01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mapenzi Yake: Kwa Swahaba Na Ummah Wake Ambao Hata Hajakutana Nao

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

01-Mapenzi Yake:  Kwa Swahaba Na Ummah Wake Ambao Hata Hajakutana Nao

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَى الْمَقْبُرَةَ فَقَالَ ‏"‏ السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ وَدِدْتُ أَنَّا قَدْ رَأَيْنَا إِخْوَانَنَا ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا أَوَلَسْنَا إِخْوَانَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ ‏"‏ أَنْتُمْ أَصْحَابِي وَإِخْوَانُنَا الَّذِينَ لَمْ يَأْتُوا بَعْدُ ‏"‏ ‏.‏ فَقَالُوا كَيْفَ تَعْرِفُ مَنْ لَمْ يَأْتِ بَعْدُ مِنْ أُمَّتِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَقَالَ ‏"‏ أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ رَجُلاً لَهُ خَيْلٌ غُرٌّ مُحَجَّلَةٌ بَيْنَ ظَهْرَىْ خَيْلٍ دُهْمٍ بُهْمٍ أَلاَ يَعْرِفُ خَيْلَهُ ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّهُمْ يَأْتُونَ غُرًّا مُحَجَّلِينَ مِنَ الْوُضُوءِ وَأَنَا فَرَطُهُمْ عَلَى الْحَوْضِ أَلاَ لَيُذَادَنَّ رِجَالٌ عَنْ حَوْضِي كَمَا يُذَادُ الْبَعِيرُ الضَّالُّ أُنَادِيهِمْ أَلاَ هَلُمَّ ‏.‏ فَيُقَالُ إِنَّهُمْ قَدْ بَدَّلُوا بَعْدَكَ ‏.‏ فَأَقُولُ سُحْقًا سُحْقًا ‏

 

Amesimulia Abuu Hurayarah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alifika makaburini akasema:

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ

 

Assalaamu ‘alaykum watu wa nyumba za Waumini, nasi In Shaa Allaah tutakutana nanyi.

 

Natamani kuwaona ndugu zangu.” Wakasema (waliosikia):  Je, kwani sisi sio nduguzo ee Rasuli wa Allaah? Akasema:  “Ninyi ni Swahaba zangu na ndugu zetu ni wale ambao, hadi sasa, hawajaja ulimwenguni. Wakasema: Ni vipi utamtambua yule ambaye bado hajakuja katika Ummah wako ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Niambieni, lau kama mtu ana farasi wenye alama usoni na miguuni wakawa baina ya farasi weusi wasio na mabaka, je hawezi kuwatambua farasi wake?”  Wakasema: Ndio, atawatambua ee Rasuli wa Allaah. Akasema:  “Basi wao watakuja nailhali wana nuru nyusoni, miguuni na mikononi kutokana na wudhuu. Na mimi ndiye nitakayewatangulia kwenye Al-Hawdh (Hodhi)  Basi jueni kwa yakini kwamba watu watazuiliwa na kufukuzwa wasije kwenye Hawdh langu kama wanavyozuiliwa ngamia wasio na mchunga. Nitawaita: Haya njooni! Patasemwa: “Hakika hao walibadili baada yako.” Nitawaambia: Poteleeni mbali kabisa!” [Muslim]

 

 
 

Share