033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 23: مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 23

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى)

 

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾

Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliokuwa wakweli kutimiza waliyoahidiana na Allaah; basi miongoni mwao waliotimiza nadhiri yao; (wamekufa shahidi), na miongoni mwao wanaongojea na hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.  [Al-Ahzaab (33:23)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ الْخُزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الأَعْلَى، عَنْ حُمَيْدٍ، قَالَ سَأَلْتُ أَنَسًا‏.‏ حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ زُرَارَةَ، حَدَّثَنَا زِيَادٌ، قَالَ حَدَّثَنِي حُمَيْدٌ الطَّوِيلُ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ غَابَ عَمِّي أَنَسُ بْنُ النَّضْرِ عَنْ قِتَالِ بَدْرٍ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، غِبْتُ عَنْ أَوَّلِ قِتَالٍ قَاتَلْتَ الْمُشْرِكِينَ، لَئِنِ اللَّهُ أَشْهَدَنِي قِتَالَ الْمُشْرِكِينَ لَيَرَيَنَّ اللَّهُ مَا أَصْنَعُ، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ أُحُدٍ وَانْكَشَفَ الْمُسْلِمُونَ قَالَ ‏"‏ اللَّهُمَّ إِنِّي أَعْتَذِرُ إِلَيْكَ مِمَّا صَنَعَ هَؤُلاَءِ ـ يَعْنِي أَصْحَابَهُ ـ وَأَبْرَأُ إِلَيْكَ مِمَّا صَنَعَ هَؤُلاَءِ ‏"‏ ـ يَعْنِي الْمُشْرِكِينَ ـ ثُمَّ تَقَدَّمَ، فَاسْتَقْبَلَهُ سَعْدُ بْنُ مُعَاذٍ، فَقَالَ يَا سَعْدُ بْنَ مُعَاذٍ، الْجَنَّةَ، وَرَبِّ النَّضْرِ إِنِّي أَجِدُ رِيحَهَا مِنْ دُونِ أُحُدٍ‏.‏ قَالَ سَعْدٌ فَمَا اسْتَطَعْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا صَنَعَ‏.‏ قَالَ أَنَسٌ فَوَجَدْنَا بِهِ بِضْعًا وَثَمَانِينَ ضَرْبَةً بِالسَّيْفِ أَوْ طَعْنَةً بِرُمْحٍ أَوْ رَمْيَةً بِسَهْمٍ، وَوَجَدْنَاهُ قَدْ قُتِلَ وَقَدْ مَثَّلَ بِهِ الْمُشْرِكُونَ، فَمَا عَرَفَهُ أَحَدٌ إِلاَّ أُخْتُهُ بِبَنَانِهِ‏.‏ قَالَ أَنَسٌ كُنَّا نَرَى أَوْ نَظُنُّ أَنَّ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ فِيهِ وَفِي أَشْبَاهِهِ ‏((‏مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ‏))‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ‏.‏

 

Ametuhadithia Muhammaad bin Sa’iyd Al-Khuzaaiy, ametuhadithia ‘Abdul-A-‘alaa toka kwa Humayd, amesema, nilimuuliza Anas, amesema, na amenihadithia ‘Amri bin Zaraarah, ametuhadithia Ziyaad amesema, amenihadithia Humayd At-Twawiyl toka kwa Anas (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: Ami yangu Anas bin An-Nadhwr alikosekana kwenye Vita vya Badr, akamwambia Rasuli: Ee Rasuli wa Allaah! Nilikosekana katika vita vya kwanza ulivyopambana na washirikina. Na ikiwa Allaah Ataniwezesha kushiriki vita vya kupambana na washirikina, basi hakika Allaah Ataona vipi nitakavyopambana kishujaa. Ilipokuwa Siku ya (Vita vya) Uhud, na Waislamu wakalemewa na kukimbia alisema: Ee Allaah! Naomba udhuru kwa waliyoyafanya hawa – yaani wenzake Swahaba - (walenga mishale ambao walikaidi agizo la Rasuli kwao la kutoondoka pale alipowapanga juu ya mlima, wakateremka chini kukusanya ngawira), na najitakasa na kujivua Kwako kutokana na waliyoyafanya hawa – yaani washirikina- (ya kuwapiga vita Waislamu na kumuudhi Rasuli wa Allaah Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha akasonga mbele (na upanga wake), na akakutana na Sa’ad bin Mu’aadh (akikimbia vita). Akamwambia: Ee Sa’ad bin Mu’aadh (mimi naihisi) Jannah (Pepo). Naapa kwa Rabb wa An-Nadhwr, hakika mimi nainusa harufu yake mbele ya Jabal Uhud. Sa’ad akasema: Sikuweza ee Rasuli wa Allaah kufanya aliyoyafanya (ya kusonga mbele na kupambana kishujaa na washirikina). Anas anasema: Tukamkuta ameuawa (kishahidi) na ana zaidi ya majeraha themanini ya kati ya kupigwa panga, kuchomwa mkuki na kulengwa mishale, na washirikina wamemkata baadhi ya viungo vyake na kuitweza maiti yake.  Hakuna aliyeweza kumtambua isipokuwa dada yake kwa ncha za vidole vyake. Anas amesema: Tulikuwa tunaona au tunadhani kuwa Aayah hii imeteremka kumzungumzia yeye na wenye msimamo na ushujaa kama wake:

 

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ 

Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliokuwa wakweli kutimiza waliyoahidiana na Allaah… mpaka mwisho wa Aayah” [Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Sita ukurasa wa 361]

 

[Al-Bukhaariy ameitaja Hadiyth hii vile vile kwa ufupi kwenye Kitaab At-Tafsiyr Mujallad wa Kumi ukurasa wa 136 kwa Sanad nyingine inayoishia kwa Anas. Al-Haafidh katika Al Fat-h Mujallad wa Sita ukurasa wa 361 na Al-Haafidh Ibn Kathiyr katika At-Tafsiyr Mujallad wa Tatu ukurasa wa 475 wamesema: “Muslim, At-Tirmidhiy [At-Tirmidhiy amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 163], na An-Nasaaiy wameikhariji toka riwaayah ya Thaabit aliyepokea toka kwa Anas. Na imekharijiwa na Ahmad katika Mujallad wa Tatu ukurasa wa 194, At-Twayaalsiy katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 22, Ibn Jariyr katika Mujallad wa Ishirini na Moja ukurasa wa 147 na Abu Nu’aym katika Al-Hilyah Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 121 pamoja na ‘Abdullaah bin Mubaarak katika Al-Jihaad ukurasa wa 68].

 

 

Share