manjano (Haldi)  - ½  kijiko cha chai

Maji ya kupikia wali - 5-6 vikombe

Stock (Maggi cubes au aina yeyote)  - 3 cubes 

Namna Ya Kupika Wali 

  1. Kaanga kitunguu,  kwa mafuta hayo, kabla ya kugeuka rangi  tia tomato 
  2. Weka vitu vyote  vingine isipokuwa stock  ukaange kidogo.
  3. Tia mchele kisha maji,  stock cubes na  ufunike wali upike katika moto  mdogo.
  4. Pakua katika sahani kisha mwagia Kababu   juu yake.

 

 

Share