A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf

 

A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari

 

‘Abdur-Rahmaan Bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Jina Lake: ‘Abdur-Rahmaan Bin ‘Awf

 

(Al-Qurayshiyy)

 

عبد الرّحمن بن عوف

 

Maana Yake: ‘Abdur-Rahmaan – Mja wa Mwingi wa Rahmah

 

 

Wasifu Wake:

 

 

Katika zama za ujahiliya, jina lake ‘Abdur-Rahman bin ‘Awf   lilikuwa ‘Abdul-K’abah. Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa kwa jina jipya na kumwita ‘Abdur-Rahman.

 

 

Ni Swahaba aliyeshuhudia vita vote alivopigana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alisimama imara na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita va Uhud.

 

 

‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  katika Swahaba kumi waliobashiriwa Jannah.

 

Alikua ni mfano bora na mfuasi wa kweli wa Uislamu ambaye alitoa mali yake kwa wingi katika jihaad fiy SabiliLlaah ikawa ni sababu ya kufikia radhi za Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى)   

 

 

Kufariki Kwake:

 

‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 75, na aliswaliwa Swalaah ya Janaazah na ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).  

 

 

 

Share