05-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Aliwaheshimu Watoto Na Kuwatimizia Haki Zao Na Mapendekezo Yao

 Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:

 

05-Aliwaheshimu Watoto Na Kuwatimizia Haki Zao Na Mapendekezo Yao 

 

Alhidaaya.com

 

Kutokana na huruma na upole wake na mapenzi yake na uadilifu wake, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaheshimu hata Watoto na Vijana kwa kuwatimizia haki zao na mapendekezo yao, akamtimizia kijana mmoja pendekezo lake la kutaka apewe yeye maziwa ambayo aliyabakisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika bilauri baada ya kunywa kama inavyoelezea Hadiyth ifuatayo:

 

  

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، حَدَّثَنَا أَبُو غَسَّانَ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أُتِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِقَدَحٍ فَشَرِبَ مِنْهُ، وَعَنْ يَمِينِهِ غُلاَمٌ أَصْغَرُ الْقَوْمِ، وَالأَشْيَاخُ عَنْ يَسَارِهِ فَقَالَ ‏ "‏ يَا غُلاَمُ أَتَأْذَنُ لِي أَنْ أُعْطِيَهُ الأَشْيَاخَ ‏"‏‏.‏ قَالَ مَا كُنْتُ لأُوثِرَ بِفَضْلِي مِنْكَ أَحَدًا يَا رَسُولَ اللَّهِ‏.‏ فَأَعْطَاهُ إِيَّاهُ‏.‏

 

Ametuhadithia Sa’iyd bin Abiy Maryama, ametuhadithia Abuu Ghassaan amesema: Amenihadithia Abuu Haazim kutoka kwa Sahl bin Sa’iyd (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  aliletewa bilauri (iliyojaa maziwa), akanywa na kuumeni mwake kulikuwa na kijana aliyekuwa mdogo wa wote waliokuwepo na wazee walikuwa kushotoni mwake. Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Ee kijana! Utaniruhusu niwapatie (kinywaji) wazee?” Akajibu: Ee Rasuli wa Allaah! Sitapendelea kumtanguliza yeyote juu yangu kunywa kutokana na ulichokunywa. Hivyo, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akampatia yeye (kijana kinywaji). [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share