14-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Anayejifunza Au Kufundisha ‘Ilmu Msikitini Yuko Katika Daraja La Mujaahid Fiy SabiliLLaah
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 14
Anayejifunza Au Kufundisha ‘Ilmu Msikitini
Yuko Katika Daraja La Mujaahid Fiy SabiliLLaah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : (مَنْ جَاءَ مَسْجِدِي هَذَا لَمْ يَأْتِهِ إِلَّا لِخَيْرٍ يَتَعَلَّمُهُ أَوْ يُعَلِّمُهُ فَهُوَ بِمَنْزِلَةِ الْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ، وَمَنْ جَاءَ لِغَيْرِ ذَلِكَ فَهُوَ بِمَنْزِلَةِ الرَّجُلِ يَنْظُرُ إِلَى مَتَاعِ غَيْرِهِ)
Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: "Yeyote anayekuja kwenye Msikiti wangu huu, na anakuja tu kwa kusudio zuri, kama vile kujifunza au kufundisha, daraja lake ni kama ya yule Mujaahid fiy SabiliLLaah. Yeyote anayekuja kwa sababu nyingine yoyote, daraja lake ni ya mtu ambaye analinda mali ya watu wengine.” [Ahmad (14/257), Ibn Maajah (223), ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (187)]