067-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karaha ya Kutamani Umauti Kwa Sababu ya Dhara Iliyomkumba na Haina Tatizo Ikiwa Anahofia Fitna Katika Dini

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

بابُ كراهة تمنّي الموت بسبب ضُرّ نزل بِهِ وَلاَ بأس بِهِ لخوف الفتنة في الدين

067-Mlango Wa Karaha ya Kutamani Umauti Kwa Sababu ya Dhara Iliyomkumba na Haina Tatizo Ikiwa Anahofia Fitna Katika Dini

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لا يَتَمَنَّ أحَدُكُمُ المَوْتَ ، إمَّا مُحْسِناً فَلَعَلَّهُ يَزْدَادُ ، وَإمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ البخاري .

وفي رواية لمسلم عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم  ، قَالَ : ((  لاَ يَتَمَنَّ أَحَدُكُمُ المَوْتَ ، وَلاَ يَدْعُ بِهِ مِنْ قَبْلِ أنْ يَأتِيَهُ ؛ إنَّهُ إِذَا مَاتَ انْقَطَعَ عَمَلُهُ ، وَإنَّهُ لاَ يَزِيدُ المُؤْمِنَ عُمُرُهُ إِلاَّ خَيْراً )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asitamani mmoja wenu mauti kwani kama kama ni mtu mwema huenda akazidisha amali njema. Na ama akiwa ni mtu muovu (mwenye kufanya madhambi) huenda akatubia (na kutadaraki yalioyopita)." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]

Katika riwaayah ya Muslim kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asitamani mmoja wenu umauti wala asiwe ni mwenye kujiombea kabla hayajamfikia, kwani akiaga dunia amali yake yote hukatika. Na kwa hakika umri wa Muumini hauongezeki ila huleta kheri zaidi."

 

 

Hadiyth – 2

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  لاَ يَتَمَنَّيَنَّ أحَدُكُمُ المَوْتَ لِضُرٍّ أصَابَهُ ، فَإنْ كَانَ لاَ بُدَّ فَاعِلاً ، فَلْيَقُلْ : اللَّهُمَّ أحْيِني مَا كَانَتِ الحَيَاةُ خَيْراً لي ، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَت الوَفَاةُ خَيراً لي )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asitamani mmoja wenu mauti kwa sababu ya madhara yaliyomsibu. Ikiwa hapana budi mpaka atamani basi aseme: 'Ee Mola wangu nipe uhai ikiwa una kheri na mimi na unifishe ikiwa kuaga dunia kwangu ni kheri kwangu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن قيسِ بن أَبي حازم ، قَالَ : دَخَلْنَا عَلَى خَبَّاب بن الأرَتِّ رضي الله عنه نَعُودُهُ وَقَدِ اكْتَوَى سَبْعَ كَيَّاتٍ ، فَقَالَ : إنَّ أَصْحَابَنَا الَّذِينَ سَلَفُوا مَضَوْا ، وَلَمْ تَنْقُصْهُمُ الدُّنْيَا ، وَإنَّا أصَبْنَا مَا لاَ نَجِدُ لَهُ مَوْضِعاً إِلاَّ التُّرَابَ وَلولا أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم نَهَانَا أنْ نَدْعُوَ بالمَوْتِ لَدَعَوْتُ بِهِ . ثُمَّ أتَيْنَاهُ مَرَّةً أُخْرَى وَهُوَ يَبْنِي حَائِطاً لَهُ ، فَقَالَ : إنَّ المُسْلِمَ لَيُؤْجَرُ فِي كُلِّ شَيْءٍ يُنْفِقُهُ إِلاَّ فِي شَيْءٍ يَجْعَلُهُ في هَذَا التُّرَابِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ رواية البخاري

Imepokewa kutoka kwake Qays bin Abu Haazim amesema: Tulimtembelea Khabbaab bin Al-Aratt (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipokuwa mgonjwa. Mishipa yake ya damu ilikuwa imefunguliwa mahali saba. Alituambia: "Hakika sahibu zetu waliotangulia wamepita, Dunia haikuwapunguza. Kwa hakika sisi tumepata ambayo hayan mahali isipokuwa udongo. Na lau sio Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutukataza kuomba mauti ningeyaomba." Kisha tulimzuru mara nyingine tukamkuta anajenga ukuta wake, akasema: "Hakika Muislaamu analipwa kwa kila kitu anachotoa isipokuwa kitu anachokijalia katika huu udongo." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy] 

 

 

 

 

Share