09-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kinachosemwa kwa Mtu Anayekaribia Kufa na Wanayoambiwa Wafiwa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب ما يقال عند الميت وَمَا يقوله من مات له ميت
09-Mlango Wa Kinachosemwa kwa Mtu Anayekaribia Kufa na Wanayoambiwa Wafiwa
Hadiyth – 1
عن أُم سَلَمة رضي اللهُ عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا حَضَرتُمُ المَرِيضَ أَو المَيِّتَ ، فَقُولُوا خَيْراً ، فَإنَّ المَلائِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ )) ، قالت: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سلَمة، أتَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فقلت : يَا رسولَ الله ، إنَّ أَبَا سَلَمَة قَدْ مَاتَ، قَالَ : (( قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ، وَأعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبى حَسَنَةً )) فقلتُ ، فَأعْقَبنِي اللهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ : مُحَمَّداً صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم هكَذا : (( إِذَا حَضَرتُمُ المَريضَ ، أَو المَيِّتَ )) ، عَلَى الشَّكِّ ، ورواه أَبُو داود وغيره : (( الميت )) بلا شَكّ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtakapo kuwepo mahali alipo mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo ya kheri kwani Malaaikah huitikia Aamiyn kwa hayo mnayoyasema." Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Alipoaga dunia Abu Salamah nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Abu Salamah ameaga dunia." Akasema: "Sema: "Allaahummaghfirli wa lahu wa A'qibniy minhu 'uqbaa hasanah (Ee Mola nisamehe na umsamehe yeye na unipatie mimi mbadala mwema)." Nikaomba dua hiyo na Allaah akanibadilishia kwa aliye bora kuliko yeye (yaani Abu Salamah), naye ni Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]. Na imenukuliwa hivi "Mtakapo kuwepo mahali alipo mgonjwa" au "maiti" juu ya shaka, lakini amepokea Abu Daawuwd na wengineo: "Maiti", bila ya shaka yoyote.
Hadiyth – 2
عن أُم سَلَمة رضي اللهُ عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ تُصيبُهُ مُصِيبَةٌ ، فَيَقُولُ : إنّا للهِ وَإنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ، اللَّهُمَّ أُجِرْنِي في مُصِيبَتي وَاخْلفْ لِي خَيراً مِنْهَا ، إِلاَّ أَجَرَهُ اللهُ تَعَالَى في مُصِيبَتِهِ وَأخْلَفَ لَهُ خَيْراً مِنْهَا )) قالت : فَلَمَّا تُوُفِّيَ أَبُو سَلَمَة قلتُ كَمَا أمَرَني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَأخْلَفَ اللهُ لِي خَيْراً مِنْهُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم .
Kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: Nimmsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Hakuna mtu anayepatwa na msiba na akasema: Hakika sisi ni wa Allaah, na kwake tunarudi. Ee Mola nilipe katika msiba wangu, na nipe mbadala bora zaidi yake", isipokuwa atalipwa na Allaah katika msiba wake huo na atampatia mbadala bora kuliko hiyo." Akasema: "Alipofariki Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema kama alivyoniamuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na Allaah akanipa mbadala bora kuliko yeye yaani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي موسى رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا مَاتَ وَلَدُ العَبْدِ ، قَالَ اللهُ تَعَالَى لِمَلائِكَتِهِ : قَبَضْتُمْ وَلَدَ عَبْدِي ؟ فيقولونَ : نَعَمْ . فيقولُ : قَبَضْتُمْ ثَمَرَة فُؤَادِهِ ؟ فيقولونَ : نَعَمْ . فيقولُ : مَاذَا قَالَ عَبْدِي ؟ فيقولونَ : حَمدَكَ وَاسْتَرْجَعَ . فيقول اللهُ تَعَالَى : ابْنُوا لِعَبْدِي بَيْتاً في الجَنَّةِ ، وَسَمُّوهُ بَيْتَ الحَمْدِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokufa mtoto wa mja, Allaah anauliza Malaaikah wake: "Mmefisha mtoto wa mja wangu?" Wanasema: "Ndio." Atasema: 'Mja wangu amesema nini?' Watasema: 'Amekuhimidi na akarejea, Atasema Allaah Ta'aalaa: 'Mjengeeni mja wangu nyumba Peponi, na iiteni Nyumba ya Kuhimidiwa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يقولُ اللهُ تَعَالَى : مَا لِعَبْدِي المُؤمِن عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أهْل الدُّنْيَا ، ثُمَّ احْتَسَبَهُ إِلاَّ الجَنَّةَ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa, husema, 'Hakika mja Wangu Muumini ambaye anasubiri na akwa na matarajio ya thawabu pindi Ninapomchukua kipenzi chake katika watu wa dunia isipokuwa ni kumuingiza Peponi." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن أسَامَة بن زَيدٍ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : أرْسَلَتْ إحْدى بَنَاتِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم إِلَيْهِ تَدْعُوهُ وَتُخْبِرُهُ أنَّ صَبِيَّاً لَهَا – أَوْ ابْناً – في المَوْتِ فَقَالَ للرسول : (( ارْجِعْ إِلَيْهَا ، فَأخْبِرْهَا أنَّ للهِ تَعَالَى مَا أخَذَ وَلَهُ مَا أعْطَى ، وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِأجَلٍ مُسَمّى ، فَمُرْهَا ، فَلْتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ )) ... وذكر تمام الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) "Bint ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma mtu kuja kumuita Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani mtoto wake alikuwa katika utangulizi wa mauti." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma salamu kwake na ujumbe ufuatao: "Kwa hakika mikononi mwa Allaah zipo Anazochukuwa na zile Anazotoa. Na kila kitu Kwake kina wakati maalumu, hivyo asubiri na atarajie thawabu (kutoka kwa Allaah)..." Na akataja Hadiyth kwa ukamilifu wake. [Al-Bukhaariy na Muslim]