Kamba (Prawns) Katika Sosi Ya Nyanya Na Nazi

Kamba (Prawns) Katika Sosi Ya Nyanya NaNazi

Vipimo 

 

Kamba- kilo 1

Chumvi - Kiasi

Mafuta- ¼ Kikombe

Bizari ya pilau (cummin) nzima - ½ Kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai

Vitungu- 2  katakata slesi ndogo ndogo

Nyanya zilioiiva - 3 katakata

Pilipili  mbuzi - kiasi 2

Tui la nazi - vikombe 2

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika    

  1. Osha kamba kisha wachuje maji.
  2. Katika karai, weka mafuta yapate moto, tia bizari ya pilau lakini usiache ikaunguwa.
  3. Kisha tia vitungu na ukaange hadi vibadilike rangi ya hudhurungi lakini zisiungue.
  4. Halafu tia nyanya, bizari ya mchuzi. Tia pilipili mbuzi.
  5. Tia kamba changanya na tia  maji kidogo sana waive.
  6. Tui la nazi, iache motoni kidogo..
  7. Epua katika chombo tayari kuliwa.  

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

   
 

Share