065-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango wa Kukumbuka Mauti na Kupunguza Matarajio

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب ذكر الموت وقصر الأمل

065-Mlango wa Kukumbuka Mauti na Kupunguza Matarajio

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾

Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu. [Aal-'Imraan: 185]

 

وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani [Luqmaan: 34]

 

 

فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٤﴾

Basi utakapofika muda wao huo, hawatataakhari wala hawatatangulia saa. [Al-A'raaf: 34]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾

Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika.

 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾

Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, basi ningetoa swadaqah na ningelikuwa miongoni mwa Swalihina.

 

وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١١﴾

Lakini Allaah Haiakhirishi kamwe nafsi yeyote inapokuja ajali yake na Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo. [Al-Munaafiquwn: 9-11]

 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾

Mpaka itakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: Rabb wangu! Nirejeshe (duniani). 

 

لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾

Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha. (Ataambiwa) Laa hasha! Hakika hilo ni neno alisemaye yeye tu.  Na nyuma yao kuna barzakh mpaka Siku watakayofufuliwa.

  

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿١٠١﴾

Basi itakapopulizwa baragumu, hakutokuwa na unasaba baina yao Siku hiyo, na wala hawatoulizana. 

 

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾

Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu.

  

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾

Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; katika Jahannam ni wenye kudumu. 

 

تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Moto utababua nyuso zao; nao humo watakuwa ni wenye midomo iliyosinyaa na kuvutika mbali na meno.

  

أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٠٥﴾

(Wataambiwa): Je, hazikuwa Aayaat Zangu zinasomwa kwenu na nyinyi mkawa mnazikadhibisha?

 

إِلَى قَوْله تَعَالَى :

 

قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ ﴿١١٢﴾

(Allaah) Atasema: Muda gani mlikaa katika ardhi kwa idadi ya miaka?

  

قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ ﴿١١٣﴾

Watasema: Tumekaa siku au sehemu tu ya siku. Basi waulize wanaohesabu.

 

قَالَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ لَّوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١٤﴾

(Allaah) Atasema: Hamkukaa (huko duniani) isipokuwa kidogo tu, lau mngelikuwa mnajua.

  

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾

Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa? [Al-Muuminuwn: 99-115]

 

 

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki. [Al-Hadiyd: 16]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : أخذ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِمِنْكَبي ، فَقَالَ : ((  كُنْ في الدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ )) . وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ رضي الله عنهما ، يقول : إِذَا أمْسَيْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ الصَّبَاحَ ، وَإِذَا أصْبَحتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ المَسَاءَ ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ ، وَمِنْ حَيَاتِكَ  لِمَوْتِكَ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akisema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaau 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishika mabega yangu akasema: 'kuwa duniani kana kwamba ni mgeni au mpita njia.' Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) alikuwa akisema: 'Na ukichelewa usingoje asubuhi, na unapopambazuka usingoje jioni. Na chukua uzima wako kwa ajili ya maradhi yako. Na chukua uhai wako kabla ya mauti yako." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا حَقُّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ ، لَهُ شَيْءٌ يُوصِي فِيهِ ، يَبيتُ لَيْلَتَيْنِ إِلاَّ وَوَصِيَّتُهُ مَكْتُوبَةٌ عِنْدَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، هَذَا لفظ البخاري .

وفي روايةٍ لمسلمٍ : ((  يَبِيتُ ثَلاَثَ لَيَالٍ )) قَالَ ابن عمر : مَا مَرَّتْ عَلَيَّ لَيْلَةٌ مُنْذُ سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ ذَلِكَ إِلاَّ وَعِنْدِي وَصِيَّتِي .

Na imepokewa kutoka kwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa Muislamu ambaye ana kitu cha kuusia (kitu ambacho kinaweza kurithiwa na warithi wake) kulala masiku mawili ila tayari ameandika usia wake." [Al-Bukhaariy na Muslim, hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]

Na katika riwaayah ya Muslim: "Analala masiku matatu." Amesema Ibn 'Umar: "Haijapita kwangu usiku mmoja baada ya kusikia maneno haya kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa nina usia wangu."

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : خَطَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم خُطُوطاً ، فَقَالَ : ((  هَذَا الإنْسَانُ ، وَهَذَا أجَلُهُ ، فَبَيْنَمَا هُوَ كَذَلِكَ إذْ جَاءَ الخَطُّ الأَقْرَبُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Alichora Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mistari mingi akasema: Huyu ni mwanadamu na 'Msitari huu ni ajali yake. Akiwa hivyo anajiwa na msitari wa karibu" (yaani mauti)." [Al-Bukhaariy] 

 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : خَطَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم خَطّاً مُرَبَّعاً ، وَخَطَّ خَطّاً في الوَسَطِ خَارِجَاً مِنْهُ ، وَخَطَّ خُطَطاً صِغَاراً إِلَى هَذَا الَّذِي في الْوَسَطِ مِنْ جَانِبهِ الَّذِي في الوَسَط ، فَقَالَ : ((  هَذَا الإنْسَانُ ، وَهذَا أجَلُهُ مُحيطاً بِهِ – أَوْ قَدْ أحَاطَ بِهِ – وَهذَا الَّذِي هُوَ خَارِجٌ أمَلُهُ ، وَهذِهِ الْخُطَطُ الصِّغَارُ الأَعْرَاضُ ، فَإنْ أخْطَأَهُ هَذَا ، نَهَشَهُ هَذَا ، وَإنْ أخْطَأَهُ هَذَا ، نَهَشَهُ هَذَا )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichora hati ya mraba, akachora msitari katikati nje yake. Akachora mistari midogo kuelekea huu wa kati toka upande wake ambao uko katikati. Akasema: 'Huyu ni mwanadamu, na hii ni ajali yake imemzunguka, au imeshamkuta. Na huu ulio nje ni matarajio yake, hii mistari midogo ni mitihani, Unapomkosa huu basi anapatwa na huu; unapomkosa huu anakutwa na huu." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه  : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  بَادِرُوا بِالأعْمَالِ سَبْعاً ، هَلْ تَنْتَظِرُونَ إِلاَّ فَقْراً مُنْسِياً ، أَوْ غِنَىً مُطْغِياً ، أَوْ مَرَضَاً مُفْسداً ، أَوْ هَرَماً مُفَنِّداً ، أَوْ مَوْتَاً مُجْهِزاً ، أَوْ الدَّجّالَ ، فَشَرُّ غَائِبٍ يُنْتَظَرُ ، أَوْ السَّاعَةَ وَالسَّاعَةُ أدْهَى وَأمَرُّ ؟! )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Harakisheni kufanya amali, kabla ya mambo saba: Je, mnangojea ufakiri unaosahaulisha, au utajiri unaopoteza, au maradhi yenye kuharibu siha, au uzee unaoharibu akili, au mauti ya ghafla, au kuja kwa Dajjaal naye ni shari iliyojificha inayongojewa, au Qiyaamah ni tukio gumu na chungu." [At-Tirmidhiy, ambaye alisema ni Hadiyth Hasan].

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  أكْثِرُوا ذِكْرَ هَاذِمِ اللَّذَّاتِ )) يَعْنِي : المَوْتَ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameseam: "Zidisheni kukumbuka kiondoa ladha" (yaani umauti)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].

 

 

Hadiyth – 7

وعن أُبَيِّ بن كعبٍ رضي الله عنه : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا ذَهَبَ ثُلُثُ اللَّيْلِ قَامَ ، فَقَالَ : ((  يَا أَيُّهَا النَّاسُ ، اذْكُرُوا اللهَ ، جَاءتِ الرَّاجِفَةُ ، تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ ، جَاءَ المَوْتُ بِمَا فِيهِ ، جَاءَ المَوْتُ بِمَا فِيهِ )) قُلْتُ : يَا رسول الله ، إنِّي أُكْثِرُ الصَّلاَةَ عَلَيْكَ ، فَكَمْ أجْعَلُ لَكَ مِنْ صَلاَتِي ؟ فَقَالَ : ((  مَا شِئْتَ )) قُلْتُ : الرُّبُع ، قَالَ :   ((  مَا شِئْتَ ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ )) قُلْتُ : فَالنِّصْف ؟ قَالَ : ((  مَا شِئْتَ ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ )) قُلْتُ : فالثُّلُثَيْنِ ؟ قَالَ : ((  مَا شِئْتَ ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ )) قُلْتُ : أجعَلُ لَكَ صَلاَتِي كُلَّهَا ؟ قَالَ : ((  إذاً تُكْفى هَمَّكَ ، وَيُغْفَر لَكَ ذَنْبكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ubayy bin Ka'b (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akiamka thuluthi ya mwisho ya usiku na kusema: "Enyi watu! Mtajeni Allaah! Tetemeko limekuja, likifuatiwa na raa-di, mauti yamekuja na yalio ndani yake." Nikamuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nimeongeza kukuswalia. Je, nikutengee kiasi gani kwenye Swalaah yangu?" Akasema: "Unavyotaka." NIkasema: "Je, robo?" Akasema: "Unavyo penda na ukizidisha ni bora kwako." Nikasema: "Je, nusu?" Akasema: "Unavyo penda na ukizidisha ni bora kwako." Nikasema: "Je, thuluthi mbili (2/3)?" Akasema: "Unavyo penda na ukizidisha ni bora kwako." Nikasema: "Je, nijaalie swalaah yangu ni yako?" Akasema: "Basi utatoshwa hamu yako, na kufutiwa dhambi yako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].

 

 

 

 

 

Share