01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuvaa Nguo Nyeupe na Kujuzu Nyekundu, Kijani, Njano, Nyeusi na Kujuzu Nguo ya Pamba, Katani, Sufi na ya Manyoa na Nyinginezo Isipokuwa ya Hariri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب الثوب الأبيض ، وجواز الأحمر والأخضر

والأصفر والأسود ، وجوازه من قطن وكتان وشعر وصوف وغيرها إِلاَّ الحرير

01-Mlango Wa Kupendeza Kuvaa Nguo Nyeupe na Kujuzu Nyekundu, Kijani, Njano, Nyeusi na Kujuzu Nguo ya Pamba, Katani, Sufi na ya Manyoa na Nyinginezo Isipokuwa ya Hariri

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ﴿٢٦﴾

Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi (nguo) inayositiri tupu zenu na libasi ya mapambo. Na libasi ya taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Ishara za Allaah ili wapate kukumbuka. [Al-A'raaf: 26]

 

وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ ﴿٨١﴾

Na Akakujaalieni katika majabali mahali pa kukimbilia na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto na mavazi (ya chuma) yanakukingeni katika vita vyenu. [An-Nahl: 81]

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمْ البَيَاضَ ؛ فَإنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vaeni katika nguo zenu nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu zilizo bora kabisa na pia muwakafini nazo maiti zenu." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 2

وعن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  الْبَسُوا البَيَاضَ ؛ فَإنَّهَا أطْهَرُ وَأطْيَبُ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ )) رواه النسائي والحاكم ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vaeni nguo nyeupe, kwani hizo ni safi na ni nzuri na wakafinini katika hizo wafu wenu." [An-Nasaai na Al-Haakim, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 3

وعن البراءِ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرْبُوعاً ، وَلَقَدْ رَأيْتُهُ في حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مَا رَأيْتُ شَيْئاً قَطُّ أحْسَنَ مِنْهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na amesema Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kati na kati (wa umbo, si mrefu wala si mfupi) na kwa hakika nilimuona katika vazi jekundu, sikuona kabisa kitu kizuri sana kuliko vazi hilo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasai]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي جُحَيفَةَ وَهْب بن عبد الله رضي الله عنه ، قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم بِمكّةَ وَهُوَ بالأبْطَحِ في قُبَّةٍ لَهُ حَمْرَاءَ مِنْ أَدمِ ، فَخَرَجَ بِلاَلٌ بِوَضُوئِهِ ، فَمِنْ نَاضِحٍ وَنَائِلٍ ، فَخَرَجَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وعليه حُلَّةٌ حَمْرَاءُ ، كَأنِّي أنْظُرُ إِلَى بَيَاضِ سَاقَيْهِ ، فَتَوَضّأ وَأذَّنَ بِلاَلٌ ، فَجَعَلْتُ أتَتَبَّعُ فَاهُ هاهُنَا وَهَاهُنَا ، يقولُ يَمِيناً وَشِمَالاً : حَيَّ عَلَى الصَّلاَةِ ، حَيَّ عَلَى الفَلاَحِ ، ثُمَّ رُكِزَتْ لَهُ عَنَزَةٌ ، فَتَقَدَّمَ فَصَلَّى يَمُرُّ بَيْنَ يَدَيْهِ الْكَلْبُ وَالْحِمَارُ لاَ يُمْنَعُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Juhayfah Wahb bin 'Abdillaah: Nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika sehemu ya Abtwahi, karibu na Makkah akiwa katika hema la ngozi nyekundu. Bilaal alikuja na maji kidogo kwa ajili ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kushikia wudhuu. Baadhi walipata maji kidogo na wengine hawana kabisa na wengine walitosheka kupata umande wa kutoka kwa mikono ya wengine. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka akiwa amevaa joho jekundu kama mimi ninaangalia weupe wa miundi yake. Alishika wudhuu na Bilaal akaadhini. Niliendelea kuangalia harakati za uso wa Bilaal akigeuka kuliani na kushotoni huku akisema: "Njooni katika Swalaah, njooni katika kufaulu." Kisha mkuki mdogo uliwekwa mbele na kuswalisha. Alipokuwa anaswalisha mbwa na punda walipita mbele yake na hawakuwa ni wenye kukatazwa. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي رمْثَة رفَاعَةَ التَّيْمِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وعليه ثوبانِ أخْضَرَان . رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح .

Amesema Abu Ramthah Rifaa'ah At-Taymiy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo mbili za kijani. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 6

وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاء . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia siku ya kufunguliwa Makkah akiwa na akiwa na kilemba cheusi." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي سعيد عمرو بن حُرَيْثٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كأنّي أنْظُرُ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وعليه عِمَامَةٌ سَوْدَاءُ ، قَدْ أرْخَى طَرَفَيْهَا بَيْنَ كَتِفَيْهِ . رواه مسلم .

وفي روايةٍ لَهُ : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم خَطَبَ النَّاسَ ، وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاءُ .

Amesema Abu Sa'iyd 'Amruw bin Hurayth (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ni kama mimi namuangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na kilemba cheusi, ncha zake mbili zikiwa kwenye mabega yake." [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyingine: Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahutubia watu akiwa amevaa kilemba cheusi.

 

 

Hadiyth – 8

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كُفِّنَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في ثلاثةِ أثْوَاب بيضٍ سَحُولِيَّةٍ مِنْ كُرْسُفٍ ، لَيْسَ فِيهَا قَمِيصٌ وَلاَ عِمَامَةٌ .متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amevishwa sanda ya nguo tatu nyeupe zisizotengenezwa Sahuuliyyah (aina ya nguo kutoka kijiji hicho cha Yemen) kwa pamba, katika nguo hizo hakukuwa na kanzu wala kilemba." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 9

وعن عائشة رضي الله عنها  ، قالت : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات غَدَاةٍ ، وَعَلَيْهِ مِرْطٌ مرَحَّلٌ مِنْ شَعرٍ أسْوَد . رواه مسلم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Alitoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mchana mmoja akiwa amejifunika na nguo ya manyoa meusi iliyokuwa na picha ya ngamia." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

وعن المغيرة بن شُعْبَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنْتُ مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ذاتَ لَيْلَةٍ في مسير ، فَقَالَ لي : ((  أمَعَكَ مَاءٌ ؟ )) قلتُ : نَعَمْ ، فَنَزَلَ عَنْ رَاحِلَتِهِ فَمَشَى حَتَّى تَوَارَى في سَوَادِ اللَّيْلِ ، ثُمَّ جَاءَ فَأفْرَغْتُ عَلَيْهِ مِنَ الإدَاوَةِ ، فَغَسَلَ وَجْهَهُ وَعَلَيْهِ جُبَّةٌ مِنْ صُوفٍ ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أنْ يُخْرِجَ ذِرَاعَيْهِ مِنْهَا حَتَّى أخْرَجَهُمَا مِنْ أسْفَلِ الْجُبَّةِ ، فَغَسَلَ ذِرَاعَيْهِ وَمَسَحَ بِرَأسِهِ ، ثُمَّ أهْوَيْتُ لأَنْزَعَ خُفَّيْهِ ، فَقَالَ : ((  دَعْهُمَا فَإنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ )) وَمَسحَ عَلَيْهِمَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية : وَعَلَيْهِ جُبَّةٌ شَامِيَّةٌ ضَيِّقَةُ الكُمَّيْنِ .

وفي رواية : أنَّ هذِهِ القَضِيَّةَ كَانَتْ في غَزْوَةِ تَبُوكَ .

Amesema Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Usiku mmoja tulikuwa katika safari pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akaniuliza: "Je, una maji?" Nikasema: "Ndio." Hapo alishuka juu ya kipando chake na kutembea kwenye njia kwa miguu mpaka akatoweka katika giza la usiku. Aliporudi nilimwagia maji kutoka katika chombo, naye akaosha uso wake. Wakati huo alikuwa amevaa juba la sufi na hivyo hakuweza kutoa mikono yake mpaka alipoitoa kutoka katika sehemu ya chini ya hilo juba. Aliosha mikono yake na kupangusa kichwa chake. Kisha nilitaka kumsaidia ili atoe soksi zake, akaniambia: "Ziache kama zilivyo kwani nilizivaa nikiwa katika hali ya tohara na usafi." Hivyo akapangusa juu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Na katika riwaayah: Alikuwaamevaa juba la Kishaam liliokuwa na mikono miwili. 

Na katika riwaayah nyingine: Hakika tukio hili lilitokea katika Vita vya Taabuk.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share