An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa): النَّاسِخُ وَالْمَنْسوخ
النَّاسِخُ وَالْمَنْسوخ
An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
A-Muqaddimah (Utangulizi) Wa An-Naasikh Wal-Mansuwkh:
Anaweza akatatizika mtu kuwa nini makusudio ya Aayah hizi na nyingine ambazo zinaonesha kuwa kuna Aayah zinaweza kufutwa ama zimefutwa kwenye Qur-aan ama kubadilishwa na kuwekwa nyingine, ima inayokuja ikafanana na iliyoondoka ama ikawa bora zaidi. La muhimu kwa Muumini ni kwamba asitilie shaka maudhui hii kwa sababu pindi inapokuwa ni jambo la Tawqifiyy (linalotokana na mafunzo na hukmu za Qur-aan na Sunnah) basi Muumini anapaswa kulipokea na kuliamini bila ya kutilia shaka au kulidhania ni mustahili na badala yake kusema:
سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ
“Tumesikia na tumetii.” [Al-Baqarah: 285]
Na Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Amewasifia ‘Ulamaa waliobobea katika ‘Ilmu ya Shariy’ah hii tukufu kuwa, wao huamini moja kwa moja bila ya kutilia shaka yoyote ile. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧﴾
Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu. Na hawakumbuki ila wenye akili [Aal-‘Imraan: 7]
Na dalili za An-Naasikh wal Mansuwkh ni Kauli Zake Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾
Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake. Je, hujui kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza? [Al-Baqarah: 106]
Na pia,
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: Hakika wewe ni mtungaji. Bali wengi wao hawajui. [An-Nahl: 101]
Na pia,
يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ﴿٣٩﴾
Allaah Anafuta yale Ayatakayo na Anathibitisha (Ayatakayo), na Kwake kiko Mama wa Kitabu. [Ar-Ra’d: 39]
Na katika Hadiyth ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ):
حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ يَحْيَى، قَالَ حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ الْحُسَيْنِ بْنِ وَاقِدٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي قَالَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ النَّحْوِيُّ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، فِي قَوْلِهِ :مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا وَقَالَ: وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَكَانَ آيَةٍ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ الآيَةَ وَقَالَ: يَمْحُو اللَّهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ وَعِنْدَهُ أُمُّ الْكِتَابِ فَأَوَّلُ مَا نُسِخَ مِنَ الْقُرْآنِ الْقِبْلَةُ وَقَالَ: وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ ثَلاَثَةَ قُرُوءٍ وَلاَ يَحِلُّ لَهُنَّ أَنْ يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِلَى قَوْلِهِ إِنْ أَرَادُوا إِصْلاَحًا } وَذَلِكَ بِأَنَّ الرَّجُلَ كَانَ إِذَا طَلَّقَ امْرَأَتَهُ فَهُوَ أَحَقُّ بِرَجْعَتِهَا وَإِنْ طَلَّقَهَا ثَلاَثًا فَنَسَخَ ذَلِكَ وَقَالَ: الطَّلاَقُ مَرَّتَانِ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuhusu Kauli Yake Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ
Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake. [Al-Baqarah: 106]
Na Anasema pia Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: Hakika wewe ni mtungaji. Bali wengi wao hawajui. [An-Nahl: 101]
Na Anasema pia Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ﴿٣٩﴾
Allaah Anafuta yale Ayatakayo na Anathibitisha (Ayatakayo), na Kwake kiko Mama wa Kitabu. [Ar-Ra’d: 39]
Basi jambo la kwanza lilofutwa katika Qur-aan lilikuwa ni kuhusu Qiblah. Na Akasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ
Na wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi (na twahara) tatu. Na wala si halali kwao kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa wakitaka suluhu. [Al-Baqarah: 228]
Hivyo basi, ilikuwa pindi mtu alipomtaliki mkewe, alikuwa na haki ya kumrudia mkewe japokuwa alimtaliki mara tatu. Basi (Allaah) Akafuta hiyo na Akasema badala yake:
الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ
Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa shariy’ah au kuachia kwa ihsaan. [Al-Baqarah: 229]
[An-Nasaaiy na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy (3556)]
B-An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa) Ni Kwa Dalili Za Shariy'ah:
Makusudio kamili ya maudhui hii na Aayah zilizotangulia ni Kufuta hukmu ya dalili ya ki-Shariy’ah au kufuta neno la dalili ya ki-Shariy’ah kwa kutumia Qur-aan ama kupitia Sunnah.
Ile inayofuta huitwa An-Naasikh, na inayofutwa inaitwa Al-Mansuwkh. Na jambo hili lipo na linawezekana, na ingawa ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu baadhi ya Aayah (zilotajwa chini kabisa) kama ni An-Naasikh Wal-Mansuwkh, lakini wengi wao wamewafikiana na wametoa dalili nyingi juu ya uwezekano wa hili, zikiwemo Aayah zilizotangulia.
Ama kwenye Hadiyth, ni hii inayoelezea ndoa ya Mut’ah, ambayo ilikuwa halaal kisha ikaja kufutwa baadae ikawa ni haraam:
الرَّبِيعُ بْنُ سَبْرَةَ الْجُهَنِيُّ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنِ الْمُتْعَةِ وَقَالَ " أَلاَ إِنَّهَا حَرَامٌ مِنْ يَوْمِكُمْ هَذَا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَمَنْ كَانَ أَعْطَى شَيْئًا فَلاَ يَأْخُذْهُ "
Rabiy’ bin Sabrah Al-Juhniy (رضي الله عنه), kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliharamisha ndoa ya Mut’ah akasema: “Tanabahini! Hakika hiyo ni haraam kuanzia siku yenu hii mpaka Siku ya Qiyaamah, na yeyote aliyetolea chochote (mahari) basi asirudi kuyachukua.” [Muslim]
Na Riwaayah nyengine:
Sabrah bin Ma’bad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Fat-h Makkah akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut’ah amtaliki na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo].
C-Sharti Za An-Naasikh Wal Mansuwkh:
Ili iweze kuwa An-Naasikh na Al-Mansuwkh, ni lazima kuna masharti ya kuzingatia, na hili ni kutokana na kwamba Naskhu haiwi ispokuwa kwenye Aayah au Hadiyth zinazozungumzia Awaamir (maamrisho) na Nawaahiy (makatazo), na masharti ni kama ifuatavyo:
1-Hukmu inayoondoshwa iwe ya ki-Shariy’ah.
2-Ishindikane kuzifanyia kazi dalili zote mbili kwa wakati mmoja.
3-Dalili itayotumika kuifuta hukmu iwe ni tamko la ki-Shariy’ah ambalo lilichelewa kuja, ukilinganisha na ile iliyofutwa.
Hayo ni baadhi ya masharti ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh.
D-Vigawanyo Vya An-Naasikh Wal-Mansuwkh
An-Naasikh Wal-Mansuwkh ina vigawanyo vinne:
1-Naskhu (kufuta) Aayah Qur-aan kwa Qur-aan (ndio kipengele tunachoelezea zaidi).
2-Naskhu ya Qur-aan kwa Sunnah.
3-Naskhu ya Sunnha kwa Qur-aan.
4-Naskhu ya Sunnah kwa Sunnah.
E-Aina Ya Naskhu Za Qur-aan.
Naskhu kwenye Qur-aan iko ya aina tatu:
1-Kufuta At-Tilaawaah (Usomaji wa Qur-aan) pamoja na Hukmu, na mfano wa hili ni Hadiyth iliyopokelewa na Muslim ikisimuliwa na Mama wa Waumini ‘Aaishah (رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهَا) kuwa katika Aayah zilizoteremshwa ni pamoja na Aayah iliyoelezea kunyonya mara kumi kunamfanya mtu kuwa maharimu yake.
عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ فِيمَا أُنْزِلُ فِي اَلْقُرْآنِ: عَشْرُ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ يُحَرِّمْنَ، ثُمَّ نُسِخْنَ بِخَمْسٍ مَعْلُومَاتٍ، فَتُوُفِّيَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَهِيَ فِيمَا يُقْرَأُ مِنَ اَلْقُرْآنِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Miongoni mwa Aayah za Qur-aan zilizoteremka ilikuwa ni Aayah hii: “Manyonyesho kumi yanayojulikana yanafanya mtu kuwa maharimu wa mnyonyeshaji.” Kisha zikafutwa kwa manyonyesho matano yanayojulikana….” [Muslim]
Baada ya kufutwa Aayah hiyo ikaletwa ya kunyonya mara tano tu, na hizo Aayah mpaka leo hazipo kwenye Mswahafu wa ‘Uthmaaniy.
2-Kufutwa Hukmu na kubakia At-Tilaawah, na mfano wa hili ni:
a) Kuwepo wa Aayah inayozungumzia Eda ya mke aliyefiwa na mumewe kuwa ni mwaka mmoja ilihali hukmu hiyo haitumiki lakini Aayah yake bado ipo na inaendelea kusomwa; nayo ni:
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ
Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. [Al-Baqarah: 240]
Ikabadlishwa kwa:
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ
Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi. [Al-Baqarah: 234]
Wanachuoni wengi wamesema kuwa Aayah (2:240) ilifutwa na Aayah (2:234) kwa lile Alilosema Allaah. “Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi.” (2:234) Mathalan, Al-Bukhaariy alisimulia kuwa Ibn Az-Zubayr alisema: “Nilimwambia ‘Uthmaan bin ‘Affaan Aayah: “Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wawausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa” (2:240), ilifutwa na Aayah (2:234), hivyo basi, kwa nini uliikusanya (ndani ya Qur-aan)? ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) akajibu: Ee mpwa wangu! Sitobadili sehemu yoyote ya Qur-aan kutoka mahala pake.” [Fat-h Al-Baariy (8/48)]
b-Kuweko Aayah inayozungumzia kutoa swadaqah kabla ya kutaka kushauriana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ilhali hukumu hiyo haitumiki lakini Aayah yake bado ipo na inaendelea kusomwa nayo ni:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ۚ
Enyi walioamini! Mnapotaka kushauriana siri na Rasuli basi kadimisheni swadaqah kabla ya mnong’ono wenu. [Al-Mujaadalah: 12]
Ikabadilishwa kwa:
أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٣﴾
Je, mnakhofu kukadimisha swadaqah kabla ya mnong’ono wenu? Ikiwa hamjafanya na Allaah Akapokea tawbah yenu; basi simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Allaah na Rasuli Wake. [Al-Mujaadalah: 13]
3-Kufutwa At-Tilaawah (Usomaji wa Qur-aan) na kubaki hukmu, na mfano wa hii ni Aayah iliyokuja kuzungumzia Ar-Rajmu (kupigwa mawe mzinifu hadi kufa):
الشَّيْخُ وَالشَّيْخَةُ إِذَا زَنَيَا فَارْجُمُوهُمَا الْبَتَّةَ
Aayah hiyo haipo kwenye Mswahafu, ila hukmu yake ndiyo inayotumika hadi sasa, kwamba anaezini ilihali ni Muhswan (aliyeoa ama kuolewa ki Shariy’ah) kuhmu yake ni kupigwa mawe hadi kufa.
F-Hikmah Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh:
Inawezekana katika baadhi ya hikmah kwenye hili ikarejea katika mambo yafuatayo:
1-Kuchunga maslahi ya waja.
2-Uboreshaji wa Shariy’ah kuelekea ukamilifu, pale ilipokuwa ikiboreka Da’wah kwa kutegemeana na hali watu na maisha yao.
3-Mtihani kwa waja juu ya hili, kujaribu Iymaan zao ili kuweza kubaini kuwa watafuata ama watapinga kama ilivyokuwa ni mtihani kuhusu idadi ya Malaika wa Moto katika Kauli ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ
Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika, na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni jaribio kwa wale waliokufuru; ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini; na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini; na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye na Anamuongoa Amtakaye. [Al-Mudath-thir: 31].
4-Kuutakia Umma mambo ya khayr na kuwapa wepesi kwenye maisha yao.
G-Baadhi Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh Katika Qur-aan:
01-Al-Baqarah (109) -At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ
Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete amri Yake. [Al-Baqarah: 109]
An-Naasikh
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo [At-Tawbah: 5]
02-Al-Baqarah (115) - Al-Baqarah (144)
Al-Mansuwkh:
فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ
basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. [Al-Baqarah: 114]
An-Naasikh:
فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ
Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. [Al-Baqarah: 144]
03-Al-Baqarah (180) - An-Nisaa (7)
Al-Mansukwh:
كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ
Mmeandikiwa shariy’ah kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia [Al-Baqarah: 180]
Maelezo:
Aayah hii wamekhitalifiana ‘Ulamaa kuhusu kufutwa kwake na kutofutwa na kuteremshwa baada yake Aayah ya miyraath ya Suwrah An-Nisaa (4: 11-12). Na wengine wamesema kuwa hiyo ni Aayah ya hukmu na haijafutwa, na wengine wameona ni makhsusi na nyingine ni ya jumla. Na wengine wameona imefutwa na Hadiyth ya Abuu Umaamah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah amekwishampatia kila mwenye haki haki yake, basi hakuna wasiyyah kwa mwenye kurithi.” Kwa kifupi, kuna ikhtilaaf ya ‘Ulamaa kuhusu Aayah hiyo katika kauli nne.
An-Naasikh:
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَان
Wanaume wana fungu katika yale waliyoacha wazazi [An-Nisaa: 7]
04-Al-Baqarah (183) - Al-Baqarah (187)
Al-Mansukwh:
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ
Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu [Al-Baqarah: 183]
An-Naasikh:
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ
Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu [Al-Baqarah: 187]
05-Al-Baqarah (184) - Al-Baqarah (185)
Al-Mansukwh:
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ
Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. [Al-Baqarah: 184]
An-Naasikh:
فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ
Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. [Al-Baqarah: 185]
06-Al-Baqarah (191) - Al-Baqarah (193)
Al-Mansukwh:
وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ
Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo. [Al-Baqarah: 191]
An-Naasikh:
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ
Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru). [Al-Baqarah: 193]
07-Al-Baqarah (217) - At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ
Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu kupigana humo. [Al-Baqarah: 217]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo [At-Tawbah: 5]
08-Al-Baqarah (240) - Al-Baqarah (234)
Al-Mansukwh:
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ
Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. [Al-Baqarah: 240]
An-Naasikh:
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ
Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi. [Al-Baqarah: 234]
09-Al-Baqarah (284) - Al-Baqarah (286)
Al-Mansukwh:
وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ
Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. [Al-Baqarah: 284]
An-Naasikh:
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ
Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. [Al-Baqarah: 286]
Maelezo:
Aayah hii na inayofuatia imeteremka kwa sababu, pale ilipoteremka Aayah iliyotangulia;
لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾
Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Baqarah (2:284)]
Ilikuwa ngumu mno kwa Swahaba, wakaogopa mno kuhusu kuhesabiwa vinavyofichika moyoni. Wakakaa kitako wakiwa wameegemea magoti yao wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tumeamrishwa ‘amali tunazoziweza kama Swalaah, Swiyaam, Jihaad, swadaqah, lakini imeteremka kwako Aayah hii wala hatuiwezi! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je mnataka kusema kama walivyosema Ahlul-Kitaab walio kabla yenu waliosema: Tumesikia natumeasi? Bali semeni:
سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia. [Al-Baqarah (2:285)]
Na walipoizoea katika ndimi zao, hapo Allaah Akateremsha:
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake. Na wakasema: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia. [Al-Baqarah (2:285)]
Kisha walipofanya hivyo, Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri. [Al-Baqarah (2:286)] [Muslim kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) na mfano wake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]
10-Aal- ‘Imraan (102) - At-Taghaabun (16)
Al-Mansukwh:
اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ
Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha [Aal- ‘Imraan: 102]
An-Naasikh:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
Basi mcheni Allaah muwezavyo. [At-Taghaabun: 16]
11-An-Nisaa (15-16) - An-Nuwr (2)
Al-Mansukwh:
وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾
Na wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni mashahidi wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine).
وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾
Na wale wawili wanaofanya huo (uchafu) waadhibuni. Wakitubu na kutengenea basi waacheni. Hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 15-16]
An-Naasikh:
الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia. Na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika hukmu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao kundi la Waumini. [An-Nuwr: 2]
Aayah An-Nisaa (4:15): Aayah hii imefutwa hukmu yake kwa Aayah ya kupigwa mijeledi mia moja kwa bikra waliozini, na Hadiyth za rajmi (kuwapiga mawe) waliozini baada ya ndoa (An-Nuwr: Aayah za mwanzo) Imehadithiwa kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Chukueni kutoka kwangu, chukueni kutoka kwangu, Allaah Amekwishawajalia wanawake njia; bikra kwa bikra, wakizini hukmu yao ni kuchapwa mijeledi mia moja, na kutolewa maeneo hayo mwaka mzima, na Ath-Thayyib (aliyekwishaoa au kuolewa) kwa Ath-Thayyib, wakizini hukmu yao ni mijeledi mia moja, na rajmu (kupigwa mawe). [Muslim]
12- An-Nisaa (33) - Al-Anfaal (75)
Al-Mansukwh:
وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ
Na wale mliofungamana nao viapo (vya undugu) basi wapeni fungu lao. [An-Nisaa: 33]
An-Naasikh:
وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ
Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika shariy’ah ya Allaah. [Al-Anfaal: 75]
Hapo mwanzo Muhaajiriyn walipofika Madiynah, Answaar walichukua viapo vya kuungana nao kindugu na kurithiana. Kisha hukmu ya Aayah hii ikafutwa baada ya hukmu ya Aayah (8:75) katika Suwrat Al-Anfaal ambayo ni Kauli Yake Allaah:
وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿٧٥﴾
Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika Shariy’ah ya Allaah. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu
13-An-Nisaa (43) – Al-Maaidah (90 -91)
Al-Mansukwh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ
Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema. [An-Nisaa 43]
An-Naasikh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾
Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni najisi na chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah; basi je mtakoma? [Al-Maaidah 90- 91]
14-An-Nisaa (63) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلًا بَلِيغًا ﴿٦٣﴾
Basi waachilie mbali na wape mawaidha na uwaambie maneno yatakayofikia kuathiri (nafsi zao). [An-Nisaa: 63]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
15-An-Niaa (81) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾
Basi waachilie mbali na tawakali kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Mdhamini Anayetegemewa kwa yote. [An-Nisaa: 81]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
16-An-Nisaa (90-91) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
إِلَّا الَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ أَوْ جَاءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَاتِلُوكُمْ أَوْ يُقَاتِلُوا قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَاتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ﴿٩٠﴾
Isipokuwa wale waliochukua kimbilio kwa watu ambao baina yenu na baina yao mna mkataba au wamekujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao, (hao msiwapige). Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasaliti juu yenu, wakapigana nanyi. Watakapojitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuwekeeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia dhidi yao.
سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَـٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿٩١﴾
Mtawakuta wengine wanaotaka kupata amani kwenu na kupata amani kwa watu wao; kila wanaporudishwa katika fitnah huangushwa humo. Wasipojitenga nanyi na wakakuleteeni amani na wakazuia mikono yao (kukupigeni), basi wachukueni na waueni popote muwapatapo. Na hao Tumekufanyieni hoja zilizo bayana dhidi yao. [An-Nisaa 90-91]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
17-An-Nisaa (92) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ
Na ikiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao. [An-Nisaa: 92]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
18-Al-Maaidah (2) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ
Enyi walioamini! Msikhalifu utukufu wa ishara za Allaah, wala miezi mitukufu [Al-Maaidah: 2]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
19-Al-Maaidah (42) – Al-Maaidah (49)
Al-Mansukwh:
فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ
Basi wakikujia wahukumu baina yao [Al-Maaidah 42]
An-Naasikh:
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ
Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah. [Al-Maaidah 49]
20–Al-Maaidah (106) – Atw-Twalaaq (2)
Al-Mansukwh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ
Enyi walioamini! Mauti yanapomfikia mmoja wenu wakati anapousia, basi chukueni ushahidi wa wawili wenye uadilifu miongoni mwenu; au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi [Al-Maaidah: 106]
An-Naasikh:
وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ
Na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu. [Atw-Twalaaq: 2]
21-Al-An’aam (68) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ
Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika Aayaat Zetu; basi jitenge nao [Al-An’aam: 68]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
22-Al-An’aam (106) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦﴾
Na jitenge na washirikina. [Al-An’aam: 106]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
23-Al-An’aam (141) – At-Tawbah (60).
Al-Mansukwh:
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ
Naye (Allaah) Ndiye Ambaye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yakitofautiana kwa ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake. [Al-An’aam: 141]
An-Naasikh:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ
Hakika Zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (katika Uislamu) na kuwakomboa mateka, na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri (aliyeharibikiwa). [At-Tawbah: 60]
24-Al-Anfaal (1), Al-Anfaal (41).
Al-Mansukwh:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira; sema: ngawira ni ya Allaah. [Al-Anfaal: 1]
An-Naasikh:
وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّـهِ
Na jueni ya kwamba ghanima yoyote mnayoipata (vitani), basi humusi yake ni ya Allaah [Al-Anfaal: 41]
25- Al-Anfaal (61) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَإِن جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا
Na kama (maadui) wakielemea kwenye amani basi nawe ielemee [Al-Anfaal: 61]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
26-Al-Anfaal (65) – Al-Anfaal (66)
Al-Mansukwh:
إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ
Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) ishirini wanaosubiri, basi watawashinda (makafiri) mia mbili. [Al-Anfaal: 65]
An-Naasikh:
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ
Sasa Allaah Amekukhafifishieni [Al-Anfaal: 66]
27-Al-Anfaal (72) – Al-Anfaal (75)
Al-Mansukwh:
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يُهَاجِرُوا مَا لَكُم مِّن وَلَايَتِهِم مِّن شَيْءٍ
Na wale walioamini lakini hawakuhajiri, hamna nyinyi wajibu wa kuwalinda lolote [Al-Anfaal: 72]
An-Naasikh:
وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ
Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika shariy’ah ya Allaah. [Al-Anfaal: 75]
28-At-Tawbah (41) – At-Tawbah (122)
Al-Mansukwh:
انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا
Tokeni mwende mkiwa wepesi na mkiwa wazito. [At-Tawbah: 41]
An-Naasikh:
وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ
Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja (kupigana jihaad). [At-Tawbah: 122]
29-Al-Hijr (85) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ﴿٨٥﴾
Basi samehe msamaha mzuri. [Al-Hijr: 85]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
30-AL-Hijr (94) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿٩٤﴾
na jitenge na washirikina. [Al-Hijr: 94]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
31-An-Nahl (125) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ
Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi. [An-Nahl: 125]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
32-An-Nuwr (3) – An-Nuwr (32)
Al-Mansukwh:
الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً
Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; [An-Nuwr: 3]
An-Naasikh:
وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ
Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume [An-Nuwr: 32]
33-As-Sajdah (30) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ ﴿٣٠﴾
Jiepushe nao na ngojea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wao (pia) wanangojea. [As-Sajdah: 30]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
34- Al-Ahzaab (52) – Al-Ahzaab (50)
Al-Mansukwh:
لَّا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِن بَعْدُ
Si halali kwako wanawake wengine baada ya hao [Al-Ahzaab: 52]
An-Naasikh:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ
Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekuhalalishia wake zako. [Al-Ahzaab: 50]
35- Az-Zumar (41) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ﴿٤١﴾
na wewe si mdhamini wao. [Az-Zumar: 41]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
36-Az-Zukhruf (89) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
Basi wapuuzilie mbali (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na sema: “Salaamun!” Na karibuni hivi watakuja jua. [Az-Zukhruf: 89]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
37-Al-Jaathiyah (14) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّـهِ
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa wale walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji Siku za Allaah [Al-Jaathiyah: 14]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
38-Qaaf (45) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ
na wala wewe si mwenye kuwalazimisha kwa ujabari. [Qaaf: 45]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
39-Adh-Dhaariyaat (54) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ ﴿٥٤﴾
Basi jitenge nao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwani wewe si mwenye kulaumiwa kabisa. [Adh-Dhaariyaat: 5]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
40-An-Najm (29) – At-Tawbah (5)
Al-Mansukwh:
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا
Basi achana mbali na ambaye ameupa mgongo ukumbusho Wetu [An-Najm: 29]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
41-Al-Mujaadalah (12) – Al-Mujaadalah (13)
Al-Mansukwh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ۚ
Enyi walioamini! Mnapotaka kushauriana siri na Rasuli basi kadimisheni swadaqah kabla ya mnong’ono wenu. [Al-Mujaadalah: 12]
An-Naasikh:
أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٣﴾
Je, mnakhofu kukadimisha swadaqah kabla ya mnong’ono wenu? Ikiwa hamjafanya na Allaah Akapokea tawbah yenu; basi simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Allaah na Rasuli Wake. [Al-Mujaadalah: 13]
42-Al-Mumtahinah (10) – At-Tawbah (5)
Al-Manswukh:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ
Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri. [Al-Mumtahinah: 10]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
43-Al-Muzzammil (1-3) – Al-Muzzammil (20)
Al-Manswukh:
يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾
Ee uliyejifunika. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa kidogo tu. Nusu yake, au ipunguze kidogo. [Al-Muzzammil: 1-3]
An-Naasikh:
إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ
Hakika Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Anajua kwamba unasimama (kuswali) karibu na thuluthi mbili za usiku au nusu yake, au thuluthi yake; na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na Allaah Anakadiria usiku na mchana. Anajua kwamba hamuwezi kuukadiria wakati wake na kusimama kuswali, basi Amepokea tawbah yenu. Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan. (Allaah) Anajua kwamba watakuweko miongoni mwenu wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta fadhila za Allaah, na wengineo wanapigana katika njia ya Allaah. Basi someni kile kilicho chepesi humo. [Al-Muzzammil: 20]
44-Al-Muzzammil (10) – At-Tawbah (5)
Al-Manswukh:
وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا﴿١٠﴾
Na subiri juu ya yale wayasemayo, na wahame, mhamo mzuri. [Al-Muzzammi: 10]
An-Naasikh:
فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ
Basi waueni washirikina popote muwakutapo. [At-Tawbah: 5]
Nyenginezo:
Kufutwa hukmu ya Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣﴾
Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Al-Maaidah (5:13)]
Amri ya kuwasamehe baada ya kuvunja kwao ahadi na fungamano na kufanya khiyana, imefutwa na Aayaat za As-Sayf (upanga),
قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ
Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki. [At-Tawbah (9:29)]
kwa kuwa baada ya hapo waliamrishwa kupigana Jihaad na makafiri.
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo zaidi kuhusu sababu ya baadhi ya Aayah kufutwa na kuteremshwa nyenginezo badala yake:
Na Allaah (عزّ وجلّ) Anajua zaidi