01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikma Zake: Akikhafifisha Swalaah Za Jamaa Ili Lisiwe Jambo Zito Kwa Watu

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

01-Hikma Zake: Akikhafifisha Swalaah Za Jamaa Ili Lisiwe Jambo Zito Kwa Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth zifuatazo zinajieleza kuhusu hikma yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ya kukhafifisha Swalaah za jamaa ili isiwe ni jambo zito kwa wale walio dhaifu katika kubakia kwenye Swalaah ya jamaa kwa muda mrefu, au wenye dharura fulani:

 

 

 عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ رَجُلٌ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لاَ أَكَادُ أُدْرِكُ الصَّلاَةَ مِمَّا يُطَوِّلُ بِنَا فُلاَنٌ، فَمَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فِي مَوْعِظَةٍ أَشَدَّ غَضَبًا مِنْ يَوْمِئِذٍ فَقَالَ ‏ "‏ أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّكُمْ مُنَفِّرُونَ، فَمَنْ صَلَّى بِالنَّاسِ فَلْيُخَفِّفْ، فَإِنَّ فِيهِمُ الْمَرِيضَ وَالضَّعِيفَ وَذَا الْحَاجَةِ ‏"‏‏.‏

 

Abu Mas’uwd Al-Answaariy amesimulia: Mara moja mtu mmoja alimwambia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Ee Rasuli wa Allaah! Naweza nisihudhurie Swalaah ya jamaa kwa sababu fulani anarefusha Swalaah anapokuwa Imaam. Msimulizi akaongeza: “Sijawahi kumwaona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameghadhibika kiasi kile wakati wa kutoa nasaha. Akasema: “Enyi watu! Baadhi yenu mnawafanya wengine kuchukia amali njema (Swalaah). Hivyo yeyote akiwa Imaam kwenye Swalaah,  lazima afupishe kwa sababu miongoni mwao kuna wagonjwa, dhaifu na wahitaji.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia

 

  حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ دِينَارٍ، حَدَّثَنَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ مُعَاذَ بْنَ جَبَلٍ ـ رضى الله عنه ـ كَانَ يُصَلِّي مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ يَأْتِي قَوْمَهُ فَيُصَلِّي بِهِمُ الصَّلاَةَ، فَقَرَأَ بِهِمُ الْبَقَرَةَ ـ قَالَ ـ فَتَجَوَّزَ رَجُلٌ فَصَلَّى صَلاَةً خَفِيفَةً، فَبَلَغَ ذَلِكَ مُعَاذًا فَقَالَ إِنَّهُ مُنَافِقٌ‏.‏ فَبَلَغَ ذَلِكَ الرَّجُلَ، فَأَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّا قَوْمٌ نَعْمَلُ بِأَيْدِينَا، وَنَسْقِي بِنَوَاضِحِنَا، وَإِنَّ مُعَاذًا صَلَّى بِنَا الْبَارِحَةَ، فَقَرَأَ الْبَقَرَةَ فَتَجَوَّزْتُ، فَزَعَمَ أَنِّي مُنَافِقٌ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَا مُعَاذُ أَفَتَّانٌ أَنْتَ ـ ثَلاَثًا ـ اقْرَأْ ‏ وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا وَ‏ سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى ‏ وَنَحْوَهَا ‏"‏‏.‏

Imepokewa kwa ‘Amru bin Diynaar kuwa Jaabir bin ‘Abdillaah  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  amesema: Mu‘aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa anaswali pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  kisha anaenda kwa kaumu zake na anawaswalisha Swalaah na akawasomea Suwratul Baqarah. Akasema: Mtu mmoja akajitenga na safu na akaswali peke yake Swalaah nyepesi, na khabari hiyo ikamfikia Mu‘aadh, naye akasema: ‘Hakika huyo ni mnafiki.” Maneno hayo yakamfikia Yule mtu, naye akaenda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Sisi ni watu tunaofanya kazi kwa mikono yetu na tunamwagilia (mashamba) kwa ngamia wetu, hakika Mu‘aadh ametuswalisha usiku uliopita, akasoma Al-Baqarah, nikaharakisha na sasa anadai kuwa eti mimi ni mnafiki. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Mu‘aadh! Hivi wewe ni mfitini? Mara tatu, ‘Soma:

وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا 

[Ash-Shams (91)]

 

Na,

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى

[Al-A’laa (87)]

 

 na mfano wake.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share