033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 51: تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 51

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَلِيمًا ﴿٥١﴾

Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako. Hivyo ni karibu zaidi kupelekea kuburudika macho yao, na wala wasihuzunike, na waridhike kwa yale uliyowapa kila mmoja wao. Na Allaah Anajua yale yaliyomo nyoyoni mwao. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu. Ahzaab (33:51)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا زَكَرِيَّاءُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، قَالَ هِشَامٌ حَدَّثَنَا عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: كُنْتُ أَغَارُ عَلَى اللاَّتِي وَهَبْنَ أَنْفُسَهُنَّ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَقُولُ أَتَهَبُ الْمَرْأَةُ نَفْسَهَا فَلَمَّا أَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى ‏((‏تُرْجِئُ مَنْ تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَنْ تَشَاءُ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلاَ جُنَاحَ عَلَيْكَ‏))‏ قُلْتُ مَا أُرَى رَبَّكَ إِلاَّ يُسَارِعُ فِي هَوَاكَ‏.‏

Ametuhadithia Zakariyya bin Yahyaa, ametuhadithia Abu Usaamah akisema: Hishaam ametuhadithia toka kwa baba yake toka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba amesema: Nilikuwa nawafanyia wivu wanawake ambao wanajitoa wenyewe kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   (ili awaoe bila mahari) nikisema (na kustaajabu): Mwanamke anajitoa mwenyewe hivi?! Na Allaah Ta’aalaa Alipoteremsha:

 

تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ 

Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako.

 

nilisema: Naona Rabb wako Hakawii kabisa katika kukidhi matashi yako (ya kuoa, kukuruhusu kupanga zamu za kulala kwa wakezo upendavyo mwenyewe na kukutanulia mambo yako uridhike)”.

 

[Al-Bukhaariy Mujallad wa 10 ukurasa wa 144]

 

[Hadiyth hii imesimuliwa na Muslim katika Mujallad wa 1 ukurasa wa 49. Walioikhariji ni Ahmad katika Mujallad wa 6 ukurasa wa 158, Ibn Jariyr katika Mujallad wa 22 ukurasa wa 26, na Al-Haakim katika Al-Mustadrak Mujallad wa 2 ukurasa wa 436 ambapo ameeleza humo akisema: “Allaah Akateremsha Aayah hii kwa Wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kisha akasema: Hadiyth hii ni Swahiyh juu ya sharti ya Mashekhe Wawili [Al-Bukhaariy na Muslim], na wao hawakuikharji kwa tamko hili, na Adh-Dhahabiy ameikubali”.

 

 

Share