Matunda Mchanganyiko Katika Juisi Ya Embe

Matunda Mchanganyiko Katika Juisi Ya Embe

VIPIMO 

Rojo La Embe (Mango pulp) - Kopo 1(850gm)

Maziwa - Nusu lita (1/2 litre)

Vanilla -  1/2 Kijiko cha chai   

'Arki (rose essence) - Vitone 3-4

 MATUNDA MAPYA (Fresh Fruit)

Zabibu nyekundu - 1 Vikombe

(chambua moja moja)

Zabibu za kijani - 1 Vikombe

Tikiti la asali (honey dew) -  1/2

(kata vipande vidogo vidogo

Shammaam (tikiti, cantelope) -  1/2

Kata kataka vipande vidogo vidogo

Mananasi (kata kataka vipande) - 1 Vikombe

Ndizi (kata kataka vipande) - 3

Papai (kata kataka vipande - 1/2

Matunda yoyote mengine unayopenda kama tofaha (apple), pea (pears)  peaches na kadhalika.

(Kata kata vipande vidogo vidogo na kila moja fanya Kikombe 1 kila tunda )

                                                                            

NAMNA YA KUTAYARISHA

1. Chukua bakuli  kubwa mimina  rojo la embe na maziwa changanya vizuri.

2. Tia vanilla na 'arki  koroga vizuri

3. Mimina matunda yako uliyoyakata changanya na weka kwenye friji ipate baridi

4. Ikishapata baridi vizuri itoe na tayari kwa kuliwa hasa baada ya chakula kama kitinda mlo.

5. Ukipenda unaweza kuongeza ice cream ya vanilla kwenye kibakuli chako unacholia.

KIDOKEZO

Kwa wale wasiotumia rojo la embe wanaweza kutumia maembe dodo ukayamenya, na kata kata vipande na usage kwenye mashine (blender) pamoja  na maziwa ili upate urojo mzito wa embe.

Hapo utaangalia uzito wa urojo unaoutaka au unaweza kuongeza maziwa kiasi.

 

Share