04-Hadiyth Husnul-Khuluq: Sifa Nyepesi Na Amali Aipendayo Zaidi Allaah Na Nzito Katika Miyzaan Siku Ya Qiyaamah

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  4

 

Sifa Nyepesi Na Amali Aipendayo Zaidi Allaah Na Nzito Katika Miyzaan Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عنْ أَنَسٍ قَالَ لَقِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا ذَرٍّ فَقَالَ: ((يَا أَبَا ذَرٍّ أَلا أَدُلُّكَ عَلَى خَصْلَتَيْنِ هُمَا أَخَفُّ عَلَى الظَّهْرِ وَأَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ غَيْرِهِمَا)) قَالَ:  بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ: ((عَلَيْكَ بِحُسْنِ الْخُلُقِ وَطُولِ الصَّمْتِ فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا عَمِلَ الْخَلائِقُ عَمَلا أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْهُمَا))

 

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokutana na Abuu Dharr alisema: ((Ee Abuu Dharr; je, nikujulishe sifa mbili ambazo ni nyepesi mgongoni mwako na nzito katika kabisa katika Miyzaan kuliko nyinginezo?)) Akasema: “Ndio Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Shikimana na Husnul-Khuluq (tabia njema) na ukae kimya mda mrefu (usiongee upuuzi), kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hakuna 'amali za viumbe Azipendazo Allaah kama hizo mbili)) [Al-Mu’jam Al-Awsatw (7287), At-Targhiyb wat-Tarhiyb ya Al-Mundiriy (3/355) kwa daraja ya Hadiyth Jayyid wasimulizi ni wenye kuaminika]

 

Share