Kuku Wa Kuchoma Katika Makaa (B.B.Q)

Kuku Wa Kuchoma Katika Makaa (B.B.Q)

Vipimo

  
Kuku - 10 Ratili (LB)

Kitunguu saumu/thomu na tangawizi  - 3 vijiko vya supu

Chumvi - Kiasi

Bizari mchanganyiko (garam masala) - 2 vijiko vya supu

Masala ya Tanduri - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu

Ukwaju - 1/2 kikombe

Siki - 3 Vijiko vya supu

Mafuta - 1 Vijiko vya supu 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Safisha kuku kisha mwache achuje maji vizuri.
  2. Changaya masala yote kwenye bakuli pamoja na mafuta.
  3. Tia masala katika kuku na rowanisha  kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Na ukipenda rowanisha kuku siku moja kabla uweke katika friji.
  4. Mchome katika jiko la makaa huku ukimpaka mafuta kidogo kidogo ka brashi. 

Kidokezo : Tolea na saladi ya karoti na ukwaju (Tazama katika saladi)

 

 

Share