13-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kupeana Mikono Mnapokutana na Kufurahi na Kuubusu Mkono wa Mcha Mungu (na Mwema) na Kubusu Mtoto Kudhihirisha Mapenzi na Kumkumbatia Anayetoka Safari na Karaha ya Kuinamisha Kichwa Mbele Yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب استحباب المصافحة عِنْدَ اللقاء وبشاشة الوجه وتقبيل يد الرجل الصالح وتقبيل ولده شفقة ومعانقة القادم من سفر وكراهية الانحناء

13-Mlango Wa Kupendeza Kupeana Mikono Mnapokutana na Kufurahi na Kuubusu Mkono wa Mcha Mungu (na Mwema) na Kubusu Mtoto Kudhihirisha Mapenzi na Kumkumbatia Anayetoka Safari na Karaha ya Kuinamisha Kichwa Mbele Yake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي الخطاب قتادة ، قَالَ : قُلْتُ لأَنَسٍ : أكَانَتِ المُصَافَحَةُ في أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : نَعَمْ . رواه البخاري .

Amesema Abil Khatwaab Qataadah (Radhwiya Allahu 'anhu): Nilimuuliza Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Je, Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakisalimiana kwa kupeana mikono?" Akasema: "Ndio." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ: لَمَّا جَاءَ أهْلُ اليَمَنِ، قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قَدْ جَاءكُمْ أهْلُ اليَمَنِ )) وَهُمْ أوَّلُ مَنْ جَاءَ بِالمُصَافَحَةِ. رواه أَبُو داود بإسناد صحيح.

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walipokuja watu kutoka Yemen, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Wamekujieni watu wa Yemen, na wao ndio wa kwanza kuanzisha (kusalimiana kwa) kupeana mikono." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 3

وعن البراءِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مُسْلِمَينِ يَلْتَقِيَانِ فَيَتَصَافَحَانِ إِلاَّ غُفِرَ لَهُمَا قَبْلَ أنْ يَفْتَرِقَا )) رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aesema: "Hakuna Waislaamu wawili wanaokutana na kupeana mikono isipokuwa wanasamehewa kabla ya kuachana." [Abu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَجُلٌ : يَا رسولَ اللهِ ، الرَّجُلُ مِنَّا يَلْقَى أخَاهُ، أَوْ صَدِيقَهُ، أينحَنِي لَهُ ؟ قَالَ : (( لاَ )) . قَالَ : أفَيَلْتَزِمُهُ وَيُقَبِّلُهُ ؟ قَالَ : (( لاَ )) قَالَ : فَيَأخُذُ بِيَدِهِ وَيُصَافِحُهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Mtu mmoja aliuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Mtu anakutana na nduguye au rafiki yake, je, amuinamie (kama ishara)?" Akasema: "Laa." Akauliza tena: "Je, amsalimie kwa kumpa mkono?" Akasema: "Ndio." [At-Tirmdhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 5

وعن صَفْوَانَ بن عَسَّالٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ يَهُودِيٌّ لِصَاحِبِهِ : اذْهَبْ بِنَا إِلَى هَذَا النَّبيِّ ، فَأتَيَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَسَألاهُ عَنْ تِسْعِ آياتٍ بَيِّنَاتٍ ... فَذَكَرَ الْحَدِيث إِلَى قَوْلهِ : فقَبَّلا يَدَهُ وَرِجْلَهُ ، وقالا : نَشْهَدُ أنَّكَ نَبِيٌّ . رواه الترمذي وغيره بأسانيد صحيحةٍ .

Imepokewa kwa Swafwaan bin 'Assaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alisema Myahudi kwa sahibu yake: "Tupeleke kwa Nabiy huyu." Wakamjia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakamuuliza ishara tisa za wazi (Hizi ni zile alizopatiwa Nabiy Muwsaa 'Alayhis Salaam); Akataja Hadiyth hadi kauli yake: Basi wakaubusu mkono wake na mguu wake, wakasema: "Tunashuhudia kwamba wewe ni Nabiy." [At-Tirmidhiy na wengineo kwa Isnaad zilizo Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عمر رضي الله عنهما قِصَّة ، قَالَ فِيهَا : فَدَنَوْنَا مِنَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَبَّلْنَا يَدَه . رواه أَبُو داود .

Na kutoka Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amehadithia ndani yake: Mwisho wa kisomo tulifika karibu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuubusu mkono wake." [Abuu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 7

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَدِمَ زَيْدُ بْنُ حَارِثَةَ المَدِينَةَ وَرسولُ الله صلى الله عليه وسلم في بَيتِي ، فَأتَاهُ فَقَرَعَ البَابَ ، فَقَامَ إِلَيْهِ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يَجُرُّ ثَوْبَهُ ، فَاعْتَنَقَهُ وَقَبَّلَهُ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba alifika Zayd bin Al-Haarithah Madiynah na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yupo nyumbani kwangu. Alikuja na kugonga mlango, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye aliinuka kwenda kumpokea kwa haraka huku anaburuza nguo yake, akamkumbatia na kumbusu." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تَحقِرَنَّ منَ الْمَعرُوف شَيْئاً ، وَلَوْ أنْ تَلْقَى أخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musichukie jema lolote hata ikiwa ni kukutana na ndugu yako kwa uso wa tabasamu na bashasha." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَبَّلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الحَسَنَ بنَ عَلِيٍّ رضي الله عنهما ، فَقَالَ الأقْرَعُ بن حَابِسٍ : إنَّ لِي عَشْرَةً مِنَ الْوَلَدِ مَا قَبَّلْتُ مِنْهُمْ أحَدَاً . فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لاَ يَرْحَمْ لاَ يُرْحَمْ ! )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbusu Al-Hasan bin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) na Aqra' bin Haabis akiwa pamoja naye. Aqra' akasema: "Hakika mimi nina watoto kumi lakini sijambusu hata mmoja kati yao." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwangalia, na kisha kusema: "Yeyote asiyewarehemu (wenzake) basi harehemewi (na Allaah)." [Al-Bukhaary na Muslim]

 

 

 

Share