Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

 

 

 

Vipimo

Mchele wa basmati -  4 cups

Samaki nguru (king fish) - 7 vipande au zaidi

Kitunguu - 5

Nyanya/tungule - 3

Njegere - 1 kikombe

Snuwbar (njugu za pine) - 1 kikombe

Viazi - 2 kata kata mapande makubwa

Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu - 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu - 1 kijiko cha chai

Bizari ya biriani/garama masala - 1 kijiko cha supu

 

 

Namna Ya Kupika:

  1. Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda.
  2. Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili.
  3. Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange.
  4. Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere,  njugu za snuwbar na ndimu kavu.
  5. Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia.
  6. Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki.
  7. Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani.
  8. Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.

 

 

Njugu Za Snuwbar:

  

 

 

Share