Ummu 'Aliy (Misri)

Ummu 'Aliy (Misri)

VIPIMO

Kara-biskuti tamu - 450 gms au 16 oz

(Puffy Crispy Biskuits)

       au

(Biscuits Feuilletés)

 Maziwa - Lita  (litre)  1 na 1/4  

Malai (cream) - 340 gms au 12 oz 

Samli - 3 vijiko vya supu

Sukari -  1/2 kikombe au zaidi

Njugu za Pistachio                                        

(zilizokatwa ndogo ndogo) - 1/2  Kikombe

 Lozi (zilizokatwa ndogo ndogo) -   1/2 kikombe

Zabibu kavu -   1/2 kikombe

Vanilla -  1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Katakata kara-biskuti kama unazichambua katika bakuli la kupikia katika oveni.
  2. Chemsha maziwa pamoja na samli, sukari, njugu za pistachio, lozi, zabibu.
  3. Tia vanilla koroga ichanganyike vizuri.
  4. Ikichemka epua na mwagia kwenye kara-biskuti.
  5. Tupia malai (Cream)  juu yake ieneze vizuri.
  6. Pika katika moto wa 400º kwa muda wa dakika 20 au hadi ikauke na kara-biskuti zigeuke rangi kidogo kwa juu.
  7. Tayari kuliwa.

VIDOKEZO:

  1. Inaweza kuliwa ikiwa ya vuguvugu na sio lazima iwe baridi.
  2. Unaweza kutumia mikate yake khaswa ya kupikia Ummu 'Aliy inayouzwa katika bekari au tumia puff-pastry, uipikie kwanza katika oveni hadi iwive kisha ichambue chambue kama kara-biskuti.

  

Share