04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Hajj Na 'Umrah: Miongoni Mwa Fadhila Za Hajj

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Hajj Na ‘Umrah

 

04-Miongoni Mwa Fadhila Za Hajj

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

1- Hajj inafuta madhambi ya miaka iliyopita

 

(a) Toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((من حج فلم يرفث ولم يفسق رجع كيوم ولدته أمه))

((Aliyehiji na hakuzungumza maneno yasiyolaiki na hakufanya mabaya wala maasia, hurejea kama siku mama yake aliyomzaa)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350)]

 

(b) ‘Amru bin Al-‘Aaswiy alipotaka kumpa bay-’a Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) ya kuingia katika Uislamu (kusilimu), alishurutisha asamehewe madhambi yake. Rasuli akamwambia:

((أما علمت أن الاسلام يهدم ما قبله، وأن الهجرة تهدم ما قبلها، وأن الحج يهدم ما قبله؟))

((Hivi hujui kuwa kusilimu kunapomosha na kufuta madhambi ya nyuma yake, na kwamba Hijra inapomosha na kufuta madhambi ya kabla yake, na kwamba Hajj inapomosha na kufuta madhambi ya kabla yake?)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (121)]

 

 

2- Hajj ni sababu ya kuachwa mtu huru na moto

 

Toka kwa ‘Aaishah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((ما من يوم أكثر أن يعتق الله فيه عبدا من النار من يوم عرفة، وإنه ليدنو ثم يباهي بهم الملائكة))

((Hakuna siku  iliyo na wingi zaidi wa Allaah kuwaacha huru waja na moto kuliko Siku ya Arafah, na hakika Yeye Hukurubia kisha Hujifaharisha nao kwa Malaika)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1348)]

 

 

3- Hajj malipo yake ni Pepo

 

Toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما، والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة))                        

((‘Umrah hadi ‘Umrah ni kafara kati yao, na Hajj salama iliyotakasika na chochote cha kuiharibu [Mabruwr], haina malipo mengine isipokuwa Pepo)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1773) na Muslim (1349)]

 

 

4- Hajj ni katika ‘amali bora kabisa

 

Toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) aliulizwa: Ni ‘amali ipi bora zaidi?. Akasema:

 

((إيمان بالله ورسوله)) قيل: ثم ماذا؟ قال: ((جهاد في سبيل الله))، قيل: ثم ماذا؟ قال: ((حج مبرور))

((Kumwamini Allaah na Rasuli Wake)). Akaulizwa: Kisha ipi? Akasema: ((Jihaad katika Njia ya Allaah)). Akaulizwa: Kisha ipi? Akasema: ((Hajj salama iliyotakasika na chochote cha kuiharibu)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (26) na Muslim (83)]

 

 

5- Hajj ni Jihaad bora zaidi ya wanawake

 

Toka kwa ‘Aaishah alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Tunaona Jihaad kuwa ‘amali bora zaidi, kwa nini na sisi tusende Jihadini? Akasema:

((لا، ولكنّ أفضل الجهاد: حج مبرور))

((Hapana, nyinyi mna Jihaad bora zaidi; Hajj salama iliyotakasika na chochote cha kuiharibu)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1520), An-Nasaaiy (5/114) na Ibn Maajah (290)]

 

 

 

 

Share