Mchuzi Wa Papa Wa Nazi Na Bamia

Mchuzi Wa Papa Wa Nazi  Na Bamia

Vipimo 

Papa - 8 vipande 

Kitunguu maji - 2 

Nyanya/tungule - 3 

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko 

Karoti -  1 

Pilipili hoho - 1 

Bamia - 10 

Chumvi - kiasi 

Bizari ya mchuzi - 2 vijiko vya chai  

Haldi/tumeric/bizari manjano - ½ kijiko cha chai 

Ndimu - 1 kamua 

Nazi - 1 

Mafuta - 3 vijiko vya supu  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Roweka vipande vya papa kwa maji ya moto kisha toa maganda yake. 
  2. Kosha na maji ya kawaida weka kando.  
  3. Kuna nazi na toa tui zito na tui maji.  
  4. Katakata vipande vidogodogo, vitunguu, nyanya/tungule, kitunguu na kitunguu thomu.  
  5. Kata karoti na bamia vipande virefu virefu  
  6. Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu, nyanya, kitunguu thomu.  
  7. Tia papa na pilipili hoho, endelea kukaanga na mchanganyiko.  
  8. Tia karoti na bamina na kisha tia  tui maji kikombe kimoja na ndimu iwivishe papa, karoti na bamia..  
  9. Tia tui zito.

 

 

 

 

Share