27-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake Katika Ibaadah: Hakujitukuza Kwa Kujitanguliza Yeye Katika Jamaraat (Kurusha Vijiwe Minaa)

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

27-Unyenyekevu Wake Katika Ibaadah Hakujitukuza Kwa  Kujitanguliza Yeye

Katika Jamaraat (Kurusha Vijiwe Minaa)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Ingawa kawaida ya viongozi hutangulia kutekeleza jambo, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ni kiongozi wa Swahaba katika kutekeleza taratibu za Hajj, lakini hakujipa umbele kama kiongozi, bali alifanya nao pamoja bila ya kujitukuza.  

 

 

 عَنْ قُدَامَةَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْمِي جَمْرَةَ الْعَقَبَةِ يَوْمَ النَّحْرِ عَلَى نَاقَةٍ لَهُ صَهْبَاءَ لاَ ضَرْبَ وَلاَ طَرْدَ وَلاَ إِلَيْكَ إِلَيْكَ ‏.‏

 

Amehadithia Qudaamah bin ‘Abdillaah kwamba: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa juu ya ngamia aliyechanganyika rangi nyekundu na kahawia, akirusha vijiwe katika Jamarah ya Al-‘Aqabah (Minaa) Siku ya An-Nahr (Siku ya Iydul-Adhw-haa), bila kumpiga mtu yeyote au kumfukuza." [At-Tirmidhiy na amesema Abuu ‘Iysaa Hadiyth Hasan Swahiyh. Imekusanywa pia na An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

 

 

Share