06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kuvaa Hariri kwa Wanaume na Uharamu wa Kukaa Juu Yake na Kuegemea na Kujuzu Kuvaa kwa Wanawake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب تحريم لباس الحرير عَلَى الرجال ، وتحريم جلوسهم

عَلَيْهِ واستنادهم إِلَيْهِ وجواز لبسه للنساء

06-Mlango Wa Uharamu wa Kuvaa Hariri kwa Wanaume na Uharamu wa Kukaa Juu Yake na Kuegemea na Kujuzu Kuvaa kwa Wanawake

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن عمر بن الخَطَّابِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  لاَ تَلْبَسُوا الحَرِيرَ ؛ فَإنَّ مَنْ لَبِسَهُ في الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musivae hariri, hakika mwenye kuvaa duniani hatovaa Aakherah." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasai]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن عمر بن الخَطَّابِ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  إنَّمَا يَلْبَسُ الحَرِيرَ مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية للبخاري : ((  مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ في الآخِرَةِ )) .

Amesema 'Umar Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) akisema: "Hakika anayevaa hariri ni yule asiye na fungu (hatovaa) Aakherah." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasai]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Ni asiye na fungu lake Aakherah."

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ لَبِسَ الحَرِيرَ في الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuvaa hariri duniani hatovaa Aakherah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن علي رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أخَذَ حَريراً ، فَجَعَلَهُ في يَمِينهِ ، وَذَهَبَاً فَجَعَلَهُ في شِمَالِهِ ، ثُمَّ قَالَ : ((  إنَّ هذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُور أُمّتي )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيحٍ .

Amesema 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akichukua hariri na kuiweka mkono wake wa kulia na dhahabu akaishika kwa mkono wake wa kushoto, kisha akasema: "Hakika hivi vitu viwili ni haramu kwa wanaume wa Ummah wangu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي موسى الأشْعَري رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  حُرِّمَ لِبَاسُ الحَرِير وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي ، وَأُحِلَّ لإنَاثِهِمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Imeharamishwa kuvaa hariri na dhahabu kwa wanaume wa Ummah wangu na ikahalalishwa kwa wanawake wao." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 6

وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : نَهَانَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم أنْ نَشْرَبَ في آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ ، وأنْ نَأْكُلَ فِيهَا ، وعَنْ لُبْس الحَريرِ وَالدِّيبَاج ، وأنْ نَجْلِسَ عَلَيْهِ . رواه البخاري .

Amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Ametukataza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha na kula ndani yake na pia kuvaa hariri na dibaji na kukaa juu yake." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 
Share