Borhowa

Borhowa

Vipimo 

Daal (lentils) nyekundu au/na kijani - 1 Kikombe kikubwa
 
 Bizari ya manjano ya unga - 1/2 Kijiko cha chai
 
 Pili pili ya unga - 1/2 kijiko cha chai
 
 Chumvi - Kiasi
 
 Maji ya ndimu - 3 Vijiko vya supu
 
 Kitunguu - 1 kiasi
 
 Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai
 
 Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai
 
 Mafuta ya kukaangia - Kiasi
 
 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Safisha daal kwa kutoa mawe ikiwa yapo, kisha osha na roweka   dakika 15 hivi.
  2.  Kisha chemsha kwa kutia maji, bizari ya manjano, chumvi, pili pili  ya unga na maji ya ndimu hadi iive na kuvurujika.  
  3.  Halafu chukua kisufuria na kaanga kitungu, kisha thomu na mwisho tia bizari ya pilau.  
  4. Kisha mimina mchanganyiko wa kitunguu kwenye sufuria ya daal (iliyokwisha iiva)na uchanganye na iwache motoni kidogo itokote.  
  5.  Ukipenda mimina mchanganyiko kwenye blenda na usage mpaka iwe laini.  
  6.  Tia kwenye bakuli na itakuwa tayari kuliwa na wali na samaki ukipenda.
Share