022-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hajj Aayah 19: هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 022-Suwrah Al-Hajj Aayah 19

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ

((Hawa ni makhasimu wawili wamekhasimikiana kuhusu Rabb wao)). [Al-Hajji (22:19)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا قَبِيصَةُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي هَاشِمٍ، عَنْ أَبِي مِجْلَزٍ، عَنْ قَيْسِ بْنِ عُبَادٍ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ نَزَلَتْ: هَذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ  فِي سِتَّةٍ مِنْ قُرَيْشٍ عَلِيٍّ وَحَمْزَةَ وَعُبَيْدَةَ بْنِ الْحَارِثِ وَشَيْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ وَعُتْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ وَالْوَلِيدِ بْنِ عُتْبَةَ‏.‏

Ametuhadithia Qabiyswah, ametuhadithia Sufyaan bin Abiy Haashim toka kwa Abiy Mijlaz, toka kwa Qays, toka kwa ‘Ibaad, toka kwa Abu Dharri (رضي الله عنه)   amesema: “[Aayah hii]

هَذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ

 

Hawa ni makhasimu wawili wamekhasimikiana kuhusu Rabb wao)) [Al-Hajj: 19], iliteremka kuwazungumzia Maquraysh sita ambao ni ‘Aliy, Hamzah, ‘Ubayd bin Al-Haarith, Shaybah bin Rabiy’ah, ‘Utbah bin Rabiy’ah na Al-Waliyd bin ‘Utbah. [Al-Bukhaariy Mujallad wa 8 ukurasa wa 298][1]

 

Hawa watu walifungua dimba la pambano la ana kwa ana, mtu kwa mtu, kabla ya kuanza vita vya Badr.

 

 

 

[1] Ameitaja Al-Bukhaariy Hadiyth hii vile vile katika At-Tafsiyr katika Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 59. Imekusanywa na Muslim katika Mujallad wa 18 ukurasa wa 166, Ibn Maajah kwa nambari 2835, At-Twayaalsiy katika Mujallad wa pili ukurasa wa 21, Ibn Sa’ad katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 10, Ibn Jariyr katika Mujallad wa 17 ukurasa wa 131, na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr Mujallad wa 3 ukurasa 164.

 

Al-Bukhaariy katika Mujallad wa 8 ukurasa wa 299 na Al-Haakim katika Mujallad wa pili ukurasa wa 386, wameikusanya Hadiyth kama hii ya Qays bin ‘Ibaad toka kwa ‘Aliy. Al-Haakim amesema: Hadiyth imekuwa Swahiyh kwa riwaayah hizi toka kwa ‘Aliy kama ilivyo Swahiyh toka kwa Abu Dharri Al-Ghiffaariyy ijapokuwa hawakuikusanya”.

 

Angalizo:

 

Hadiyth ya Abu Dharri ni katika Hadiyth ambazo zimekosolewa na Al-Haafidh Abul Hasan ‘Aliy bin ‘Umar Ad-Daaraqutwniy (Rahimahu-Allaah), kwa kuwa Abu Mijlaz anaisimulia kwa kuipokea toka kwa Abu Dharri, na wakati mwingine anaisimulia kwa kauli yake mwenyewe, hivyo Hadiyth inakuwa Mudhwtwarib.

 

An Nawawiy (Rahimahu-Allaah) katika Mujallad wa 18 ukurasa wa 166 amesema Hadiyth hii ni katika ambazo Ad-Daaraqutwniy ameziongeza baada ya kuzisaka na kuziona kuwa ni Swahiyh.

 

Akasema: “Al-Bukhaariy ameikhariji toka kwa Abu Mijlaz toka kwa Qays toka kwa ‘Aliy (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) aliyesema: Mimi ndiye wa mwanzo nitakayechuchumalia magoti [mbele ya Allaah Ar-Rahmaan] kudai haki [ya kwake na ya wenzake dhidi ya makhasimu makafiri]. Qays amesema: Na kwa ajili yao Aayah hii imeteremka. Kisha Al-Bukhaariy akasema: ‘Uthmaan amesimulia usimulizi wake toka kwa Jariyr toka kwa Mansuwr toka kwa Abu Haashim toka kwa Abu Mijlaz. Ad Daaraqutwniy amesema, na kwa hivyo Hadiyth imekuwa Mudhwtwarib. An-Nawawiy kasema, nikasema: Hailazimishi kwa hili Hadiyth kuwa Dhwa’iyf au Mudhwtwarib kwa kuwa Qays ameisikia toka kwa Abu Dharri kama alivyoisimulia Muslim hapa, akaisimulia toka kwake, na akasikia sehemu ya Hadiyth toka kwa ‘Aliy na Qays akaiongezea kwa yale aliyoyasikia toka kwa Abu Dharri, na Abu Mijlaz akaitolea fatwa baadhi ya nyakati na hakusema ni maneno yake au rai yake.

Kama unataka kupekua mengi zaidi, basi angalia Muqaddimatul Fat-h Mujallad wa Pili ukurasa wa 132, na Al Fat-h Mujallad wa Kumi kurasa za 59 na 60. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi

 

Share