05-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Kuteremshwa Mvua Tele Kwa Du’aa Yake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

05-Miujiza Yake:  Kuteremshwa  Mvua Tele Kwa Du’aa Yake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa miujiza aliyojaaliwa nayo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na Rabb wake ni du’aa zake, kwani alikuwa pindi alipoomba jambo basi halirudi bali hutaqabaliwa na hutaqabaliwa kwa miujiza ya kutoka mbinguni.  Watu walipolalamika kuwa kuna ukame wakaomba mvua, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliomba du’aa kwa Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Ateremshe mvua, basi naam! Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Aliteremsha na hali ilikuwa kama inavoelezewa katika Hadiyth ifuatayo:

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَجُلاً، دَخَلَ الْمَسْجِدَ يَوْمَ جُمُعَةٍ مِنْ بَابٍ كَانَ نَحْوَ دَارِ الْقَضَاءِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمًا ثُمَّ قَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُغِيثُنَا" فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا)). قَالَ أَنَسٌ: وَلاَ وَاللَّهِ مَا نَرَى فِي السَّمَاءِ مِنْ سَحَابٍ، وَلاَ قَزَعَةً، وَمَا بَيْنَنَا وَبَيْنَ سَلْعٍ مِنْ بَيْتٍ وَلاَ دَارٍ‏.‏ قَالَ فَطَلَعَتْ مِنْ وَرَائِهِ سَحَابَةٌ مِثْلُالتُّرْسِ، فَلَمَّا تَوَسَّطَتِ السَّمَاءَ انْتَشَرَتْ ثُمَّ أَمْطَرَتْ، فَلاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا، ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ الْبَابِ فِي الْجُمُعَةِ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قَائِمًا فَقَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا"‏.‏  قَالَ:  فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلاَ عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الآكَامِ وَالظِّرَابِ وَبُطُونِ الأَوْدِيَةِ وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ)) ‏ قَالَ: فَأَقْلَعَتْ وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ‏.‏ قَالَ شَرِيكٌ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ أَهُوَ الرَّجُلُ الأَوَّلُ فَقَالَ مَا أَدْرِي‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba mtu mmoja aliingia Masjid siku ya Ijumaa kupitia mlango ulioelekea Daar Al-Qadhwaa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa amesimama akikhutubia. Akasimama mbele ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) kisha akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Wanyama wameteketea na njia zimekatika, basi muombe Allaah Atuteremshie mvua.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akanyanyua mikono akaomba:

اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا

Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa 

Ee Allaah tubarikie kwa mvua

Anas amesema:  Wa-Allaahi hakukuwa na mawingu mbinguni na hakukuwa na nyumba au jengo baina yetu na baina ya mlima wa Sal’i.  Basi wingu kubwa kama ngao lilitokea nyuma yake.  Lilipofika katikati lilienea kisha ikanyesha mvua. Basi wa-Allaahi, hatukuona jua siku sita. Kisha Ijumaa iliyofuatia aliingia mtu kupitia mlango huo huo na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa akikhutubia khutbah ya Ijumaa, akasimama mbele yake akasema: “Ee Rasuli wa Allaah!  Mifugo ya nyama inateketea na njia zimekatika, muombe Allaah Atuzuilie mvua!” Anas akasema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akanyanyua mikono yake akaomba: 

 

اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلاَ عَلَيْنَا

Allaahumma hawaalaynaa walaa ‘alaynaa.”

Ee Allaah! Pembezoni mwetu na si juu yetu. 

Eee Allaah juu ya majabali, na vilimani, na ndani ya mabonde na juu ya sehemu zinazoota miti.”

 

Anas akasema: Mvua ikasita na tukatoka tukitembea katika jua.  Shariyk alimuuliza Anas kama huyo mtu alikuwa ni yule yule wa kwanza? Akajibu kuwa hajui. [Al-Bukhaariy, Kitaab Al-Istisqaa]

 

Na ndio maana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akatunfundisha du’aa zifuatazo zinazohusiana na kuomba mvua hadi inaponyesha.   

 

063-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Istisqaa (Kuomba Mvua)

 

064-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Mvua Inaponyesha

 

064-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Mvua Inaponyesha

 

066-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kutaka Mvua Iondoke (Wakati Itakapoleta Madhara)

 

 

Share