042-Asbaabun-Nuzuwl: Ash-Shuwraa Aayah 23: قُلْ لا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 042-Asbaabun-Nuzuwl Ash-Shuwraa Aayah 23

 

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّـهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ۗ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ شَكُورٌ﴿٢٣﴾

Hayo ndiyo Aliyowabashiria Allaah waja Wake wale walioamini na wakatenda mema. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu. Na yeyote yule anayechuma mazuri, Tutamzidishia humo zuri. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Ash-Shuwraa (42:23)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حدثنا يحيى عن شعبة حدثني عبد الملك بن ميسرة عن طاووس قال أتى ابن عباس رجل فسأله. وسليمان بن داود قال أخبرنا شعبة أنبأني عبد الملك قال سمعت طاووسا يقول سأل رجل ابن عباس المعنى عن قول الله عز وجل ((قُلْ لا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى)) فقال سعيد بن جبير قربى محمد صلى الله عليه وعلى آله وسلم قال ابن عباس عجلت إن رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم لم يكن بطن من قريش إلا لرسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فيهم قرابة فنزلت ((قُلْ لا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى)) إلا أن تصلوا قرابة ما بيني وبينكم-.

Ametuhadithia Yahyaa, toka kwa Shu‘ubah, amenihadithia ‘Abdul-Malik bin Maysarah, toka kwa Twaawuws amesema: Mtu alimwendea Ibn ‘Abbaas akamuuliza. Na Sulaymaan bin Daawuwd amesema: Ametueleza Shu‘ubah, amenijuvya ‘Abdul-Malik amesema: Nimemsikia Twaawuws akisema: Mtu mmoja alimuuliza Ibn ‘Abbaas kuhusu maana ya Kauli Yake Allaah (عز وجل):  

قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu. [Ash-Shuwraa (42:23)]

 

Sa’iyd bin Jubayr (ambaye alikuwepo hapo) akasema: Ni Jamaa wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Ibn ‘Abbaas akamwambia: Umeharakia (kujibu). Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuna tumbo lolote katika Maquraysh, isipokuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ana ukaraba ndani yao. Na hapo ikateremka:

قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu. [Ash-Shuwraa (42:23)] -Sitaki kutoka kwenu chochote isipokuwa muwe tu wema kwangu kutokana na ukaraba kati yangu mimi na nyinyi”- [Maneno ya Ibn ‘Abbaas akisherehesha Aayah].
 

[Ahmad katika Mujallad wa 1 Uk. wa 229]

 

Hadiyth iko kwa Al-Bukhaariy toka Hadiyth ya Shu‘bah. At-Twabariy ameikhariji kama ilivyo hapa katika Mujallad wa 25 Uk. wa 23, nayo inasema: “Isipokuwa ukaraba ambao uko baina yangu na nyinyi, muunge (kwa kunitendea wema, kunisaidia na kutonifanyia vitimbi)”.

 

Al-Haafidh katika “Al-Matwaalib Al-‘Aaliyah” Mujallad wa 3 Uk. wa 368 ameinasibisha kwa Ahmad bin Maniy-’i, na amesema ni Swahiyh.

 

 

 

 

 

Share