59-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ujira Wa Ummah Wake Ni Zaidi Kuliko Ujira Wa Umati Za Nyuma

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

59-Ujira Wa Ummah Wake Ni Zaidi Kuliko Ujira Wa Umati Za Nyuma

 

Alhidaaya.com

 

 

Kutokana na Rahmah za Allaah (سبحانه وتعالى) na Fadhila zake kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), Amejaalia Ummah wa Kiislamu kupata fadhila hii ya kuwa thawabu za ‘amali za Waumini ni nyingi kulikoni thawabu za ‘amali walizotenda Umati zilizotangulia. Hadiyth na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zimethibiti hayo kama ifuatavyo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِنَّمَا مَثَلُكُمْ وَالْيَهُودُ وَالنَّصَارَى كَرَجُلٍ اسْتَعْمَلَ عُمَّالاً فَقَالَ مَنْ يَعْمَلُ لِي إِلَى نِصْفِ النَّهَارِ عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ فَعَمِلَتِ الْيَهُودُ عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ، ثُمَّ عَمِلَتِ النَّصَارَى عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ، ثُمَّ أَنْتُمُ الَّذِينَ تَعْمَلُونَ مِنْ صَلاَةِ الْعَصْرِ إِلَى مَغَارِبِ الشَّمْسِ عَلَى قِيرَاطَيْنِ قِيرَاطَيْنِ، فَغَضِبَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ عَمَلاً وَأَقَلُّ عَطَاءً، قَالَ هَلْ ظَلَمْتُكُمْ مِنْ حَقِّكُمْ شَيْئًا قَالُوا لاَ‏.‏ فَقَالَ فَذَلِكَ فَضْلِي أُوتِيهِ مَنْ أَشَاءُ ‏"‏‏.‏

 Amesimulia ‘Abdillaahi bin ‘Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنهما)   kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Hakika mfano wenu na mfano wa Mayahudi na Manaswara ni mfano wa mtu aliyewaajiri vibarua, akawaambia: ‘Nani atakayenifanyia kazi kuanzia asubuhi mpaka mchana (saa sita) kwa Qiraatw moja?’ Mayahudi walikubali na kutekeleza kazi hiyo kwa Qiraatw moja; na kisha Manaswara wakafanya kazi mpaka Swalaah ya Alasiri kwa Qiraatw; na sasa nyinyi Waislamu mnafanya kazi kuanzia Swalaah ya Alasiri mpaka machweo kwa Qiraatw mbili kila mmoja.” Mayahudi na Manaswara walighadhibika, na wakasema: ‘Kwa nini tufanye kazi zaidi kwa malipo duni? Mwajiri (Allaah) Akawauliza: “Je, Nimenyakua haki yenu? Wakasema: ‘Hapana.’ Akasema: Hiyo ni Fadhila Yangu, Ninampatia Nimtakaye." [Al-Bukhaariy]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾ لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾

 

28. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakughufurieni; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. 29. Ili wajue Ahlul-Kitaabi kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu. [Al-Hadiyd: 28 – 29]

 

 

Na pindi Ahlul-Kitaab wakisilimu kwa kumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), basi wameahidiwa kupata ujira mara mbili katika ‘amali zao kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾ وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾ أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾

52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao wanaiamini (Qur-aan). 53. Na wanaposomewa husema: Tumeiamini, hakika hiyo ni haki kutoka Rabb wetu, hakika Sisi kabla yake tulikuwa Waislamu waliojisalimisha. 54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa. [Al-Qaswasw: 52 – 54]

 

 

Na Hadiyth ifuatayo inaunga mkono:

 

 

حدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ حَىٍّ أَبُو حَسَنٍ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَاهُ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ ثَلاَثَةٌ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُمْ مَرَّتَيْنِ الرَّجُلُ تَكُونُ لَهُ الأَمَةُ فَيُعَلِّمُهَا فَيُحْسِنُ تَعْلِيمَهَا، وَيُؤَدِّبُهَا فَيُحْسِنُ أَدَبَهَا، ثُمَّ يُعْتِقُهَا فَيَتَزَوَّجُهَا، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَمُؤْمِنُ أَهْلِ الْكِتَابِ الَّذِي كَانَ مُؤْمِنًا، ثُمَّ آمَنَ بِالنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ الَّذِي يُؤَدِّي حَقَّ اللَّهِ وَيَنْصَحُ لِسَيِّدِهِ ‏"‏‏.‏ ثُمَّ قَالَ الشَّعْبِيُّ وَأَعْطَيْتُكَهَا بِغَيْرِ شَىْءٍ وَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يَرْحَلُ فِي أَهْوَنَ مِنْهَا إِلَى الْمَدِينَةِ‏.‏

Imepokewa kwa babake Abu Burdah (رضي الله عنه) amesema: “Watu watatu watapewa ujira wao mara mbili: Mtu aliye na kijakazi, naye akamsomesha inavyotakiwa na akamfundisha adabu njema, kisha akamuacha huru na kumuoa. Mtu huyo atapata ujira mara mbili. Na Muumini miongoni mwa Ahlul-Kitaab, ambaye alikuwa Muumini, kisha akamuamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa anayetekeleza haki za Allaah na akawa na ikhlasi kwa bwanake”.  [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share